Petroli Bei Juu Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), iimetangaza bei kikomo za bidhaa za Mafuta zilizoanza kutumika leo Oktoba 4, 2023 ambapo kwa Dar es Salaam Petroli ni Tsh. 3,281, Dizeli 3,448 na Mafuta ya Taa Tsh. 2,943 ikiwa na ongezeko la Tsh. 68 kwa kila Lita.

Tanga, Petroli ni Tsh. 3,327, Dizeli 3,494, Mafuta ya Taa Tsh. 2,989 na Mtwara, Petroli itauzwa Tsh. 3,353, Dizeli Tsh. 3,520 na Mafuta ya Taa Tsh. 3,016 ambapo EWURA imesema ongezeko hilo linatokana na kupanda kwa 4.21% ya Gharama za Mafuta katika Soko la Dunia.

Aidha, EWURA imesema gharama za uagizaji Mafuta zimepanda hadi kufikia 17% kwa Petroli, 62% kwa Dizeli na 4% kwa Mafuta ya Taa. Pia, Bei za Mafuta zimeathiriwa na uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa Mafuta duniani (OPEC+) waliopunguza uzalishaji pamoja na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi ya
Urusi.

========
 
ewura ni matapeli
 
Hivi Bei ya mafuta ya Taa kuwa chini kuliko bei ya Pertol na Dizeli hakuwezi kusababisha uchakachuaji?🤔
 
Hapo ruzuku ya 100 bilioni inatolewa kila mwezi. Tunaipongeza Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama
Wapunguze zile kodi ipo 26% kwenye mafuta hiyo ruzuku hata wasipotoa wakatoa baadhi ya kodi kichefuchefu za mafuta life itaenda sawa...
 
Kiongozi wa nchi ni mwanamke tusitegemee Jambo jema kutoka kwake
 
Tutafute wawekezaji vya vyeo vya juu kitaifa. Wenye maono. Na definition sahihi ya Kiongozi
 
na bado mtatema bungo,na mamayao yuko kwa wawekezaji kule anaangalia maonesho ya mboga mboga sijui takataka gani, yaani Mungu atuhurumie wadanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…