Picha Adimu za Historia ya Kupigania Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PICHA ADIMU ZA HISTORIA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

Nimepokea picha kutoka kwa Mshindo Ibrahim ikimuonyesha marehemu baba yake Mzee Ibrahim Mwinyimvua Makongwa aliyepata kuwa Mwenyekiti wa TANU Iringa wakati Tanganyika ilipopata uhuru mwaka wa 1961 akimuaga uwanja wa ndege wa Iringa Provincial Commissioner wa Southern Highlands baada ya Tanganyika kuwa huru.

Historia ya TANU na harakati za kudai uhuru bado inahitaji kufanyiwa utafiti ili isipotee na nchi kupoteza historia ya mashujaa walioikomboa Tanganyika kutoka mikono ya ukoloni.

344982848_545845947709387_4130162373379589840_n.jpg

Mzee Ibrahim Mwinyimvua Makongwa Mwenyekiti wa TANU akimuaga Provincial Commissioner wa Nyanda za Juu akiondoka Tanganyika baada ya Sherehe za Uhuru December 1961.
 
Tuendelee kutafuta walioshiriki harakati za uhuru kutoka ule upande wa wavaa makobazi ili kuonesha na kuaminisha jamiii kuwa tulipambania ila tulipuuzwa na mjanja kutoka butiama

Shida hao unaojaribu kuwatetea walikua wanywa kahawa tu Nyerere aliwasoma kitambo sana, ukitaka kuamini hawa watu ni wepesi we mpatie Hela ndogo ndogo za kahawa, alkasus pia mhakikishie upatikanaji wa mitende
 
Ndio uwezo wako wakufikiri umeishia hapo? kwahiyo wewe unawazidi akili watu wote ambao sio member wa JF?
Uliaminishwa na nani kua akili ya mtu inapimwa kwa kuangalia kajiunga JF lini? kwa taarifa yako nipo JF kabla yako ila kwa ID nyingine,
Punguza upumbavu.
Wewe ni mpumbavu huna ulijuwalo hapa JF.

Angalia aliyekupa like kwa post yako hii ya kipumbavu huenda ukaanza kupata Mwanga.
 
UHURU umeshindwa kumkomboa mwafrika umekuwa ni faida kwa wachache, maisha ya waafrika yamerudi nyuma baada ya UHURU kuanzia miaka ya 80s
 
Harakati za UHURU zilianza na waislamu wa pwani wao ndio walimkaribisha Mwalimu na kumpa kijiti awaongoze sababu alikuwa msomi
 
Wewe ni mpumbavu huna ulijuwalo hapa JF.

Angalia aliyekupa like kwa post yako hii ya kipumbavu huenda ukaanza kupata Mwanga.
Nilijua tu unaendeshwa na chuki za udini,wewe ulitaka nani anipe like ili uone kua ndio sawa? unataka kuwapangia mpaka watu jinsi ya kutoa likes zao?

Ukiwa mpumbavu jaribu kupiga kimya ili usijulikane kua wewe ni mpumbavu.
 
Harakati za UHURU zilianza na waislamu wa pwani wao ndio walimkaribisha Mwalimu na kumpa kijiti awaongoze sababu alikuwa msomi
Showman,
Julius Nyerere hakuwa msomi pekee.

Kulikuwa na wasomi wengi katika TAA: Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, Hamza Mwapachu, John Ketto, Chief David Kidaha Makwaia na wengine wengi.

Abdul Sykes kipindi hicho 1953 alikuwa keshapata nafasi ya kuingia Princeton University, New Jersey.

Hiki ni kisa kati ya Abdul Sykes na Earle Seaton.

Ukisoma barua ya Earle Seaton kwa Abdul Sykes kuhusu kwenda Princeton University kipindi kile na siasa zilivyokuwa moto utaelewa TAA ilikuwa na viongozi wa uwezo upi.

Mwalimu alikuwa na bahati moja kuwa kwanza alikuwa rafiki wa Hamza Mwapachu na Hamza na Abdul Sykes walikuwa marafiki.

Hamza yeye alimtaka Abdul amtie Nyerere kwenye "circle" achukue uongozi badala ya Chief Kidaha Makwaia ambae Abdul alimtaka.

Yapo na mengine.

Ni bahati mbaya sana kuwa huijui historia ya Mwalimu na yeye mwenyewe hakupenda historia yake ifahamike.

Hii ndiyo sababu wengi wenu leo mnajifunza upya historia ya Mwalimu Nyerere.
 
"Ni bahati mbaya sana kuwa huijui historia ya Mwalimu na yeye mwenyewe hakupenda historia yake ifahamike "

Nikweli hili limeleta shida sana kwakuwa Mwl. Nyerere halupenda historian yake ifahike
 
Showman,
Julius Nyerere hakuwa msomi pekee.

