Petro Bwimbo mzalendo aliyemuokoa Nyerere asiuliwe na waasi mwaka 1964

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Usiku wa manani Jumapili, tarehe 19 Januari 1964, Bw. PETRO BWIMBO, aliyekuwa Mlinzi Mkuu wa Rais JK NYERERE, alionesha ushujaa na uzalendo wa hali ya juu baada ya wanajeshi wa Tanganyika Rifles wa Colito barracks kuasi.

Usiku huo, kikundi cha wanajeshi 25 kikiwa "Fullmassnondo" kikiongozwa na Sajenti FRANCIS HINGO ILOGI, aliyejipachika cheo cha Brigedia, kikaondoka Colito na kikaenda Ikulu.

Bw. LEON KAZIMIR, aliyekuwa mlinzi wa zamu Ikulu usiku huo, alimpigia simu Bw. BWIMBO saa 8.00 usiku kumjulisha kuhusu maasi hayo baada ya kuwa amepigiwa simu na Kiongozi mzungu wa Tanganyika Rifles, PATRICK SHOLTO DOUGLAS. Bw. BWIMBO, aliyekuwa akiishi Upanga, alifika Ikulu kwa Mercedes Benz yake TD 5067 saa 8.20 na kuwakuta Rais NYERERE na Waziri Mkuu Mh. RASHID MFAUME KAWAWA, aliyekuwa akiishi jirani na ikulu wakiwa Ikulu, wameamshwa na KAZIMIR. Muda mfupi baadae, Mkuu wa Usalama EMILIO CHARLES MZENA na Mkuu wa Polisi, ELANGWA SHAIDI nao pia waliwasili Ikulu.

Hata hivyo, hakukuwa na yeyote aliyejua nini kifanyike kuwaokoa viongozi hao. Hivyo, Bw. BWIMBO "akatia akili mukichwa"na kuamua kutumua ujuzi aliosomea Marekani 1963 kuwaokoa viongozi hao. Saa 8.45, huku kukiwa giza totoro, akawatorosha viongozi hao kupitia mlango wa nyuma (Obama drive) na kwenda nao feri ambapo MZENA na SHAIDI wao walibaki Ikulu.

Bw. BWIMBO aliwadanganya wafanyakazi wa kivuko cha Magogoni kuwa anataka kuwawahisha viongozi hao Chuo cha chama Kivukoni kwenye kikao cha dharura hivyo wakavushwa haraka. Lengo lake lilikuwa ni kuwapeleka "Government rest house" huko Mji mwema, Kigamboni ambako NYERERE alipenda kupumzika wikiendi.

Walitembea kwa miguu huku mbwa wakiwabwekea hadi kufika kijiji cha Salanga ambapo waliamua kulala nyumbani kwa msamaria mwema, Bw. SULTAN KIZWEZWE, kwani tayari kulikaribia kukucha. Bw. KIZWEZWE alikuja kupewa zawadi ya baiskel na serikali baada ya kukataa kujengewa nyumba kwani aliona kuwahifadhi viongozi hao ulikuwa mchango wake kwa Taifa lake!.

Wanajeshi waasi baada ya kumkosa Rais NYERERE Ikulu, kesho yake walimpata Mh. OSCAR SATIEL KAMBONA aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na kwenda nae Carito(Lugalo-jina hili ilikuwa ni kumuenzi Mnyalukolo Chief Mkwawa aliyepigana na Wajerumani huko Lugalo, Iringa).

Waasi hao walidai wameamua kuasi kwavile uhuru haujasaidia chochote kwani nafasi zote za juu bado zilikuwazinashikwa na Wazungu na mishahara yao ilikuwa ni midogo.

Mjini kukawa na mtafaruku mkubwa jijini ambapo kulikuwa na ghasia na uporaji uliofanywa na waasi na vibaka hasa Kariakoo na Magomeni ambapo maduka kadhaa yalivunjwa.

