Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Shukran sana mzee MS nakupongeza kwa ujasiri wako haya maandiko yako unayo yaandika bila ujasiri ulionao sirahisi kuyaandika.
Dunia hii ya leo yenye uhuru wa kuandika utegemee kupata mjibu machafu zaidi ya maandiko lakini nadhani kwa umri wako na elmu yako unao uwezo wakuhimili.
 
Salahsahim,
Nashukuru kuwa nimesema kile kilichotakiwa kusemwa.

Marehemu Ahmed Rashad Ali alikuwa rafiki mkubwa wa Abdul Sykes zilipoanza kejeli juu African Association alikuwa akimwambia Abdul aeleze ukweli wa chama.hicho.

Propaganda zilikuwa kuwa TAA hakikuwa chama cha siasa bali cha starehe na Nyerere ndiye aliyeunda TANU.
Abdul alikuwa akikataa kusema lolote vipi baba yake na yeye na mdogo wake Ally walivyofanya juhudi ya kuunda TANU toka 1945.

Hali hii ilidumu kwa miaka mingi na hata historia ya TANU ilipokujaandikwa na Chuo Cha Kivukoni 1981ilimtaja Nyerere peke yake. Namshukuru Allah kwa kuniwezesha kuiandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.
 
Mkuu Mohamed Said, hakika makala zako kuhusu Tanganyika zinavutia, hasahasa pale unapoambatanisha na picha za enzi hizo.

Ila punguza hisia za udini kwenye hizi makala ili jamii nzima ifaidi elimu hii.

Ni ushauri tu mzee wangu.
 
Jungle Warrior,
Nimeandika kitabu cha Abdul Sykes (London)na kilipita kwa mhariri.

Nimeandika kitabu kingine Torch on Kilimanjaro (Nairobi).
Nimeandika Uamuzi wa Busara (Nairobi).

Nimeandika kama mchangiaji katika Dictionary of African Biographies (DAB)
(New York).

Vitabu hivi vyote vimepita katika mikono ya wahariri wajuzi wa Oxford
Nairobi na New York na wachapaji wengine.

Hakuna hata mhariri mmoja aliyenieleza lolote kuhusu udini katika vitabu
vyangu.

Sasa labda wewe unifahamishe kipi unachokiona ni udini katika haya ninayoandika.
Ni ushauri tu kutoka kwangu.
 
Back
Top Bottom