PFP PSYCHOLOGY PART 2: Unataka kujua picha ya profile yako inasema Nini kuhusu wewe?! Usiache kusoma hapa.

The ghost writer

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2023
Posts
967
Reaction score
1,971
1. The couple PFP
1401588.jpg

Ni profile picture ya wapenzi wawili wakikumbatiana, wakishikana mikono (soul tie). Hawa ndio wale Wanajionaga "Wamiliki wa Hati Miliki za Mapenzi"! 😅

Tafsiri ya Picha Jinsi inavyoonekana;
Nina mtu wangu. Tayari Nimechukuliwa. Respect the badge. 😅

Maisha Yao mtandaoni.
Mara nyingi anataka kuwaonyesha watu mtandaoni Kuwa yupo kwenye seriously relationship. Wanapenda komment au kupost Maneno kama " Ninajivunia Partner wangu" au " Msije mkapoteza muda kunitongosha". Ingawa hakuna aliyemuuliza kumhusu huyo mpenzi wake anayemjivunia Wala kumtongoza yeye😅

Wakati mwingine akaunti inaweza kuwa ya pamoja , itaitwa "JohnAndGrace" kwa Siri. Siku Ukimtumia ujumbe John, jua Grace ndio anasoma na kukujibu huku amekunja sura.😅

Kazi yao ni ku-comment chini ya picha za kila mmoja: "Mume wangu mzuri," "Mke wangu kipenzi," hata kama wamekaa kiti kimoja sebuleni wakitazamana live.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Hawa ndio wale Wazee wa "Nani Amekutumia Ujumbe?" (Wivu) na Mara nyingi, picha hii haitoki moyoni mwa wote wawili. Ni matokeo ya ugomvi mkubwa wa wivu uliopita! Mmoja alifanya kosa, adhabu yake ikawa ni kuwekwa kwenye Profile Picture ili "kufuta madambi." 😂

Mtandaoni picha ina tabasamu la bilioni moja, lakini live huko nyumbani wanaweza kuwa hawasemeshani tangu asubuhi kisa mmoja amesahau Kuzima taa ya bafuni😅

Marafiki zao wote mtandaoni wanakuwa wanaiangalia ile picha kwa jicho la dongo, wakisubiri kwa hamu siku itakayobadilishwa na kuwekwa picha ya ua au "Black Screen" ili wajue kuwa kimenuka! 😂

2.The footballer PFP.
IMG_20260717_130857.jpg

Hao sasa ndio "Wachezaji wa Akiba wa Mtandaoni"! 😅

Ni watu wanaoweka picha za wachezaji wa mpira iwe ni Cristiano Ronaldo akishangilia "Siuuu", Messi ameinua mikono juu, Neymar akilia, au picha ya mchezaji mdogo wa sasa kama Lamine Yamal n.k

Uhalisia was maisha Yao Mtandaoni;
Wanajiona kama wajumbe rasmi wa FIFA.

Ni makocha wa Mtandaoni Kazi yao kubwa ni kupanga vikosi vya timu zao Utasikia: "Kocha hana akili, kwanini amemweka fulani benchi?" Wanaongea kwa kujiamini kana kwamba wana leseni ya ukocha ya FIFA

Utawakuta kwenye magroup ya WhatsApp ya soka, wao ndio wanaoongoza kutuma ujumbe wa sauti (voice notes) wa dakika tano wakichambua mechi iliyoisha, huku wakipiga kelele kwa hasira.

Kwenye maisha Halisi:
Licha ya mahaba yote ya soka, ujuzi wao mkubwa wa mpira unaishia kwenye kuangalia mechi kwenye vibanda vya kuonyeshea mpira (vibanda umiza) au kwenye magemu ya EA Sports FC ,(FIFA) kwenye PlayStation

Huwa wana jezi moja ya timu wanayoipenda ambayo wameivaa tangu miaka mitatu iliyopita. Imeshafuba, maandishi ya mdhamini kifuani yamebanduka, lakini ndio nguo yao ya mtoko kila Jumamosi na Jumapili kisa "inaleta bahati" kwa timu.

3. The Religious PFP.
Screenshot_20260717_115343.jpg

Hao sasa ndio wanajionaga "Walinzi wa Lango la Mbinguni" 😅
Ni wat wanaoweka picha za kidini iwe ni picha ya Yesu, Bikira Maria, maneno ya aya za Qur'ani au Biblia, au picha ya mchungaji/shehe wao maarufu.