Mwarabu mmoja wa Magomeni, baada ya kuona waasi wakipora dukani kwake, "alimuwasha shaba" muasi mmoja aliyeitwa KASSIM. Koplo NASHON MWITA , alipoona hivyo, akarudi Carito kujizatiti ambapo alirudi na kumi la wenzake wakammiminia risasi mwarabu huyo na kisha "kutia kibiriti" duka lake na kupelekea watu 8, akiwemo mtoto wa miaka 6, kuteketea.

Kukawa na mtafaruku na kimuhemuhe kikubwa jijini huku wananchi wengi wakiogopa kutoka nje na huku wakiwa na wasiwasi juu ya usalama wa Rais wao na viongozi. Tarehe 20 Januari 1964 maasi hayo yakasambaa hadi kambi ya Tabora na tarehe 21 Januari 1964 yalifika kambi ya Nachingwea ambayo ndio kwanza ilikuwaimeanzishwa ikiongozwa na Meja TEMPLE MORRIS.

Baada ya siku 2, Mh. BHOKE MUNANKA, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, aliweza kufika kijiji cha Salanga na kuonana na Rais NYERERE na KAWAWA ambao muda wote walijibanza ndani ili wasionekane.

Jumatano, tarehe 22 Januari 1964, viongozi hao, kwa msaada wa BWIMBO, walirudi Ikulu baada ya kuhakikishiwa hali imetulia kidogo. Rais NYERERE alitoa hotuba fupi ya dakika 3 kuwataka wananchi watulie:-

"Ndugu wananchi, kuna uzushi kuwa Mimi na viongozi hatupo na serikali haipo. Huo ni uzushi na muupuuze".

Alhamis, tarehe 23 Januari 1964, Rais NYERERE aliongea na waandishi wa habari na kuwaeleza uasi huo hauna uhusiano na mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 na wananchi watulie. Aidha, kulikuwa na uzushi mitaani kuwa Mh. KAMBONA anahusika na uasi huo. Hiyo ilipelekea Mh. WILLIAM LEONHART(Balozi wa Marekani) na Mh. STEPHEN MILES(Kaimu Balozi wa Uingereza) waende Ikulu kwa Rais NYERERE kupata ukweli ambapo aliwajibu:-

"Poor Oscar had always been unlucky in that people were always saying he was trying to outst the President. Oscar broke down and wept as a result of the baseless allegations."

Rais NYERERE akiwa na Mh. JOB LUSINDE MALECELA, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, walitembelea maeneo kadhaa jijini hasa Kariakoo kujionea hali halisi kwa kutumia Land rover.

Ijumaa, tarehe 24 Januari 1964, hali ilikuwa 'vururuvururu" na ghasia tupu kambini Colito na wanajeshi waligoma hata kuvaa "uniform". Rais NYERERE, Mh.KAWAWA, Mh.LUSINDE na Mh. KAMBONA wakawa na kikao kizito Ikulu. kwa moyo mzito, Rais NYERERE akaamua kuomba msaada kwa Waingereza. Kwake hii ilikuwa ni aibu kubwa kwani mwaka 1961 alikuwaamewakoga kuwa warudi baada ya miaka 10 wajionee Tanganyika iliyoyafanya ambayo wao Waingereza waliyashindwa.

Saa 8.45 alasiri tarehe 24 Januari 1964, Mh.KAMBONA na Mh PAUL BOMANI, aliyekuwa Waziri wa Fedha, waliwakilisha barua nyumbani kwa Mh. FRANK STEPHEN MILLES, aliyekuwa Kaimu Balozi wa Uingereza isemayo:-

"Your Excellency, I am directed by President of the United Republic of Tanganyika to approach the British Government with a request for military assistance...." . Barua hiyo iliandikwa na kusainiwa kwa mkono na Mh. KAWAWA, baada ya kuelekezwa na Rais NYERERE, ikiwa na maandishi TOP SECRET.

Rais NYERERE, baada ya hapo, akaenda ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu kutoa mada ya "The Hammarskjold Memorial Lecture" kama vile hamna kilichotokea!.