Kulikuwa na wasomi wengi katika TAA: Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, Hamza Mwapachu, John Ketto, Chief David Kidaha Makwaia na wengine wengi.

Abdul Sykes kipindi hicho 1953 alikuwa keshapata nafasi ya kuingia Princeton University, New Jersey.

Hiki ni kisa kati ya Abdul Sykes na Earle Seaton.

Ukisoma barua ya Earle Seaton kwa Abdul Sykes kuhusu kwenda Princeton University kipindi kile na siasa zilivyokuwa moto utaelewa TAA ilikuwa na viongozi wa uwezo upi.

Mwalimu alikuwa na bahati moja kuwa kwanza alikuwa rafiki wa Hamza Mwapachu na Hamza na Abdul Sykes walikuwa marafiki.

Hamza yeye alimtaka Abdul amtie Nyerere kwenye "circle" achukue uongozi badala ya Chief Kidaha Makwaia ambae Abdul alimtaka.

Yapo na mengine.

Ni bahati mbaya sana kuwa huijui historia ya Mwalimu na yeye mwenyewe hakupenda historia yake ifahamike.

Hii ndiyo sababu wengi wenu leo mnajifunza upya historia ya Mwalimu Nyerere.
Mbona wasomi wengi ni Wagalatia.
 
Mbona wasomi wengi ni Wagalatia.
Ngongo,
Mimi sipendi hizi "name callings" na yote yanayodhalilisha.

Wasomi wengi ni Wakristo kwa kuwa Wamishionari ndiyo waliotangulia kufika Tanganyika wakafuatiwa na Wajerumani na Waingereza.

Wamishionari mfano Johann Krapf kafika kawakuta Waislam wamelimika wanajua kusoma kuandika na hisabati wakitumia hati za Kiarabu.

Wamishionari hawakupendezwa.
Walipoingia wakoloni Wamishionari na wakoloni wakaungana kupiga vita Uislam na kila kitu kilichofungamana na Uislam.

Hati za Kiarabu na madrasa zilizokuwa ndiyo vituo vya elimu kwa Waislam zikapigwa marufuku na elimu ikawa inatolewa kwa ubaguzi katika shule za Wamishionari na za serikali.

Ili mtoto wa Kiislam asome ilibidi aukane Uislam na kubatizwa.

Hiki kikawa kikwazo kikubwa kwa Waislam.

Hii ndiyo sababu ya Waislam kukosa elimu na pia ndiyo sababu Waislam wakawa mstari wa mbele katika kuunda African Association 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 na TANU 1954 kupambana na ukoloni.
 
Ngongo,
Mimi sipendi hizi "name callings" na yote yanayodhalilisha.

Wasomi wengi ni Wakristo kwa kuwa Wamishionari ndiyo waliotangulia kufika Tanganyika wakafuatiwa na Wajerumani na Waingereza.

Wamishionari mfano Johann Krapf kafika kawakuta Waislam wamelimika wanajua kusoma kuandika na hisabati wakitumia hati za Kiarabu.

Wamishionari hawakupendezwa.
Walipoingia wakoloni Wamishionari na wakoloni wakaungana kupiga vita Uislam na kila kitu kilichofungana na Uislam.

Hati za Kiarabu na madrasa zilizokuwa ndiyo vituo vya elimu kwa Waislam zikapigwa marufuku na elimu ikawa inatolewa kwa ubaguzi katika shule za Wamishionari na za serikali.

Ili mtoto wa Kiislam asome ilibidi aukane Uislam na kubatizwa.

Hiki kikawa kikwazo kikubwa kwa Waislam.

Hii ndiyo sababu ya Waislam kukosa elimu na pia ndiyo sababu Waislam wakawa mstari wa mbele katika kuunda African Association 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 na TANU 1954 kupambana na ukoloni.
Ww mbona ulisoma mission st Joseph forodhani!!. nitajie jina lako la ubatizo?
 
Tueleze hiyo historia nyingine.. nje ya hapo ni chuki zako na udini
Madogo hapa jamvini kama kina The Icebreaker ila tunaokujua sie tunakuelewa vyema mission zako cc Ngongo Dr Matola PhD
Inside...
Katika mambo yaliyonistaajabisha na sikuyategemea kabisa ni kujulikana kama ulivyoandika.

Mimi hakika ninayo chembelecho, "mission," nayo ilikuwa kuandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na kueleza mchango wqa wazee wangu na wengine ambao historia iliwasahau.

Nashukuru kama ulivyosema kuwa naeleweka vyema.

Ikiwa wewe unaona mtu kuandika historia mfano wa hii yangu ni chuki na udini wajibu wangu ni kuheshimu fikra zako.

Kuhusu historia nyingine hivi punde katika jukwaa hili nimeweka post mpya.
 
Back
Top Bottom