Picha Adimu za Mkutano wa Kura Tatu Tabora 1958

Picha Adimu za Mkutano wa Kura Tatu Tabora 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Athmani Kondo ni mmoja wa Wazee Mashuhuri na Maarufu wa Tabora walionialika kuzungumza katika Kongamano la CCM kuhusu mchango wa Tabora katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nilizungumza Ukumbi wa Chuo Cha Uhazili Tabora.

Athmani Kondo ameniletea picha hizo hapo chini zikionyesha mambo kama yalivyokuwa katika Mkutano wa TANU wa mwaka wa 1958 kujadili Kura Tatu.

Hizi ni picha adimu kupita kiasi ambazo zingestahili kuning'inizwa katika kuta za Makao Makuu ya CCM Dodoma na hali kadhalika kuhifadhiwa Makumbusho ya Taifa.

1741360281946.jpeg

Mapokezi ya Rais wa TANU na wajumbe wa mkutano Ofisi ya TANU Barabara ya Usagara, Gongoni Ofisi ya TANU ilikuwa katika nyumba ya kupangisha ya Issa Kibira.
1741360435517.jpeg

Julius Nyerere na Bibi Titi wakiwa na wenyeji wao majina yao hayakuweza kupatikana.
1741360541646.jpeg

Ndani ya ukumbi wa mkutano wa Kura Tatu Parish Hall, Tabora.
1741360710506.jpeg

Wananchi wakielekea Uwanja wa Polisi kuhudhuria mkutano wa TANU baada ya TANU kupitisha Azimio la Busara kuamua kushiriki Kura Tatu.
1741360845753.jpeg

Mkutano wa hadhara wa TANU Uwanja wa Polisi Mwalimu Nyerere alizungumza na katika ya hotuba alinyamaza na kulia akisema kuwa ikiwa Waingereza hawatakubali kutoa uhuru TANU itamshtakia Mungu. Uwanja mzima uliangua kilio.
 
Athmani Kondo ni mmoja wa Wazee Mashuhuri na Maarufu wa Tabora walionialika kuzungumza katika Kongamano la CCM kuhusu mchango wa Tabora katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nilizungumza Ukumbi wa Chuo Cha Uhazili Tabora.

Athmani Kondo ameniletea picha hizo hapo chini zikionyesha mambo kama yalivyokuwa katika Mkutano wa TANU wa mwaka wa 1958 kujadili Kura Tatu.

Hizi ni picha adimu kupita kiasi ambazo zingestahili kuning'inizwa katika kuta za Makao Makuu ya CCM Dodoma na hali kadhalika kuhifadhiwa Makumbusho ya Taifa.
wapi picha..?
 
Huyu mzee athumani kondo in Early 1980 alikuwa ni afisa wa shirika la ndege Tanzania. Is it right
 
Back
Top Bottom