PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

Msukuma amewahinga maprofesa wa UDOM waliokuwa wanajaza madokezo toka Global USA. Hawa UDOM njaa Sana hawa.
 
Msukuma usomi anaupenda ila kukaa darasani ndio hataki.
Kwa nin asirudi shule tu akaanza form 1 hadi afikie ngazi ya elimu anayoitaka?
 
Wachunguzi wanadai kwamba eti Chuo hicho kiko India na kwamba kina matawi yake Uingereza na Marekani , bali uchunguzi unaonyesha kwamba hakijawahi kusajiliwa Uingereza wala Marekani na wala hakipo huko .

Kingine ambacho wachunguzi wamekifuatilia ni vigezo ambavyo Vimezingatiwa ili kumpa heshima hiyo Musukuma , yadaiwa ni mchongo mwanzo mwisho .

Baba Askofu Bagonza amenukuliwa kwamba aliombwa dola 500 na chuo hicho ili aingizwe kwenye mchakato wa watakaopewa PhD hiyo na hicho chuo cha Musukuma , ila yeye akagoma na akawaambia wahusika kwamba anazo ofa kadhaa kutoka kwenye vyuo vikubwa duniani vinavyomuomba akubali kupewa PhD za heshima , tena kwa vyuo vyenyewe kumlipa hadi US D Elfu 10 , siyo kwa yeye kuvilipa vyuo kama chuo cha Musukuma kinavyodai .

Swali ni hili , ni nani anafaidika na vyuo vya uongo kama hiki cha Musukuma na ili iweje ?
Ila unakosea kutumia neon PhD za heshima huyumika Dr.
 
Usitumie nguvu, soma historia Amani Karume ni daktari wa heshima lakini ni F6, kuna watu hawapendi sifa mwl alitunikiwa mara kibao lakini hakupenda hata Mkapa wote hawakuwahi kuitwa Dr, PhD huwa wanaandika mfano Dr Mapapai Mamba(PhD) lakini Msukuma ataishia kuandika Dr Msukuma pekee
Mkuu mizania yako ikoje lakini.
Kuwafananisha intellect ya Mwalimu na kina msukuma.
Sioni relevance ya argument.
 
Nilipokuwa sekondari Kuna mwandishi mmoja wa vitabu mwenye jina la kihaya nimemsahau alileta TAFRANI kwa baadhi ya VIONGOZI kwa kuwataja kuwa si madaktari wa kweli.......

Kuhusu hizi "HONORIS CAUSA" aliyopatiwa mh.Musukuma anaweza kupewa yeyote mwenye MCHANGO katika jamii ...hoja tu ni kutoka CHUO KIKUU GANI CHENYE ITHIBATI ZILIZOSIMAMA .....

Hata Nassib Abdul "alias" Diamond Platinumz naye ana SHAHADA ya heshima kutoka UDSM ........
Kainerugaba
 
Ni wehu tu wa kuamini porojo za huyo Bagonza.

Anapenda ku-trend kama mademu wa bongo movie.

Kwa nini hakuenda Police Post au PCCB ili hata akiongea hivi pawepo na reference ya kueleweka mahali.

Huo si ni utapeli alikuwa anataka kufanyiwa!
 
Kajishonea "GAUNI' avae pale wenzake wanapo vaaa
Tofautisha juho la Jana wakati anabatizwa udakitari na joho wakati wako kwenye vikao vya madiwani Nzera.

20211206_112449.jpg
 
PhD ya ujasiri wa kuongea kwa hoja bungeni bila woga. Ila anajua kujenga hoja.
 
PHD ya heshima huwezi kuitumia kama 'ante' rasmi ya jina.. neno DR. utalitumia tu kwenye mawasiliano na chuo kilichokupatia hiyo shahada ya heshima na siyo vyuo vingine. Katika CV inakuwa kwenye 'awards' siyo 'academic qualification'..
Hivyo ushawishi wa shahada ya heshima inaishia kwenye uzio wa nyumba yake..😛
Mbona Mh.kikwete anatumia hiyo Dr popote na hata Marehemu Dr Mengi naye ilikuwa inatumika pote
Ikitumika unavyosema wewe basi itakuwa haina maana sasa.!
 