Kesho yake, tarehe 25 Januari 1964,Kikosi cha makomandoo 45 kilitia nanga na chopa likawapeleka hadi Carito. Huko, chini ya BRIGEDIA PATRICK SHOLTO DOUGLAS, walionesha "shoo ya kibabe" kwa kulipua lango la mbele na kisha mtiti wa nguvu ukazuka. Waasi 3 wakauawa, 20 wakajeruhiwa, 400 wakakamatwa na wengine wakaamua "kusepa na kula kona".

Jioni hiyohiyo, Rais NYERERE akalihutubia Taifa kupitia Tanganyika Broadcasting Cooperation akisema:

"Ndugu wananchi, jana nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza na bahati akakubali. Asubuhi hii kikosi cha kwanza kikawasili na kimefanya kazi nzuri na sasa hali ni shwari. Naskia maneno ya wajinga eti sasa Waingereza wamerudi Tanganyika. Ujinga mtupu. Hata hivyo, askari wetu wametuvua nguo. Tupo uchi.......".

Baada ya hapo hali nchini ikatulia.

Tarehe 16 Februari 1964, Rais NYERERE aliitisha mkutano mkubwa Jangwani na kusema:-

"Wanajeshi walioasi walidanganywa. Wendawazimu walikuwa wawili, watatu. Wale wengine walivutishwa bangi na kusombwa kuja mjini kufanya uporaji. Tukaenda kwa Mwingereza kumwambia "Bwana Mwingereza tusaidie kuondoa balaa hili. Mwingereza maana, akatusaidia. Sasa tuko salama".

Baada ya hapo, hatua mbalimbali zilichukuliwa.

Jumanne ya tarehe 21 Aprili 1961, Rais NYERERE alimuapisha Sir RALPH WILDHAM kuwa Jaji Mkuu wa Tanganyika na kumwambia awashughulikie kikamilifu na mara moja wahuni wote waliofanya maasi.

Rais NYERERE akawateua vijana wadogo wazalendo CAPT. ABDALLAH TWALIPO(35) na CAPT LUKIAS SHAFTAEL(39) kuwa wajumbe wa Mahakama ya Kijeshi huku Jaji Mkuu akiwa Rais wake.

DPP Mzimbabwe, HERBERT WILTSHERE CHITEPO, akatangaza washtakiwa watafikishwa kortin jumatatu ya tarehe 27 April 1964 na kwamba mashahidi 25 watatoa ushahidi.

Kesi hiyo ilipelekwa "nginjanginja" na tarehe 15 Mei 1964, hukumu zikatolewa. Sajenti ILONGI, Kiongozi wa maasi hayo, alipigwa "mvua" 15, waasi 10 walipigwa "mvua" 10 na wengine 2 walipigwa "mvua" 5 wakati washtakiwa 5 waliachiwa huru.

Wanajeshi wa Uingereza walikaa nchini hadi Machi 1964. Siku ya kuwaaga makamandoo hao chini ya Lt Col. CARTER , Rais NYERERE na Mh. KAMBONA walitilia suti zao nadhifu nyeusi huku Mh. KAWAWA akiwa amevalia suti ya brauni na wakawashukuru wanajeshi hao kwa kazi nzuri. Wanajeshi wa Nigeria walikuja kuchukua nafadi zao na kukaa hadi Septemba 1964.

Kwa hakika, Bw. BWIMBO, aliyezaliwa tarehe 4 Machi 1929 Ukerewe, alifanya ushujaa na uzalendo wa hali ya juu usiku wa tarehe 19 Januari 1964 siku ambayo Rais NYERERE aliiita "Siku ya aibu sana kwa Taifa letu". Ndio maana mwaka 1985, Bw BWIMBO alipewa medali ya ushupavu(Gallantry Medal).

