Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Mangula ameachia nafasi ya umakamu mwenyekiti CCM, kaona isiwe tabu.

Ila hii Ni Mara ya Pili mzee anawekwa pembeni, sijajua ana tatizo gani na wenzio huko.

Nafasi imechukuliwa na Kinana

Membe karudishwa CCM

===

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula leo Alhamisi Machi 31, 2022 amewasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia nafasi hiyo.

Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ambapo atachukua nafasi ya Philip Mangula.

Kikao hicho kimefanyika leo 31 Machi 2022 Jijini Dodoma.


Pia soma;

1). Nashauri Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula ang'atuke na akabidhi mikoba kwa Abdulrahman Kinana

2). Ukatibu Mkuu CCM: Nani anafaa kuchukua nafasi ya Daniel Chongolo? Kinana ndani

Kwa sasa nadhani umri umeenda sana.
 
Sera za kuhamasisha uhai wa chama kwa kutumia ubwabwa na magharagwe zarudi kwa kasi ya kazi iendelee . Muda si mrefu Mungu ataonesha Neema yake juu ya Tanzania atanyanyua mawe ya tetee wanyonge na maskini wa Taifa hili.
Jiwe lilishainuka likakataliwa,kazi iendelee
 
Naona wengi wanatoa maoni humu kuwa kurudi kwa Kinana na kuwa Makamu wa Mwenye kiti, basi tembo na twiga nk wataumizwa sana. Ina maana huyu mzee Kinana ndiye aliyekuwa ana husika na kuumiza wanyama awamu zilizopita? Kwa maoni ya wengi inaonekana ni kweli huyo mzee anahusika kwa mambo hayo.
 
Hiyo ni mikakati ya 2025

Abdrahaman kinana mpanga mipango
 
Radio mbao zinasema mzee wa mikakati anaingia kuupanga uchaguzi wa 2025.
Na bado watu hawaelewi ulichoandika hapa!

Timu nzima sasa ni kamilifu: Kinana, Nape, Makamba..., ni kama ujio wa mara ya pili wa Kikwete.

Nani tena aliyeko huko ndani mwenye vinasaba vya Magufuli? Hakuna.

Sasa ndio "Kazi Inaendelea" barabara hadi 2025.
 
Rais
Waziri mkuu
Katibu mkuu kingozi
Makamu mwenyekiti hapo ni Islamic state kweli.
Mr shaka , mwenezi wa ccm,
Riziwani kikwete
January makamba
Wazuri wa viwanda na uwekezaji
Waxiri wa kilimo na mifugo
Naibu spika
 
Ndo mwisho wao wa kufikiri? Kwanini hawatengenezi timu ya majina mapya tunarudia rudia yaleyale?
Wapore tena mali za chama!

Recycling old, tired, corrupt people. CCM kwa sasa hakina maono, umakini, utashi, mikakati ya kusaidia na kuwazesha Watanzania.

CCM ya sasa ipo kwa ajili ya genge fulani, familia chache, watoto wao na washkaji wao.
 
Sera za kuhamasisha uhai wa chama kwa kutumia ubwabwa na magharagwe zarudi kwa kasi ya kazi iendelee . Muda si mrefu Mungu ataonesha Neema yake juu ya Tanzania atanyanyua mawe ya tetee wanyonge na maskini wa Taifa hili.
Watz ni wapumbavu Mungu hawezi kushughulika nao tena

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Hhahahaha

Yaan Mwenyekiti akiwa Samia, Makamu Kinana na Katibu Chongolo inakuwa udini

Ila ikiwa Mwenyekiti John, Makamu Philip na Katibu Bashiru inakuwa hakuna udini
Mwenyekiti - samia suluhu hassan
makamu mwenyekiti/bara - Abdulrahmani kinana
makamu m/kiti visiwani - hussein ally mwinyi/ally mohamed shain
Katibu mwenezi shaka hamdu shaka
Katibu mkuu - Daniel chongolo
Naibu katibu mkuu Alhaji ?????
 
Back
Top Bottom