Wanataka kila mtu ajue kuwa wao wameshaandika majina yao kwenye kitabu cha uzima.

Huu hapa UHALISIA wao usio na usiri Mtandaoni;
Kazi yao kubwa ni kusambaza picha zenye maneno "Sema Amina ubarikiwe" au "Share picha hii kwa watu 10 upate muujiza leo. 😅

Ukipost picha ukiwa klabu au umevaa nguo fupi, watakuja kwenye comment kukwambia "Tubu, dunia inaisha kesho" au kukupigia mistari mirefu ya vitabu vitakatifu ili ujisikie una dhambi kuliko shetani. 😅

Status zao za WhatsApp zote zimejaa nyimbo za kwaya, kaswida, au mahubiri ya masaa mawili. Ukifungua unahisi kama umeingia kanisani au msikitini kabisa.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Mabingwa wa Udaku: Mtandaoni ni watakatifu, lakini live ndio wale wanaoongoza kujua udaku wote wa mtaani! Ukikaa nao sebuleni, watakwambia habari za kila jirani.

Ni watu wenye hasira za ghafla. Licha ya quotes zote za amani na kusamehe, live ndio watu wanaoweza kugombana na mtu sokoni kisa tu ameibiwa shilingi mia mbili ya chenji, au kufokea watoto nyumbani hadi sauti inakauka.

Kiuhalisia, wengi wao huwa wanaweka hizo picha kama ngao ya kujikinga na majaribu ya dunia au kuficha "madambi" yao ya sirini ili watu wawaone ni watu wema na waaminifu.

4.The Old photo PFP.
12431.jpg
Screenshot_20260717_121333.jpg

Hao Sasa ndio wazee wa kumbukumbu 😅

Ni wale wanaoweka picha za zamani sana zilizofuba iwe ni picha zao wenyewe wakiwa watoto au Picha zao enzi za ujana wao (miaka ya 90 au 2010s)

Huu hapa uhalisia wao Mtandaoni;
Wapinzani wa Kizazi Kipya. Kazi yao kubwa ni kulalamikia maisha ya sasa. Utasikia "watoto wa siku hizi wanajua tu TikTok." Kila post yao inaishia na "Maisha ya sasa yamepoteza mwelekeo.

Wachambuzi wa Muziki wa Kale: Ndio wale wanaoingia YouTube kutafuta video za nyimbo zamani na kucomment Utasikia "Huu ndio ulikuwa muziki halisi, sio kelele za sasa!" 😂

Ni watu wapenda Amani na Utulivu. Hawashiriki kabisa kwenye drama za mtandaoni, udaku, au mabishano ya nani kavaa au kanyoa vizuri. Wapo tu kwa ajili ya kuangalia mambo yanavyoenda.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check).
Kama ni kijana ameweka picha yake ya utotoni, jua live ana roho ya kizee kabisa! Mapema saa tatu usiku ashalala, anachukia kelele za klabu, na kinywaji chake kikubwa ni chai ya rangi yenye tangawizi nyingi.

Kundi la pili wanaweka picha za miaka 10 iliyopita kwa sababu wanaogopa kuonesha jinsi maisha, mabadiliko ya miili (kitambi au unene), au mvi zilivyowakabili kwa sasa. Wanataka ulimwengu uwakumbuke kwa ule muonekano wao wa "dhahabu.

Ni mastaa wa Hadithi za "Enzi Zetu": Ukikutana nao live, jiandae kusikiliza hadithi zisizoisha. Utasikia "mimi enzi zangu nasoma sekondari nilikuwa nawakimbiza sana mademu," hata kama kiuhalisia alikuwa watu waoga wanaokaa benchi la nyuma kabisa darasani.

5. The Hoodies face PFP.
4b39e2480e5bfa1e6392d3a0d60dc217.jpg

Hawa watu sijui ndio wanajionaga "Wajumbe wa FBI" au ?😅

Ni wale wanaoweka picha ya mwanaume aliyevaa koti la 'hoodie' lililofunika kichwa, sura haionekani (faceless) au kuna kivuli kikubwa mbele utadhani wadukuzi (hackers) wa mitandaoni au watu wenye maisha ya hatari sana.