Uasi huu ndio uliopelekea kuundwa kwa jeshi jipya lililoitwa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo tunalo sasa likifanya majukumu yake kwa nidhamu, utii, uzalendo, uadilifu na ufanisi wa hali ya juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Walitembea kwa miguu huku mbwa wakiwabwekea hadi kufika kijiji cha Salanga ambapo waliamua kulala nyumbani kwa msamaria mwema, Bw. SULTAN KIZWEZWE, kwani tayari kulikaribia kukucha. Bw. KIZWEZWE alikuja kupewa zawadi ya baiskel na serikali baada ya kukataa kujengewa nyumba kwani aliona kuwahifadhi viongozi hao ulikuwa mchango wake kwa Taifa lake!. "

Huo uzalendo ulisha enzi hizo za Nyerere tu sasa hivi kila mtu ni mwizi tu hata viongozi wanajali familia na ndugu zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kw kutujuza.lkn ilikuja kutokeaje nyerere na kambona wakahitilafiana?? Na ilikuwaje kambona aliikimbia nchi na kwenda uhamishoni uingereza??? Lkn pia mtoto wa kambona alipigwa risasi ktkt ya jiji la london akiishuka kwenye gari yake kuingia kwenye duka la vito.je nani alihusika na hayo mauaji?? Na nani alikuwa nyuma ya hayo mauaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe wajeda wa zamani walikuwa wanajiellewa, huwezi kunyonyaaa kisha ukanyonyaaa watu wanakuchekea tu.
 
Ninaposema kuwa hili ni jamvi adhimu maana yake ni hii.
 
Bandiko zuri, tatizo mwandishi kuna mahali katumia lugha za kihuni! Mfano eti wakapigwa mvua. Andishi nyeti kama hili hizo lugha siyo!!!!!!!!!
 
"Bwana Mwingereza tusaidie kuondoa balaa hili. Mwingereza maana, akatusaidia. Sasa tuko salama"

"Eti Bwana Mwingereza".....hahahaaa
 
Ahsante kw kutujuza.lkn ilikuja kutokeaje nyerere na kambona wakahitilafiana?? Na ilikuwaje kambona aliikimbia nchi na kwenda uhamishoni uingereza??? Lkn pia mtoto wa kambona alipigwa risasi ktkt ya jiji la london akiishuka kwenye gari yake kuingia kwenye duka la vito.je nani alihusika na hayo mauaji?? Na nani alikuwa nyuma ya hayo mauaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa natamani sana kuipata hii history kwa ukamilifu wake! Kuna mahali nilisoma kuwa hata wale walioasi wakateka ndege kule mwanza walipofika Uingereza aliyewatuliza wakakubali kujisalimisha alikuwa Kambona baada ya barozi kushindwa!

Kambona inaonekana alikuwa wa muhimu kwa wanajeshi!

Wajuzi wa hizi story muhimu hebu tupeni ukweli maana kwa sasa hazina madhara yoyote zaidi ya kutupa mafunzo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale jahazi linapozama,beberu hugeuka malaika hata kwa Africanist wa aina ya Nyerere pamoja na suluba walizowahi kumpatia.

Historia nzuri.
 
Ahsante kw kutujuza.lkn ilikuja kutokeaje nyerere na kambona wakahitilafiana?? Na ilikuwaje kambona aliikimbia nchi na kwenda uhamishoni uingereza??? Lkn pia mtoto wa kambona alipigwa risasi ktkt ya jiji la london akiishuka kwenye gari yake kuingia kwenye duka la vito.je nani alihusika na hayo mauaji?? Na nani alikuwa nyuma ya hayo mauaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa natamani sana kuipata hii history kwa ukamilifu wake! Kuna mahali nilisoma kuwa hata wale walioasi wakateka ndege kule mwanza walipofika Uingereza aliyewatuliza wakakubali kujisalimisha alikuwa Kambona baada ya barozi kushindwa!

Kambona inaonekana alikuwa wa muhimu kwa wanajeshi!

Wajuzi wa hizi story muhimu hebu tupeni ukweli maana kwa sasa hazina madhara yoyote zaidi ya kutupa mafunzo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninapenda kujua zaidi pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom