Petrol station zinatumia mfumo kwa kadi

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,296
Reaction score
12,972
Hamjamboje wanajamvi

Naomba kufahamu ni vituo gani vya mafuta (Petrol station) vinavyotumia mfumo wa kadi na visivyo na usumbufu? Pia isiyochakachua pump zao. Mfano unahitaji kuwekea kadi yako sh. 100,000/- kisha ukawa unafika kituo cha mafuta wanakata kwenye kadi mpaka hapo itakapokwisha then unatop up.

Natanguliza shukrani

CL
 
Puma
Engene
Total

Mbadala tumia Mastercard tu.
 
Laki moja mbona ndogo sana, depositi 300-500kpm. Lake oil/Total wako poa
 
Badala ya kuhangaika na fuel cards , kwa nini usitumie kadi ya benki kununua mafuta ? Ie master card au visa card
Tunakoelekea vituo vingi vya matuta vita adopt mfumo wa malipo kwa bank card kirahisi kuliko ku implement fuel cards,
Moja ya faida ya fuel card ni kuwa kunakuwa na discount kwenye bei za mafuta, ila nachukia kuwa inabidi kuwe na namna ya kuijaza balance hiyo card ambayo in most cases itakuwa ni benki.
 
Sure na mimi ndio nilivoshauri. La Mastercard usitegemee utauziwa kwa bei ile ile. Kuna charges za bank na transactions.
Kwahiyo possibly ukanunua mafuta Petrol lita moja kwa 2500 au zaidi.

Ila kwa fuel card unapunguza gharama nadhani lita moja kwa 2100 au less.

 
Hapana mkuu," point of sales "( Pos) , hukatwi chochote zaidi ya kiwango tajwa ,

Kwa mfano umeenda puma kununua lets say diesel, ambayo bei yake labda ni 2300 tshs kwa lita , utakapofanya malipo kununua hiyo lita utakatwa 2300 tu, hakunaga charges zozote kwenye pos , ni cheap kuliko hata kutoa hela Atm.
 
Sijawahi kufikiria hivo boss. Mawazo yangu unakatwa na service charges.
 
upande wa Total nikihitaji card napataje? na je ile card inatumika kwa vituo vyote mfano total,puma n.k au kama ni ya total ni total tu peke yake? nimekuwa mpenzi wa kununua petrol ya total pekee.
 
upande wa Total nikihitaji card napataje? na je ile card inatumika kwa vituo vyote mfano total,puma n.k au kama ni ya total ni total tu peke yake? nimekuwa mpenzi wa kununua petrol ya total pekee.
Sijui procedures za kupata hizo fuel cards , lakini nafahamu kuwa haziingiliani, ie ya puma utatumika puma na ya total itatumika total
 

Mastercard ninayo ila sihutaji kuitumia kwa matumizi hayo... Ninataka ikifika mwisho wa mwezi ninaweka pesa fixed kwa ajili ya fuel pekee... ile mastercard itanifanya nitumie mafuta zaidi pia charges nahisi ziko juu maana kila transaction inaweZa kuwa inakatwa
 
Sijui procedures za kupata hizo fuel cards , lakini nafahamu kuwa haziingiliani, ie ya puma utatumika puma na ya total itatumika total
[emoji848][emoji848][emoji107][emoji107][emoji107]
 
Kwa ninavyojua point of sales (pos ) hakuna makato, no direct transaction , hata kama utafanya multi transaction as long as no pos hakuna makato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…