Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Massa,
Siwezi kulipa hisani ambayo JF wamenifanyia mimi.
Nani akinijua kabla sijaandika JF?

Hakika sina cha kuilipa JF.
Hata kama nitaanzisha jukwaa langu halitaweza hata kwa mbali kuifikia JF.
Huyu mzee Kiswahili cha kulainisha anakijua sana-katika kuongea kama ni hivi hivi, basi ni mtu hatari sana
 
Jembepori,
Maswali unayouliza hayaendani na mnakasha uliopo Majlis.
Narudia unajadili kitabu ambacho hujasoma.

Kasome kitabu kwanza ukimaliza kusoma rudi jamvini tujadili.
 
Jackline,
Usitishike na lugha.
Mie sina "vernacular."

Kiswahili ndiyo "mother tongue" yangu.

Wala mimi si mtu hatari.

Kilichokugusa wewe ni kuwa hukutegemea
jibu lile.

Ukweli ni kuwa JF ndiyo walonipa uwanja na watazamaji tena
bila malipo yoyote.
 
Huyu mzee Kiswahili cha kulainisha anakijua sana-katika kuongea kama ni hivi hivi, basi ni mtu hatari sana

Umejuwaje kama ni "hatari" sana? Kwa ulaini wa lugha yake tu? Au kwa Uislam wake?
 
WAZEE+WA+TANU.jpg

Waliokuwa Katika Picha Hii na Ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU
(Wengine: Hawapo)

  1. [*=left]Abdallah Shomari (Tandamti No. 3)
    [*=left]Nassoro Kalumbanya (Simba)
    [*=left]Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo)
    [*=left]Mtoro Ally (Muhonda)
    [*=left]John Rupia (Misheni Kota)
    [*=left]Julius Nyerere (Pugu Sekondari)
    [*=left]Said Chaurembo (Congo/Mkunguni)
    [*=left]Jumbe Tambaza (Upanga)
    [*=left]Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
    [*=left]Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande)
    [*=left]Mshume Kiyate (Tandamti)
    [*=left]Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo)
    [*=left]Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
    [*=left]Rajab Simba (Kiungani)
    [*=left]Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala)
    [*=left]Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
    [*=left]Makisi Mbwana (Aggrey/Congo)
    [*=left]Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
    [*=left]Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo).

Kwa post hii, nimezidi kumkubali Nyerere. Hakuwa mdini kabisa.

Mungu aendelee kumrehemu na hawa wazee wetu ( ambao wameshatangulia mbele ya haki) ambao wametufikisha hapa tulipo kwa moyo wa kishujaa sana.

Wazungu na Waarabu wamefanikiwa sana kutubagua watanzania na hizi dini zao.

Ntabakia kuwa mwafrika na kufuata imani ya mababu zangu.
 
Tazama Nyerere kazungukwa na wadini wangapi hapo?

Ikiwa Udini ni Uislam, basi kwa hakika Nyerere hakuwa mdini. Ila hao Waislam waliompokea, wakamuheshimu, wakamuenzi kwa usomi wake, wakala nae, wakalala nae, wakamfundisha Kiswahili, ndiyo walikuwa wadini wakubwa sana.
 
Tzama Nyerere kazungukwa na wadini wangapi hapo?

Ikiwa Udini ni Uislam, basa kwa hakika Nyerere hakuwa mdini. Ila hao Waislam waliompokea, wakamuheshimu, wakamuenzi kwa usomi wake, wakala nae, wakalala nae, wakamfundisha Kiswahili, ndiyo walikuwa wadini wakubwa sana.

Hapana. Na wao pia hawakuwa wadini bali wenye upendo mkubwa.

Hao wazee na huyu Julius wote kwa pamoja hawakuwa wadini.

Nashangaa udini umeanzia kwenye kizazi hiki.

Wenye madini yao Uarabuni na Ulaya huko wametulia. Sisi miafrika tunajifanya tunazijua dini zao kuwashinda. Afu tunabaguana. Majinga sana sisi.....

Ama kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo.... nakubaliana na komredi Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:

Udini ulianzishwa na Nyerere.