Uhalisia wa maisha Yao mtandaoni.
Wanajifanya (The Mystery Man). Wenye Maneno ya mafumbo. Hawana stori za kawaida. Kila wakipost, wanaandika maneno mafupi ya siri au mafumbo kama: "Trust no one," au "Usinifuate."

Hawataki kabisa mtu ajue sura zao, umri wao, au wanakoishi. Ukijaribu kuwauliza maswali ya kawaida DM, wanakujibu kwa ukavu utadhani wanahojiwa na polisi.

Wanapenda kushea memes za watu wapweke (lonely text) au zile za "Sigma Male" wakijifanya wao hawahitaji marafiki duniani.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Mtandaoni picha inaonekana ya kijasusi na hatari, lakini live ndio wale watu wapole kupitiliza ambao wakikaa kwenye kikundi cha watu hawaongei neno, na mtu akiwatazama machoni wanainamisha kichwa haraka kwa aibu.

Sababu kubwa ya kuficha sura kwenye hoodie sio kwamba wao ni majasusi, bali labda wanaona sura zao hazina "vibe" la kitajiri, kwahiyo hoodie inakuwa kama kichujio (filter) cha bei rahisi.

Licha ya muonekano wao wa mtandaoni, live ni watoto wazuri kabisa wa mama zao, wanaotumwa kununua vitunguu gengeni na wanafua nguo zao wenyewe kila Jumamosi asubuhi huku wakisikiliza nyimbo za taarab au Bongo Flava.

6.The black PFP.
dark-abstract-background_1048-1920.jpg

Watu wanaoweka picha ya weusi tupu (Black Screen/Solid Black PFP) huwa wanatuma ujumbe mzito sana usio na sauti.

UHALISIA wa maisha Yao Mtandaoni;
Wanapenda kuweka status au kupost stories za huzuni. Utakuta nyimbo za huzuni za Adele au Billie Eilish, au maandishi madogo ya kiingereza yanayosema: "I'm fine." Japo moyoni anaungua 😅

Wanataka kuonesha ulimwengu kuwa wamechoka na mitandao na wanapitia kipindi kigumu, lakini cha kuchekesha ni kwamba bado wapo mtandaoni masaa 24 wakichungulia nani kapost au nani kaangalia status zao au stories zao.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check);
Ni watu wanaopenda kufanya Maamuzi ya Hasira (Impulsive): Mara nyingi picha hii inawekwa baada ya ugomvi wa dakika mbili na mpenzi wao, au baada ya kufanya vibaya kwenye usaili wa kazi, au baada ya kufeli mitihani, Ni hasira za ghafla zinawapelekea kufanya hivo. Kiufupi wako very less emotional control😓

Ni watu wanaongoza kuwa na depression. Mawazo ya kujiua Yana tawala vichwani mwao. Ni watu wanohitaji msaada sana wa kisaikolojia kabla hawajachukua maamuzi ya kucomit suicide. Ukiona mtu ameweka hii, jua kuna jambo.

7. The Cartoon PFP.
Screenshot_20260717_130738.jpg

Hao ndio "Wakaazi wa Dunia ya Kufikirika"! 😅

Ni watu wanaoweka picha za katuni (Cartoon/Anime PFP) iwe ni Naruto, SpongeBob, Tom&jerry, au zile katuni za kuchorwa za 3D.

Uhalisia wa maisha Yao mtandaoni;
Mara nyingi wanajua mambo mengi ya ndani ya mtandao, michezo ya video (gaming), VPN, jinsi ya kudownload vitu vya bure, au mambo ya AI.

Wanapenda uhuru wa hali ya juu.

Ukiingia kwenye profile zao, hakuna jina halisi, hakuna mahali wanapoishi.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check:
Hawa ni watu wanaoweza kushinda ndani mchana mzima wakicheza game au kuangalia movie.

Sababu kubwa ya kuweka katuni si kwamba wanazipenda sana, bali wanajiona "hawapigi picha vizuri" au hawajiamini na sura zao (low self-esteem) kwa kipindi hicho. Katuni inakuwa kama ngao yao ya usalama.

Mtandaoni wanaweza kuwa ni watu wenye kelele na fujo sana lakini live ni watu wapole na wenye aibu.

8.The feminist PFP.
71GXIylZ9wS._AC_UF894,1000_QL80_.jpg

Hao sasa ndio wanajionaga "Majenerali wa Vita vya Jinsia" au "Walinzi wa Haki za Akina Dada"!

