Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Kuna mambo ambayo yana ashiria lengo lake lilikua udini. Haya ni pamoja na suala la
Kura tatu kabla ya uhuru , hili waislam walilamika sana nini matokeo yake!
Kuvunjwa kwa baraza la wazee walokua chachu ya kudai uhuru na kumbeba Nyerere
Kuvunjwa kwa jumuia yenye nguvu ya waislam na kuundiwa Bakwata
Sheria ya ndoa
Kutaifisha mashule
Azimio la Arusha na kutaifisha mali na nyumba za watu mijini
Na vijiji vya ujamaa
Yote haya yalikuwa na direct impact na waislam na hali zao. Ukitaka kujua how ni kuingalia kila item kwa upeo wake utagungua tatizo la udini.

Crabat,
Nakusihi ndugu yangu hapana haja ya kulizungumza tatizo hili la udini katika
nchi yetu.

Haya tulosema yanatosha.
 
Huwezi kuona hata picha moja ya wapigania uhuru mapdri au maaskofu,uhuru wa nchi hii kwa sana umepiganiwa na waislamu, lakini ndio wanaongoza kudharauliwa na kizazi cha sasa inasikitisha sana

Hizo ni picha za wapigania Uluru Dar es salaam ...mikoani pia kulikuwa na harakati za kupinga ukoloni Tena za damu
 
Nimesema hakuna padri wala mchungaji aliyepigania uhuru, kama wewe unabisha weka picha kumuonyesha yyte aliyekuwa katika harakati hizo,
 
Juhudi za wana Mzizima kuweka vuguvugu la Uhuru ...ukiwasha Barua hawakuwahi kufanya mkutano ...wowote wa harakati nje ya Kariakoo na Magomeni ...Huo ndio udhaifu mkubwa wa Watu wa Mzizima ...kuamini kuwa Kila KITU kilichoongelewa pale New street ...na mitaa ya msimbazi ..na jioni kwenye dhumna au Kahawa ni cha NCHI nzima .....hatukatai harakati zikianza Dar Ila udhaifu mkubwa waliofanya ni kutokueneza chama nje

TAA na baadaye TANU Ilianza kufanya ziara mikoani kwa kasi Baada ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ,Rashid Kawawa ,Oscar Kambona ,Titi Mohamed ...na wengine kuingia na kufanya ziara ndefu sana mikoani ...Hii ndio iliunganisha Juhudi zilizokuwa zikiendelea Dar na Kina Paul Bomani ( Ziwa ) , George Kahama ( kagera ), hamza mwapachu ( Tanga ) , abdala said fundikira ,kasela bantu ,kasanga tumbo ( tabora ) , chief kunambi ( tabora ) Amir kaluta ( kigoma ) , Japhet killiro ( Arusha ) , chief marealle ,chief shangali ,Nsillo Swai ( Kilimanjaro ) ...na wengine wengi

Tanzania haingeweza kupata Uhuru Kama TANU au TAA ingendelea kubaki mitaa wa Lumumba !!!! Kwa Baadhi ya maeneo hata ya Kaskazini walikuwa wanakaribiwa kupewa free state ..Hadi Mwalimu alipofika na kutaka Province zote ziunganishe nguvu .....Sasa unawezaje Kusema kuwa Uhuru ulidaiwa Dar tu Kama tayari sehem Kama Kilimanjaro walishafikia kuwa na serikali ya Ndani ya Wenyeji ( native Gorvernment ) ..yenye Ikulu , mahakama , walinzi na mawaziri ...the only second after Buganda In the region ...hata Kikuyu Kenya hawakuwahi kuwa na serikali ya Ndani
 
Wewe huna mamlaka ya kuhodhi suala lolote juu ya nchi hii.

Ngongo,
Hilo suala la Nyerere kuwa au kutokuwa mdini nani wa kupitisha hukumu?
Wewe au mie?

Hili tulishalizungumza hapa na rejea kadhaa zikatolewa.
Sidhani kama kuna haja kwa sasa kulichokonoa hili jambo zaidi.
 
Hili nalo neno.