Rais wa Kiafrika ambae anataka kupewa Utakatifu na Kanisa lake, kwa lipi zaidi? Fikiri.
 
Udini ulianzishwa na Nyerere.

Rais wa Kiafrika ambae anataka kupewa Utakatifu na Kanisa lake, kwa lipi zaidi? Fikiri.

Kumbe?

Hivi alitaka kupewa utakatifu?? Kweli?? Au kuna watu wanajipendekeza kumpa?? Kabla ya kifo chake sijawahi kusikia akitaka afanywe mtakatifu.

Anyway, mi si mdini kivile. Siamini sana kwenye haya madini yenu ya kuambukizwa na ngozi nyeupe.... yaliyokuja kwa meli na ndege...

Usiku mwema mama. (kama uko kwetu huku)
 
achana na hicho kibibi kinapenda udini hujapara kuona...
 
Wewe ndiye umepotoka kidogo. Hizo kofia hazikuwa na maana wala tafsiri yoyote ya kidini hadi vijijini watu walivaa tu. Na kubaguana hakukuwepo katika jamii watu walipoishi pamoja.

Lakini Nyerere aliimarisha zaidi mshikamano wa kitaifa na matabaka yote kwa level ya taifa. Kwamba watu wa dini zote kabila zote na makundi yote waishi kwa amani wao kwa wao, wao na makundi mengine lakini pia sehemu moja kwenda nyingine ndani ya mipakaya Tanzania. Nyerere aliendelea na mtazamo wa hata kuunganisha Africa ili watu wawe wamoja na ndiyo maana aliimarisha mahusiano mipakani mwetu na ujirani mwema.

Na hii ilifanyika kwa namna nyingi ikiwemo mtoto anasomea Moshi, halafu akifaulu anapangiwa Milambo Secondary, huyu wa Nansio anapangiwa Songea Boys, na huyu wa Mafia anakwenda kusoma Murutunguru n.k. n.k. Na mtindo wa elimu sahihi yenye malengo ya kuimarisha standards za taifa. Watu walishirikiana bila tatizo. Kumbuka tunapigania uhuru hapakuwa na umoja wa kitaifa.

Nyerere ndiye alihimiza waislam waende shule za maana badala ya kuishia madrasa walizoachiwa na waarabu. Tunaona kina Kikwete wamesoma shule za mission baada ya kujanjaruka kwenye madrasa ni mauti.

Nyerere ndiye aliuunda na matumizi ya lugha moja.

Udini undini wenu huu wa kuona Bargashia ndio usilam safi, huku watu wamejaa chuki, na kuanza kuona eti wako wachache kwenye uongozi wakisahau kwamba uongozi si migawo wala dini basi ni sifa na uwezo, vimeanza wakati wa Mwinyi.

Na hii ni kwa sababu ya waislam kukosa vision na kuishi kwa manung'uniko pasipo kukubali tatizo ni mafundisho ya dini yenu kama vile watoto sasa kule Singida wanakatazwa kusoma shule, eti wanatakiwa wamfie allah, wanfundishwa Karate misikitini, au wale wanaopasishwa kwa marks za kusubu, halafu kesho waanze kusema hawapati nafasi nzuri. Hilo si tatizo?

Faiza Foxy usikwepeshe agenda.

Narudia tena, hivyo vibandiko vilivaliwa na watu wote hivyo ukiona picha za kale zinaonyesha watu wanavibandiko, usianza kujenga picha ya udini kwamba wlakuwa waislam. Vibandiko haikuwa alama ya dini kama unavyotamani kuongopea watu hapa.

Na mshikamano wa kitaifa Nyerere ndiye kaujenga. Unaharibiwa na ccm ya sasa inayogawa watu kwa misingi ya dini ujinga ujinga tu. Hilo liko dhahiri.

KWA HIYO HOJA YAKO YA UDNI ETI WAISLAM WALIMPOKEA NYERERE, KWANI WAISLAM KUPOKEA MTU NI KOSA? MBONA HAO WAISLAM NAO WALIPOKELEWA NA WATU WENGINE WASIO WAISLAM NA WAKAKIRIMIWA TU? NA HAO WENYE VIBANDIKO SIYO WOE WAISLAM. NI WATU MCHANGANYIKO, USIJICHANGANYE.

