PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

Aisee wanasiasa mnakatisha watu tamaa ya kusoma bhana, watu wanahangaika kusoma kwa taabu wanakesha usiku, Kuna wengine Familia zinauza Mali za ukoo ili kijana asome, wengine wa nashindwa kumaliza kwa kukosa Ada na wengine wanashindwa kwa kufeli mitihani(discontinuation).
Masikini ya Mungu na wengine watoto wa kike mpaka wanauza utu wao kwa waalimu wao kwa kutoa rushwa ya ngono, halafu huku nyie yaani mnapeanapeana tu, eti mara Degree ya heshima, mara PhD ya heshima, acheni mzaha na elimu jamani, Elimu ni IBADA.

Eti PHD, hivi wewe Kasheku unajua PHD au unaisikia tu!!!

Udaktari wa Heshima katika Siasa na uongozi, kwa hiyo Sasa hivi tumuite Dr. MSUKUMA[emoji23][emoji23][emoji23]? AFADHARI ya Dr. MAJI MAREFU Udaktari wake aliojitangaza nao ulikuwa unajulikana anafanya nini!

Wapi umewahi kusikia standard Seven anapata PHD? [emoji23]

Na mbona hizo shahada za heshima kila siku wanapewa wanasiasa tu???
 
Hicho chuo nakifahamu nichakihuni kabisa nakumbuka kilianza pale mpanda na huyo jamaa sijui ndio mkuu ni askofu wakanisa linaitwa penuel,lipo mpanda pale karibu na kwa pinda kutokana na usanii flan flan jamaa kahamishia huduma tabora kwa hiyo ametengeneza connection flani ya kijanja janja hivi na kufungua hicho chuo tuanzie hapa serikali ufanye uchunguzi na hiko chuo,,,Mara moja Kuna watu wanatapeliwa
 

 
Msukuma hata cheti cha la saba hana. Bungeni hana mchango wowote. Kwenye jamii hana mchango wowote zaidi ya kuvimba tu.


Sasa unampaje huyu mtu honorary doctorate? Huo ni ufala.

Tumekuwa tuniaminisha jamii kuwa ukiwa na shahada na hasa Ph.D ndio utathaminika na kama ni mbunge unakuwa na nafasi kubwa kupata uwaziri!!! Ndio maana hivi sasa kuna mlolongo wa wabunge wanafukuzia hizo Ph.D kwa udi na jvumba. Walianza wakina Nchimbi na sasa hata wakina Lukuvi karibuni nao watatunukiwa hizo shahada!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…