Watu wanaoweka picha zenye mrengo wa ufeministi mara nyingi Huwa ni picha ya mwanamke anaenokana karusha ngumi, amekunja misuli (We Can Do It!), au picha zao wenyewe wakiwa wamekunja sura, huwa hawaji mtandaoni kuchekesha.

Hali ya maisha Yao Mtandaoni;
Kazi yao kubwa ni kupinga mfumo dume. Ndio wanaongoza kuwatukana wanaume yeyote anaye andika post ya mzaha kuhusu wanawake, Utasikia " Sibabaishwi na mwanaume". "Unikome". Au "wanaume wote ni mbwa" na matusi mengine ya nguoni na ya sirini.

Hawana uvumilivu kabisa. Ukileta ubishi wa kizamani kwenye comment zao, au walishindwa kujadili hoja hawajadiliani na wewe Tena unapigwa 'Block' ya maisha.

Post zao zote zinasema "Sisi kama wanawake tunajitosheleza," na kazi yao ni kupongezana wao kwa wao kwenye comment kwa kuandika "shoga yangu Mimi huyo!" au "Penda sana Mamy ake" au "shosti umetisha"

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check)

Wakati mtandaoni wanapigana vita vya ukombozi wa mwanamke duniani, live wanaweza kuwa wamekaa sebuleni kwao huku mama yao akiwafokea: "Nanihii! Tangu asubuhi umeshika hiyo simu tu, hebu nenda kasafishe vyombo au nenda kasafishe bafuni!"

Licha ya kelele zote za "Hatuhitaji wanaume maishani," gizani usiku ndio wale wanaoweza kuwa wanaangalia tamthilia za mapenzi (Romantic Comedies) huku wakilia na kutamani kupata mwanaume mtanashati wa kuja kuwabeba juu juu na kuwadekeza.
 
YOU ARE WHAT YOU THINK

Mithali 23:7
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.

luka 6 45
kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake

username /avator ya mtu-ina akisi kwa kiasi fulani yale yauzayo moyo wake
katika nchi ya palestina mtoto mdogo wa miaka 7 alipewa kalamu na karatasi akaambiwa aandike au achore chochote.

akachora bunduki...
SO PYSCHOLOGICALY...alikuwa anareflect kilichoujaza moyo wake..

mtu Akiweka status ya Footballer simply kwa namna moja ana mpira una nafasi una effect katika maisha yake kwa namna moja.

mtu akiweka status ya YESU ina maana Yesu amegusa maisha yake kwa namna moja ,Yesu ana nafasi katika maisha yake.
 
😅 Ni Kweli mkuu🙏
 
1. The couple PFP
View attachment 3630915
Ni profile picture ya wapenzi wawili wakikumbatiana, wakishikana mikono (soul tie). Hawa ndio wale Wanajionaga "Wamiliki wa Hati Miliki za Mapenzi"! 😅

Tafsiri ya Picha Jinsi inavyoonekana;
Nina mtu wangu. Tayari Nimechukuliwa. Respect the badge. 😅

Maisha Yao mtandaoni.
Mara nyingi anataka kuwaonyesha watu mtandaoni Kuwa yupo kwenye seriously relationship. Wanapenda komment au kupost Maneno kama " Ninajivunia Partner wangu" au " Msije mkapoteza muda kunitongosha". Ingawa hakuna aliyemuuliza kumhusu huyo mpenzi wake anayemjivunia Wala kumtongoza yeye😅

Wakati mwingine akaunti inaweza kuwa ya pamoja , itaitwa "JohnAndGrace" kwa Siri. Siku Ukimtumia ujumbe John, jua Grace ndio anasoma na kukujibu huku amekunja sura.😅

Kazi yao ni ku-comment chini ya picha za kila mmoja: "Mume wangu mzuri," "Mke wangu kipenzi," hata kama wamekaa kiti kimoja sebuleni wakitazamana live.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Hawa ndio wale Wazee wa "Nani Amekutumia Ujumbe?" (Wivu) na Mara nyingi, picha hii haitoki moyoni mwa wote wawili. Ni matokeo ya ugomvi mkubwa wa wivu uliopita! Mmoja alifanya kosa, adhabu yake ikawa ni kuwekwa kwenye Profile Picture ili "kufuta madambi." 😂

