PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

Msukuma amewahinga maprofesa wa UDOM waliokuwa wanajaza madokezo toka Global USA. Hawa UDOM njaa Sana hawa.
 
Msukuma usomi anaupenda ila kukaa darasani ndio hataki.
Kwa nin asirudi shule tu akaanza form 1 hadi afikie ngazi ya elimu anayoitaka?
 
Ila unakosea kutumia neon PhD za heshima huyumika Dr.
 
Mkuu mizania yako ikoje lakini.
Kuwafananisha intellect ya Mwalimu na kina msukuma.
Sioni relevance ya argument.
 
Kainerugaba
 
Ni wehu tu wa kuamini porojo za huyo Bagonza.

Anapenda ku-trend kama mademu wa bongo movie.

Kwa nini hakuenda Police Post au PCCB ili hata akiongea hivi pawepo na reference ya kueleweka mahali.

Huo si ni utapeli alikuwa anataka kufanyiwa!
 
PhD ya ujasiri wa kuongea kwa hoja bungeni bila woga. Ila anajua kujenga hoja.
 
Mbona Mh.kikwete anatumia hiyo Dr popote na hata Marehemu Dr Mengi naye ilikuwa inatumika pote
Ikitumika unavyosema wewe basi itakuwa haina maana sasa.!
 
#ShuleKidogo

Media nyingi zimekua zikifanya makosa kama waliofanya TBC leo, kuchanganya Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) na shahada ya Udaktari wa heshima (Honoris causa/doctorate).

Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) inasomewa darasani, inafanyiwa utafiti, na utafiti huo unatetewa kwenye jopo la maprofesa. Lakini Shahada ya udaktari wa heshima inatolewa bila kusomewa. Inatolewa kwa mtu yeyote aliyefanya jambo kubwa lililogusa jamii.

Bodi ya chuo inakaa na kuangalia mtu aliyefanya jambo kubwa kwa jamii wanamtunuku shahada ya udaktari wa heshima kama njia ya kutambua mchango wake. Chuo kikuu UDSM, idara ya sanaa (FPA) inaweza kumtunuku Diamond shahada ya udaktari wa heshima kama njia ya kutambua mchango wake ktk kukuza sanaa yetu kupitia muziki.

Udaktari wa Falsafa (PhD) na udaktari wa heshima (Honoris causa) ni vitu viwili tofauti kabisa. Havina uhusiano hata kidogo. Moja ni academia na nyingine ni just honorarium.

#Swali1: Je kuna shahada za udaktari wa aina ngapi?

#Jibu1: Zipo nyingi. Kwa uchache kuna shahada ya udaktari wa binadamu (MD), udaktari wa falsafa (PhD), udaktari wa Sheria (LLD), Udaktari wa sheria za kanisa (JCD), udaktari wa heshima (Honoris Causa) etc.

#Swali2: Je nawezaje kuzitofautisha?

#Jibu2: Inatakiwa kwenye mabano kuweka initials. Kwa mfano Dr.Benson Bagonza (PhD), Dr.Chris Cyrilo (MD), Dr.Wilbroad Slaa (JCD), Dr.Seng'ondo Mvungi (LLD) au Dr.Jakaya Kikwete (Honoris causa).

#Swali3: Je mtu mwenye udaktari wa heshima anaruhusiwa kuanza na Dr kwenye jina lake?

#Jibu3: Inaruhusiwa japo sio jambo la kuendekeza sana. Wengi wametunukiwa udaktari wa heshima na hawajiiti Doctors. Bill Clinton alitunukiwa mara 3 lakini hajawahi kujiita doctor. Mwal.Nyerere alitunukiwa mara 8 na vyuo mbalimbali vyenye hadhi lakini hakuwahi kujiita Dr.Nyerere.

Juzi mshambuliani wa Man U, Marcus Rashford ametunukiwa shahada ya udaktari wa heshima na Manchester University, moja ya vyuo vikubwa sana duniani, na hajiiti Dr.Rashford.

Lakini Afrika tunapenda sana utukufu. Mtu akitunukiwa udaktari wa heshima na Mchambawima University, kesho yake utasikia "naitwa Dr.Makoroboi Vuai Makaratasi" anaongeza na neno PhD mwishoni. Ulimbukeni tu.!

Malisa GJ
 
Hahahaha[emoji23].. Ogopa Mungu na teknolojia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…