Juhudi za wana Mzizima kuweka vuguvugu la Uhuru ...ukiwasha Barua hawakuwahi kufanya mkutano ...wowote wa harakati nje ya Kariakoo na Magomeni ...Huo ndio udhaifu mkubwa wa Watu wa Mzizima ...kuamini kuwa Kila KITU kilichoongelewa pale New street ...na mitaa ya msimbazi ..na jioni kwenye dhumna au Kahawa ni cha NCHI nzima .....hatukatai harakati zikianza Dar Ila udhaifu mkubwa waliofanya ni kutokueneza chama nje

TAA na baadaye TANU Ilianza kufanya ziara mikoani kwa kasi Baada ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ,Rashid Kawawa ,Oscar Kambona ,Titi Mohamed ...na wengine kuingia na kufanya ziara ndefu sana mikoani ...Hii ndio iliunganisha Juhudi zilizokuwa zikiendelea Dar na Kina Paul Bomani ( Ziwa ) , George Kahama ( kagera ), hamza mwapachu ( Tanga ) , abdala said fundikira ,kasela bantu ,kasanga tumbo ( tabora ) , chief kunambi ( tabora ) Amir kaluta ( kigoma ) , Japhet killiro ( Arusha ) , chief marealle ,chief shangali ,Nsillo Swai ( Kilimanjaro ) ...na wengine wengi

Tanzania haingeweza kupata Uhuru Kama TANU au TAA ingendelea kubaki mitaa wa Lumumba !!!! Kwa Baadhi ya maeneo hata ya Kaskazini walikuwa wanakaribiwa kupewa free state ..Hadi Mwalimu alipofika na kutaka Province zote ziunganishe nguvu .....Sasa unawezaje Kusema kuwa Uhuru ulidaiwa Dar tu Kama tayari sehem Kama Kilimanjaro walishafikia kuwa na serikali ya Ndani ya Wenyeji ( native Gorvernment ) ..yenye Ikulu , mahakama , walinzi na mawaziri ...the only second after Buganda In the region ...hata Kikuyu Kenya hawakuwahi kuwa na serikali ya Ndani
 
hii makala imenifungua kitu kimoja, ndio maana nyerere pindi likitokea jambo alikua anaongea na wazee wa darisalama!...
 
wa africa bwana na hisia potofu za dini walizoletewa na watu toka nje hadi wanasahau maana halisi ya huu uzi.nice thread ila mnaweka dini zenu mbele unaweza kuta hao mnao waongelea unaweza kuta hata hawakuna mitizamo mliyo kuwa nayo.
 
Juhudi za wana Mzizima kuweka vuguvugu la Uhuru ...ukiwasha Barua hawakuwahi kufanya mkutano ...wowote wa harakati nje ya Kariakoo na Magomeni ...Huo ndio udhaifu mkubwa wa Watu wa Mzizima ...kuamini kuwa Kila KITU kilichoongelewa pale New street ...na mitaa ya msimbazi ..na jioni kwenye dhumna au Kahawa ni cha NCHI nzima .....hatukatai harakati zikianza Dar Ila udhaifu mkubwa waliofanya ni kutokueneza chama nje

TAA na baadaye TANU Ilianza kufanya ziara mikoani kwa kasi Baada ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ,Rashid Kawawa ,Oscar Kambona ,Titi Mohamed ...na wengine kuingia na kufanya ziara ndefu sana mikoani ...Hii ndio iliunganisha Juhudi zilizokuwa zikiendelea Dar na Kina Paul Bomani ( Ziwa ) , George Kahama ( kagera ), hamza mwapachu ( Tanga ) , abdala said fundikira ,kasela bantu ,kasanga tumbo ( tabora ) , chief kunambi ( tabora ) Amir kaluta ( kigoma ) , Japhet killiro ( Arusha ) , chief marealle ,chief shangali ,Nsillo Swai ( Kilimanjaro ) ...na wengine wengi

Tanzania haingeweza kupata Uhuru Kama TANU au TAA ingendelea kubaki mitaa wa Lumumba !!!! Kwa Baadhi ya maeneo hata ya Kaskazini walikuwa wanakaribiwa kupewa free state ..Hadi Mwalimu alipofika na kutaka Province zote ziunganishe nguvu .....Sasa unawezaje Kusema kuwa Uhuru ulidaiwa Dar tu Kama tayari sehem Kama Kilimanjaro walishafikia kuwa na serikali ya Ndani ya Wenyeji ( native Gorvernment ) ..yenye Ikulu , mahakama , walinzi na mawaziri ...the only second after Buganda In the region ...hata Kikuyu Kenya hawakuwahi kuwa na serikali ya Ndani

Phillemon Mikael,
Inaelekea huijui historia ya TANU.
Mikutano ya hadhara ilianza baada ya kuwa na chama cha siasa.

