PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

Musukuma sasa hivi ni msomi, hatahangaika tena kutukana wasomi. "Chuo" kilichompa digrii hiyo kiko India na huwa kinachaji dola 500 kutoa digrii yoyote ya heshima, ofizi za chuo ni chumba kimoja tu, ila kina washkaji 15 kutoka sehemu mbalimbali za India, Sri Lanka na Indonesia; wote ni wahindi.
 
Mkazania kusema hicho chuo hakitambuliki,SI MKITAJE?
Hicho hakina hata hadhi ya kuitwa chuo
20211206_044643.jpg
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA[emoji116][emoji116][emoji116]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa nimejua. Siku za karibuni Kuna mtu aliniita kutokea Arusha akaniambia jina langu limependekezwa ili nipewe udaktari wa heshima kwa sababu (akataja nyingi). Kisha akasema zinatakiwa dola 500 haraka sana na deadline ni siku ya pili yake. Akataja chuo hikihiki.

Nikamwambia hiyo hela Sina. Akasema basi leta dola 210 kwa punguzo maalum.

Nikamwambia kwa Sasa Kuna vyuo vikuu 3 humu duniani vinaniomba nipokee udaktari wa heshima kutoka kwao lakini itaambatana na cheki ya dola elfu kumi kwangu. Nikamwambia bado nasita kwa sababu walizonitajia kuwa ninazo bado nina mashaka nazo kama ninazo kweli. Tukaachana hivo.

Kumbe wakapatikana kina Msukuma?!
Kwani Bagonza ni Mungu ?
 
Tumekuwa tuniaminisha jamii kuwa ukiwa na shahada na hasa Ph.D ndio utathaminika na kama ni mbunge unakuwa na nafasi kubwa kupata uwaziri!!! Ndio maana hivi sasa kuna mlolongo wa wabunge wanafukuzia hizo Ph.D kwa udi na jvumba. Walianza wakina Nchimbi na sasa hata wakina Lukuvi karibuni nao watatunukiwa hizo shahada!!!
Walianza akina Kamala....
Screenshot_20211205-221556_Chrome.jpg
 
Aisee wanasiasa mnakatisha watu tamaa ya kusoma bhana, watu wanahangaika kusoma kwa taabu wanakesha usiku, Kuna wengine Familia zinauza Mali za ukoo ili kijana asome, wengine wa nashindwa kumaliza kwa kukosa Ada na wengine wanashindwa kwa kufeli mitihani(discontinuation).
Masikini ya Mungu na wengine watoto wa kike mpaka wanauza utu wao kwa waalimu wao kwa kutoa rushwa ya ngono, halafu huku nyie yaani mnapeanapeana tu, eti mara Degree ya heshima, mara PhD ya heshima, acheni mzaha na elimu jamani, Elimu ni IBADA.

Eti PHD, hivi wewe Kasheku unajua PHD au unaisikia tu!!!

Udaktari wa Heshima katika Siasa na uongozi, kwa hiyo Sasa hivi tumuite Dr. MSUKUMA[emoji23][emoji23][emoji23]? AFADHARI ya Dr. MAJI MAREFU Udaktari wake aliojitangaza nao ulikuwa unajulikana anafanya nini!

Wapi umewahi kusikia standard Seven anapata PHD? [emoji23]

Na mbona hizo shahada za heshima kila siku wanapewa wanasiasa tu???View attachment 2034376View attachment 2034377
Udaktari wa Heshima katika Siasa na uongozi, kwa hiyo Sasa hivi tumuite Dr. MSUKUMA[emoji23][emoji23][emoji23]? AFADHARI ya Dr. MAJI MAREFU Udaktari wake aliojitangaza nao ulikuwa unajulikana anafanya nini!
 
Kasheku Msukuma Naye Ametoboa Kwa Ujanjaujanja
Maisha Unaweza Kutumia Nguvu Sana Baadaye Huna Lolote
 
nani wa kupinga pale makao makuu ya hospitali ya vichaa ambayo nyerere ndio aliona bora kuweka pale
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA[emoji116][emoji116][emoji116]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa nimejua. Siku za karibuni Kuna mtu aliniita kutokea Arusha akaniambia jina langu limependekezwa ili nipewe udaktari wa heshima kwa sababu (akataja nyingi). Kisha akasema zinatakiwa dola 500 haraka sana na deadline ni siku ya pili yake. Akataja chuo hikihiki.

Nikamwambia hiyo hela Sina. Akasema basi leta dola 210 kwa punguzo maalum.

Nikamwambia kwa Sasa Kuna vyuo vikuu 3 humu duniani vinaniomba nipokee udaktari wa heshima kutoka kwao lakini itaambatana na cheki ya dola elfu kumi kwangu. Nikamwambia bado nasita kwa sababu walizonitajia kuwa ninazo bado nina mashaka nazo kama ninazo kweli. Tukaachana hivo.

Kumbe wakapatikana kina Msukuma?!
Inatakiwa ashitakiwe haraka
 
Back
Top Bottom