Mtandaoni picha ina tabasamu la bilioni moja, lakini live huko nyumbani wanaweza kuwa hawasemeshani tangu asubuhi kisa mmoja amesahau Kuzima taa ya bafuni😅

Marafiki zao wote mtandaoni wanakuwa wanaiangalia ile picha kwa jicho la dongo, wakisubiri kwa hamu siku itakayobadilishwa na kuwekwa picha ya ua au "Black Screen" ili wajue kuwa kimenuka! 😂

2.The footballer PFP.
View attachment 3630914
Hao sasa ndio "Wachezaji wa Akiba wa Mtandaoni"! 😅

Ni watu wanaoweka picha za wachezaji wa mpira iwe ni Cristiano Ronaldo akishangilia "Siuuu", Messi ameinua mikono juu, Neymar akilia, au picha ya mchezaji mdogo wa sasa kama Lamine Yamal n.k

Uhalisia was maisha Yao Mtandaoni;
Wanajiona kama wajumbe rasmi wa FIFA.

Ni makocha wa Mtandaoni Kazi yao kubwa ni kupanga vikosi vya timu zao Utasikia: "Kocha hana akili, kwanini amemweka fulani benchi?" Wanaongea kwa kujiamini kana kwamba wana leseni ya ukocha ya FIFA

Utawakuta kwenye magroup ya WhatsApp ya soka, wao ndio wanaoongoza kutuma ujumbe wa sauti (voice notes) wa dakika tano wakichambua mechi iliyoisha, huku wakipiga kelele kwa hasira.

Kwenye maisha Halisi:
Licha ya mahaba yote ya soka, ujuzi wao mkubwa wa mpira unaishia kwenye kuangalia mechi kwenye vibanda vya kuonyeshea mpira (vibanda umiza) au kwenye magemu ya EA Sports FC ,(FIFA) kwenye PlayStation

Huwa wana jezi moja ya timu wanayoipenda ambayo wameivaa tangu miaka mitatu iliyopita. Imeshafuba, maandishi ya mdhamini kifuani yamebanduka, lakini ndio nguo yao ya mtoko kila Jumamosi na Jumapili kisa "inaleta bahati" kwa timu.

3. The Religious PFP.
View attachment 3630913

Hao sasa ndio wanajionaga "Walinzi wa Lango la Mbinguni" 😅
Ni wat wanaoweka picha za kidini iwe ni picha ya Yesu, Bikira Maria, maneno ya aya za Qur'ani au Biblia, au picha ya mchungaji/shehe wao maarufu.

Wanataka kila mtu ajue kuwa wao wameshaandika majina yao kwenye kitabu cha uzima.

Huu hapa UHALISIA wao usio na usiri Mtandaoni;
Kazi yao kubwa ni kusambaza picha zenye maneno "Sema Amina ubarikiwe" au "Share picha hii kwa watu 10 upate muujiza leo. 😅

Ukipost picha ukiwa klabu au umevaa nguo fupi, watakuja kwenye comment kukwambia "Tubu, dunia inaisha kesho" au kukupigia mistari mirefu ya vitabu vitakatifu ili ujisikie una dhambi kuliko shetani. 😅

Status zao za WhatsApp zote zimejaa nyimbo za kwaya, kaswida, au mahubiri ya masaa mawili. Ukifungua unahisi kama umeingia kanisani au msikitini kabisa.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Mabingwa wa Udaku: Mtandaoni ni watakatifu, lakini live ndio wale wanaoongoza kujua udaku wote wa mtaani! Ukikaa nao sebuleni, watakwambia habari za kila jirani.

Ni watu wenye hasira za ghafla. Licha ya quotes zote za amani na kusamehe, live ndio watu wanaoweza kugombana na mtu sokoni kisa tu ameibiwa shilingi mia mbili ya chenji, au kufokea watoto nyumbani hadi sauti inakauka.

Kiuhalisia, wengi wao huwa wanaweka hizo picha kama ngao ya kujikinga na majaribu ya dunia au kuficha "madambi" yao ya sirini ili watu wawaone ni watu wema na waaminifu.