Isingewezekana kufanya mkutano wa hadhara wa siasa chini ya TAA.
Kwa hili hapakuwa na udhaifu wowote kwa watu wa Dar es Salaam.

Ikiwa unataka tutaje udhaifu basi huo udhaifu utafutwe kwengine ambako
hapakuwa na vuguvugu lolote dhidi ya ukoloni.

Kwa mukhtasari tu nitakueleza kuwa baada ya TANU kuundwa safari ya
kwanza mwaka wa 1954 ilikuwa Morogoro ambako Zuberi Mtemvu aliongozana
na Nyerere.

Safari ya pili ilikuwa Lindi ambako Nyerere aliongozana na Ali Mwinyi Tambwe na
safari hii ilikuwa lazima ifanyike kwa kuwa Kanisa lilikuwa linawavunja waumini wao
nguvu wasiunge mkono TANU.

Ukipenda kusoma zaidi kuhusu haya kitafute kitabu cha Abdul Sykes.

Ndani ya kitabu hiki nimeeleza nini kilifanyika kati ya 1950 - 1954 kuwaamsha
wananchi kujiunga na TAA majimboni.

Makaratasi yaliyokuwa yanamwagwa huko majimboni yalikuwa yanachapwa Mtaa wa
Kipata nyumbani kwa Ally Sykes akitumia mashine ya kudurufu aliyokuwa ameificha.

Katika utafiti wangu nimesoma haya makaratasi na yapo katika orodha ya rejea katika
kitabu cha Abdul Sykes.

Juu ya juhudi hizi kulikuwa na safari alizofanya Abdulwahid Sykes kupita majimboni
akifanya mikutano ya siri na viongozi wa TAA kuwaeleza nini kinaendelea New Street.

Katika viongozi mashuhuri aliokutananao ni Paul Bomani ukimtoa Chief Kidaha ambae
alikuwa akikutanananae nyumbani kwake Dar es Salaam.

Habari za mikutano hii unaweza kuipata katika Tanganyika Intelligence Gazette taarifa
za kikachero za Special Branch za miaka ya 1950.

Viongozi hawa walikuwa wanajua fika kuwa bila ya kuwa na umoja wa Watanganyika wote
safari ya uhuru itakuwa ndefu sana.

Bahati mbaya wewe umeweka majina tu ya kina Marealle, Kirilo, Shangali na wengineo
bila kujua historia zao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Soma kitabu cha Abdul Sykes uione historia ya uhuru wa Tanganyika kwa ukweli wake.
 
Wewe huna mamlaka ya kuhodhi suala lolote juu ya nchi hii.

Ngongo,
Siwezi kuhodhi chochote katika historia hii ila nilichokuwa na uhakika ni kuwa
historia ya TANU naijua kuliko watu wengi sana.

Ushahidi uko hapa Majlis jinsi ninavyoeleza yote yaliyojiri katika kipindi kile.
 
kwa kweli waislamu ndio waliikomboa nchi hii tuseme za ukweli.
Halafu? Baada ya kuikomboa? Wakaitelekeza au wakaisalimisha kwa Mwalimu au vipi? Nina hakika ungeweza kujiuliza haya maswali ungeuona ujinga wa dai lako.
 
Mohamed Said

My guess is,
Nyerere was like a celebrity by then na watu wengi walipiga naye picha walipopata nafasi. Na si lazima kila aliyepiga picha naye alikuwa ni "mpigania uhuru".
Maeneo fulani yalikaliwa zaidi na watu wa utamaduni/dini fulani kuliko watu wa utamaduni mwingine. Hata ingekuwa leo, Nyerere apige picha Pemba, ataonekana kama amepiga na waislam watupu.
Ninaamini kuwa alipokuwa anatembelea maeneo ya wasukuma au wamasai (kama picha zitawekwa za enzi hizo), picha zitaonesha kuwa ni watanzania wa kawaida wa asili ya kisukuma au kimasai ndio walimpiga "tafu" kwenye mambo ya uhuru. Pia ninaamini kuwa zilikuwepo picha nyingi zilizopigwa wakati huo lakini hazikukidhi ule mtazamo wa mwandishi. It is therefore no coincidence, kwa tunavyokufahamu Mohamed Said, kubandika picha zilizopigwa DSM na kuziacha za sehemu nyingine ili tu kukidhi haja yako ya kuonesha kuwa watu fulani wamesahaulika.

Uhuru ulitafutwa maeneo ya Pwani na kidogo Tabora mjini kwa maustaz pia wala sio huko kwa Wamasai na Wasukuma.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom