Philip Basiimire CEO mpya Vodacom Tanzania

Philip Basiimire CEO mpya Vodacom Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kampuni ya Vodacom Tanzania imetangaza kumteua Ndg. Philip Besimire kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya kuanzia Oktoba 25, 2022.

Philip anajiunga kutokea kampuni ya MTN ya Afrika Kusini, alipokuwa na wadhifa wa Afisa Mkuu wa Mauzo, Usambazaji na Uendeshaji.

Besiimire anachukua nafasi ya Hilda Bujiku ambaye alikuwa akitumikia nafasi hiyo kama Kaimu Mkurugenzi kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Sitholizwe Mdlalose.

Philip anakuja na uzoefu wa kimataifa wa uongozi na ufahamu mkubwa unaoendana na nafasi hii muhimu. Uteuzi wake unaakisi jitihada za Bodi ya Vodacom Tanzania kuimarisha nafasi ya kampuni hiyo katika sekta hii muhimu na kuendeleza kauli mbiu ya Vodacom - kuiongoza Tanzania katika ulimwengu wa kidigitali na kubadili maisha ya Watanzania kupitia Teknolojia.

Katika uzoefu wake wa miaka 15 katika MTN, pia aliwahi kuwa mkuu wa masoko na kaimu Mkurugenzi Mtendaji nchini Eswatini (Swaziland).

Vodacom imesema kuwa katika uteuzi wa Besimiire ni ishara ya wapi wanatamani kwenda kwa pamoja huku wakipanua nafasi zao na kuendelea kutekeleza mkataba na madhumuni yao ya kijamii ambayo wanasema ni kuifikisha Tanzania katika zama za kidijitali na mabadiliko ya maisha. kupitia teknolojia.

Besimiire ana Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara kutoka Uholanzi na Shahada ya Kwanza ya Sanaa katika sayansi ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Makerere Kampala, Uganda.

47181f3d-f438-44d0-80a1-73bf9103e8bb.jpg
 
Elimu ya bongo tujitathimini.kwa makampuni haya makubwa ni ngumu kabisa kumkuta mtanzania kuwa mkurugenzi.Sisi tumebanana tu kwenye ajira za kujipendekeza ili uteuliwe(siasa)
 
Kwa surname yake,huyu atakuwa Mganda,
Ni mganda

Philip Besiimire has a Bachelor of Science in Social Sciences from Makerere University in 1999 and a Master of Business Administration in Marketing from BSN Nederland in 2008.
 
Hapo voda hio nafasi ya uceo ni kwa ajili ya watu wa nje tu huyo kaimu hilda bujiku mbona cv yake iko poa tu
 
Back
Top Bottom