4.The Old photo PFP.
View attachment 3630910View attachment 3630912
Hao Sasa ndio wazee wa kumbukumbu 😅

Ni wale wanaoweka picha za zamani sana zilizofuba iwe ni picha zao wenyewe wakiwa watoto au Picha zao enzi za ujana wao (miaka ya 90 au 2010s)

Huu hapa uhalisia wao Mtandaoni;
Wapinzani wa Kizazi Kipya. Kazi yao kubwa ni kulalamikia maisha ya sasa. Utasikia "watoto wa siku hizi wanajua tu TikTok." Kila post yao inaishia na "Maisha ya sasa yamepoteza mwelekeo.

Wachambuzi wa Muziki wa Kale: Ndio wale wanaoingia YouTube kutafuta video za nyimbo zamani na kucomment Utasikia "Huu ndio ulikuwa muziki halisi, sio kelele za sasa!" 😂

Ni watu wapenda Amani na Utulivu. Hawashiriki kabisa kwenye drama za mtandaoni, udaku, au mabishano ya nani kavaa au kanyoa vizuri. Wapo tu kwa ajili ya kuangalia mambo yanavyoenda.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check).
Kama ni kijana ameweka picha yake ya utotoni, jua live ana roho ya kizee kabisa! Mapema saa tatu usiku ashalala, anachukia kelele za klabu, na kinywaji chake kikubwa ni chai ya rangi yenye tangawizi nyingi.

Kundi la pili wanaweka picha za miaka 10 iliyopita kwa sababu wanaogopa kuonesha jinsi maisha, mabadiliko ya miili (kitambi au unene), au mvi zilivyowakabili kwa sasa. Wanataka ulimwengu uwakumbuke kwa ule muonekano wao wa "dhahabu.

Ni mastaa wa Hadithi za "Enzi Zetu": Ukikutana nao live, jiandae kusikiliza hadithi zisizoisha. Utasikia "mimi enzi zangu nasoma sekondari nilikuwa nawakimbiza sana mademu," hata kama kiuhalisia alikuwa watu waoga wanaokaa benchi la nyuma kabisa darasani.

5. The Hoodies face PFP.
View attachment 3630909

Hawa watu sijui ndio wanajionaga "Wajumbe wa FBI" au ?😅

Ni wale wanaoweka picha ya mwanaume aliyevaa koti la 'hoodie' lililofunika kichwa, sura haionekani (faceless) au kuna kivuli kikubwa mbele utadhani wadukuzi (hackers) wa mitandaoni au watu wenye maisha ya hatari sana.

Uhalisia wa maisha Yao mtandaoni.
Wanajifanya (The Mystery Man). Wenye Maneno ya mafumbo. Hawana stori za kawaida. Kila wakipost, wanaandika maneno mafupi ya siri au mafumbo kama: "Trust no one," au "Usinifuate."

Hawataki kabisa mtu ajue sura zao, umri wao, au wanakoishi. Ukijaribu kuwauliza maswali ya kawaida DM, wanakujibu kwa ukavu utadhani wanahojiwa na polisi.

Wanapenda kushea memes za watu wapweke (lonely text) au zile za "Sigma Male" wakijifanya wao hawahitaji marafiki duniani.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check):
Mtandaoni picha inaonekana ya kijasusi na hatari, lakini live ndio wale watu wapole kupitiliza ambao wakikaa kwenye kikundi cha watu hawaongei neno, na mtu akiwatazama machoni wanainamisha kichwa haraka kwa aibu.

Sababu kubwa ya kuficha sura kwenye hoodie sio kwamba wao ni majasusi, bali labda wanaona sura zao hazina "vibe" la kitajiri, kwahiyo hoodie inakuwa kama kichujio (filter) cha bei rahisi.

Licha ya muonekano wao wa mtandaoni, live ni watoto wazuri kabisa wa mama zao, wanaotumwa kununua vitunguu gengeni na wanafua nguo zao wenyewe kila Jumamosi asubuhi huku wakisikiliza nyimbo za taarab au Bongo Flava.

6.The black PFP.
View attachment 3630908

Watu wanaoweka picha ya weusi tupu (Black Screen/Solid Black PFP) huwa wanatuma ujumbe mzito sana usio na sauti.