#ShuleKidogo

Media nyingi zimekua zikifanya makosa kama waliofanya TBC leo, kuchanganya Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) na shahada ya Udaktari wa heshima (Honoris causa/doctorate).

Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) inasomewa darasani, inafanyiwa utafiti, na utafiti huo unatetewa kwenye jopo la maprofesa. Lakini Shahada ya udaktari wa heshima inatolewa bila kusomewa. Inatolewa kwa mtu yeyote aliyefanya jambo kubwa lililogusa jamii.

Bodi ya chuo inakaa na kuangalia mtu aliyefanya jambo kubwa kwa jamii wanamtunuku shahada ya udaktari wa heshima kama njia ya kutambua mchango wake. Chuo kikuu UDSM, idara ya sanaa (FPA) inaweza kumtunuku Diamond shahada ya udaktari wa heshima kama njia ya kutambua mchango wake ktk kukuza sanaa yetu kupitia muziki.

Udaktari wa Falsafa (PhD) na udaktari wa heshima (Honoris causa) ni vitu viwili tofauti kabisa. Havina uhusiano hata kidogo. Moja ni academia na nyingine ni just honorarium.

#Swali1: Je kuna shahada za udaktari wa aina ngapi?

#Jibu1: Zipo nyingi. Kwa uchache kuna shahada ya udaktari wa binadamu (MD), udaktari wa falsafa (PhD), udaktari wa Sheria (LLD), Udaktari wa sheria za kanisa (JCD), udaktari wa heshima (Honoris Causa) etc.

#Swali2: Je nawezaje kuzitofautisha?

#Jibu2: Inatakiwa kwenye mabano kuweka initials. Kwa mfano Dr.Benson Bagonza (PhD), Dr.Chris Cyrilo (MD), Dr.Wilbroad Slaa (JCD), Dr.Seng'ondo Mvungi (LLD) au Dr.Jakaya Kikwete (Honoris causa).

#Swali3: Je mtu mwenye udaktari wa heshima anaruhusiwa kuanza na Dr kwenye jina lake?

#Jibu3: Inaruhusiwa japo sio jambo la kuendekeza sana. Wengi wametunukiwa udaktari wa heshima na hawajiiti Doctors. Bill Clinton alitunukiwa mara 3 lakini hajawahi kujiita doctor. Mwal.Nyerere alitunukiwa mara 8 na vyuo mbalimbali vyenye hadhi lakini hakuwahi kujiita Dr.Nyerere.

Juzi mshambuliani wa Man U, Marcus Rashford ametunukiwa shahada ya udaktari wa heshima na Manchester University, moja ya vyuo vikubwa sana duniani, na hajiiti Dr.Rashford.

Lakini Afrika tunapenda sana utukufu. Mtu akitunukiwa udaktari wa heshima na Mchambawima University, kesho yake utasikia "naitwa Dr.Makoroboi Vuai Makaratasi" anaongeza na neno PhD mwishoni. Ulimbukeni tu.!

Malisa GJ
 
Wachunguzi wanadai kwamba eti Chuo hicho kiko India na kwamba kina matawi yake Uingereza na Marekani bali uchunguzi unaonyesha kwamba hakijawahi kusajiliwa Uingereza wala Marekani na wala hakipo huko .

Kingine ambacho wachunguzi wamekifuatilia ni vigezo ambavyo vimezingatiwa ili kumpa heshima hiyo Musukuma, yadaiwa ni mchongo mwanzo mwisho.

Baba Askofu Bagonza amenukuliwa kwamba aliombwa dola 500 na chuo hicho ili aingizwe kwenye mchakato wa watakaopewa PhD hiyo na hicho chuo cha Musukuma ila yeye akagoma na akawaambia wahusika kwamba anazo ofa kadhaa kutoka kwenye vyuo vikubwa duniani vinavyomuomba akubali kupewa PhD za heshima, tena kwa vyuo vyenyewe kumlipa hadi USD Elfu 10, siyo kwa yeye kuvilipa vyuo kama chuo cha Musukuma kinavyodai.

Swali ni hili, ni nani anafaidika na vyuo vya uongo kama hiki cha Musukuma na ili iweje?
Hahahaha[emoji23].. Ogopa Mungu na teknolojia
 
Back
Top Bottom