UBAGUZI WA KIDINI UMELETWA NA CCM BAADA YA NYERERE KUFA, MFUMO UKAWA DHAIFU, MAJUNGU YAKASHIKA HATAMU NA WAPUMBA.VU WAKACHUKUA SHERIA MIKONONI KULAZIMISHA KUPEWA VYEO VILA ELIMU NA UWEZO. JK KAMA ALIVYONUIA, KAWAPA VYEO KAMA NJUGU BILA KUJALI UWEZO NA SIFA SASA SEIKALI IMEMFIA. MTASEMA TENA MPEWE VYEO KWA MISINGI YA DINI? LABDA SI TANZANIA TENA.

TUNAJENG ATAIFA LENYE UMOJA NA MSHIKAMANO KAMA ALIOUACHA MWALIMU. HATUHADAIKI. TUTAWEKA WATU SAHIHI, MAHALA, SAHIHI KWA WAKATI SAHIHI BILA KUJALI DINI WALA KABILA LA MTU. UJINGA UJINGA HUU WA KUCHEZA REDE KWENYE MAISHA YA WATU ALIOUFANYA HUYU, UMELIGHARIMU TAIFA. HATURUDII.

NINAOMBA TENA WENYE TABIA ZA KUHUBIRI UDINI UJINGA UJINGA ACHENI MARA MOJA!

Mkuu mbona unajamba mpaka unaharisha
 
Kumbe?

Hivi alitaka kupewa utakatifu?? Kweli?? Au kuna watu wanajipendekeza kumpa?? Kabla ya kifo chake sijawahi kusikia akitaka afanywe mtakatifu.

Anyway, mi si mdini kivile. Siamini sana kwenye haya madini yenu ya kuambukizwa na ngozi nyeupe.... yaliyokuja kwa meli na ndege...

Usiku mwema mama. (kama uko kwetu huku)

Ukinisoma vizuri utanielewa tu.
 
Hizi picha zinaonyesha hali halisi ya wazee hawa walivyokuwa Wazalendo.
 
Mwenyezi Mungu amzidishie heri Mwl Nyerere hakuwa mdini kabisa alikaa na kuishi katikati ya watu wa dini nyingine lakini hakuwa na dharau,aliishi na watu wa kada ya chini kabisa wasiokuwa na elimu dunia labda elmu ahera bila matatizo yoyote.Hakuna kama Mwl Nyerere Tanzania itachukua miaka mingi kumpata mtu wa aina ya Mwl Nyerere.
 
Ngongo,
Hilo suala la Nyerere kuwa au kutokuwa mdini nani wa kupitisha hukumu?
Wewe au mie?

Hili tulishalizungumza hapa na rejea kadhaa zikatolewa.
Sidhani kama kuna haja kwa sasa kulichokonoa hili jambo zaidi.
 
Mwenyezi Mungu amzidishie heri Mwl Nyerere hakuwa mdini kabisa alikaa na kuishi katikati ya watu wa dini nyingine lakini hakuwa na dharau,aliishi na watu wa kada ya chini kabisa wasiokuwa na elimu dunia labda elmu ahera bila matatizo yoyote.Hakuna kama Mwl Nyerere Tanzania itachukua miaka mingi kumpata mtu wa aina ya Mwl Nyerere.

Kuna mambo ambayo yana ashiria lengo lake lilikua udini. Haya ni pamoja na suala la
Kura tatu kabla ya uhuru , hili waislam walilamika sana nini matokeo yake!
Kuvunjwa kwa baraza la wazee walokua chachu ya kudai uhuru na kumbeba Nyerere
Kuvunjwa kwa jumuia yenye nguvu ya waislam na kuundiwa Bakwata
Sheria ya ndoa
Kutaifisha mashule
Azimio la Arusha na kutaifisha mali na nyumba za watu mijini
Na vijiji vya ujamaa
Yote haya yalikuwa na direct impact na waislam na hali zao. Ukitaka kujua how ni kuingalia kila item kwa upeo wake utagungua tatizo la udini.
 
Back
Top Bottom