UHALISIA wa maisha Yao Mtandaoni;
Wanapenda kuweka status au kupost stories za huzuni. Utakuta nyimbo za huzuni za Adele au Billie Eilish, au maandishi madogo ya kiingereza yanayosema: "I'm fine." Japo moyoni anaungua 😅

Wanataka kuonesha ulimwengu kuwa wamechoka na mitandao na wanapitia kipindi kigumu, lakini cha kuchekesha ni kwamba bado wapo mtandaoni masaa 24 wakichungulia nani kapost au nani kaangalia status zao au stories zao.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check);
Ni watu wanaopenda kufanya Maamuzi ya Hasira (Impulsive): Mara nyingi picha hii inawekwa baada ya ugomvi wa dakika mbili na mpenzi wao, au baada ya kufanya vibaya kwenye usaili wa kazi, au baada ya kufeli mitihani, Ni hasira za ghafla zinawapelekea kufanya hivo. Kiufupi wako very less emotional control😓

Ni watu wanaongoza kuwa na depression. Mawazo ya kujiua Yana tawala vichwani mwao. Ni watu wanohitaji msaada sana wa kisaikolojia kabla hawajachukua maamuzi ya kucomit suicide. Ukiona mtu ameweka hii, jua kuna jambo.

7. The Cartoon PFP.
View attachment 3630907

Hao ndio "Wakaazi wa Dunia ya Kufikirika"! 😅

Ni watu wanaoweka picha za katuni (Cartoon/Anime PFP) iwe ni Naruto, SpongeBob, Tom&jerry, au zile katuni za kuchorwa za 3D.

Uhalisia wa maisha Yao mtandaoni;
Mara nyingi wanajua mambo mengi ya ndani ya mtandao, michezo ya video (gaming), VPN, jinsi ya kudownload vitu vya bure, au mambo ya AI.

Wanapenda uhuru wa hali ya juu.

Ukiingia kwenye profile zao, hakuna jina halisi, hakuna mahali wanapoishi.

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check:
Hawa ni watu wanaoweza kushinda ndani mchana mzima wakicheza game au kuangalia movie.

Sababu kubwa ya kuweka katuni si kwamba wanazipenda sana, bali wanajiona "hawapigi picha vizuri" au hawajiamini na sura zao (low self-esteem) kwa kipindi hicho. Katuni inakuwa kama ngao yao ya usalama.

Mtandaoni wanaweza kuwa ni watu wenye kelele na fujo sana lakini live ni watu wapole na wenye aibu.

8.The feminist PFP.
View attachment 3630906

Hao sasa ndio wanajionaga "Majenerali wa Vita vya Jinsia" au "Walinzi wa Haki za Akina Dada"!

Watu wanaoweka picha zenye mrengo wa ufeministi mara nyingi Huwa ni picha ya mwanamke anaenokana karusha ngumi, amekunja misuli (We Can Do It!), au picha zao wenyewe wakiwa wamekunja sura, huwa hawaji mtandaoni kuchekesha.

Hali ya maisha Yao Mtandaoni;
Kazi yao kubwa ni kupinga mfumo dume. Ndio wanaongoza kuwatukana wanaume yeyote anaye andika post ya mzaha kuhusu wanawake, Utasikia " Sibabaishwi na mwanaume". "Unikome". Au "wanaume wote ni mbwa" na matusi mengine ya nguoni na ya sirini.

Hawana uvumilivu kabisa. Ukileta ubishi wa kizamani kwenye comment zao, au walishindwa kujadili hoja hawajadiliani na wewe Tena unapigwa 'Block' ya maisha.

Post zao zote zinasema "Sisi kama wanawake tunajitosheleza," na kazi yao ni kupongezana wao kwa wao kwenye comment kwa kuandika "shoga yangu Mimi huyo!" au "Penda sana Mamy ake" au "shosti umetisha"

Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check)

Wakati mtandaoni wanapigana vita vya ukombozi wa mwanamke duniani, live wanaweza kuwa wamekaa sebuleni kwao huku mama yao akiwafokea: "Nanihii! Tangu asubuhi umeshika hiyo simu tu, hebu nenda kasafishe vyombo au nenda kasafishe bafuni!"

Licha ya kelele zote za "Hatuhitaji wanaume maishani," gizani usiku ndio wale wanaoweza kuwa wanaangalia tamthilia za mapenzi (Romantic Comedies) huku wakilia na kutamani kupata mwanaume mtanashati wa kuja kuwabeba juu juu na kuwadekeza.
Na wewe ni mdukuzi tu kujifanya unajua ya watu...
 
Back
Top Bottom