PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wachunguzi wanadai kwamba eti Chuo hicho kiko India na kwamba kina matawi yake Uingereza na Marekani bali uchunguzi unaonyesha kwamba hakijawahi kusajiliwa Uingereza wala Marekani na wala hakipo huko.

Kingine ambacho wachunguzi wamekifuatilia ni vigezo ambavyo vimezingatiwa ili kumpa heshima hiyo Musukuma, yadaiwa ni mchongo mwanzo mwisho.

Baba Askofu Bagonza amenukuliwa kwamba aliombwa dola 500 na chuo hicho ili aingizwe kwenye mchakato wa watakaopewa PhD hiyo na hicho chuo cha Musukuma ila yeye akagoma na akawaambia wahusika kwamba anazo ofa kadhaa kutoka kwenye vyuo vikubwa duniani vinavyomuomba akubali kupewa PhD za heshima, tena kwa vyuo vyenyewe kumlipa hadi USD Elfu 10, siyo kwa yeye kuvilipa vyuo kama chuo cha Musukuma kinavyodai.

Swali ni hili, ni nani anafaidika na vyuo vya uongo kama hiki cha Musukuma na ili iweje?

Pia, soma=> Dkt. Joseph Kasheku Msukuma: Napitia post za wanaonibeza mitandaoni, kuanzia Ijumaa nitaanza kuwajibu

1638783209299.png
 
Nilipokuwa sekondari Kuna mwandishi mmoja wa vitabu mwenye jina la kihaya nimemsahau alileta TAFRANI kwa baadhi ya VIONGOZI kwa kuwataja kuwa si madaktari wa kweli.

Kuhusu hizi "HONORIS CAUSA" aliyopatiwa mh.Musukuma anaweza kupewa yeyote mwenye MCHANGO katika jamii. Hoja tu ni kutoka CHUO KIKUU GANI CHENYE ITHIBATI ZILIZOSIMAMA.

Hata Nassib Abdul "alias" Diamond Platinumz naye ana SHAHADA ya heshima kutoka UDSM.
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA[emoji116][emoji116][emoji116]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa nimejua. Siku za karibuni Kuna mtu aliniita kutokea Arusha akaniambia jina langu limependekezwa ili nipewe udaktari wa heshima kwa sababu (akataja nyingi). Kisha akasema zinatakiwa dola 500 haraka sana na deadline ni siku ya pili yake. Akataja chuo hikihiki.

Nikamwambia hiyo hela Sina. Akasema basi leta dola 210 kwa punguzo maalum.

Nikamwambia kwa Sasa Kuna vyuo vikuu 3 humu duniani vinaniomba nipokee udaktari wa heshima kutoka kwao lakini itaambatana na cheki ya dola elfu kumi kwangu. Nikamwambia bado nasita kwa sababu walizonitajia kuwa ninazo bado nina mashaka nazo kama ninazo kweli. Tukaachana hivo.

Kumbe wakapatikana kina Msukuma?!
 
Back
Top Bottom