Hili swali ni zito sana.
Je walitajwa wakristo na wasio na dini tu katika historia ya kivukoni?
Yeye atakwambia "wazee wake" walisahaulika, na anandika historia ya wazee wake.
Huyu bwana anatumia mlango huu wa kuandika historia ya wazee wake, kutimiza nia yake ya kufarakanisha jamii huku akifikiri anawaunganisha waislam kwa ujumla wao kwa kuwafanya wawe na chuki ya pamoja dhidi ya Nyerere na ukristo. Na ana sababu yake iliyojengeka kwenye kisasi, mdingi wake ambaye alikuwa kwenye AMNUT alishughulikiwa na serikali. Lakini badala ya kuilaumu serikali kwa ujumla, anamlaumu Nyerere na ukristo. Ila hali kama hiyo ikitokea wakati Rais ni muislam, lawama haziendi kwa Rais, bali zinaenda kwa serikali inayoongozwa na anachokiita christian lobby au mfumo kristo. He is a man on a mission...
Nanren,
Unajitisha bure na unataka kuwatisha watu wengine bila sababu.
Sijapata kuona swali gumu hapa
Majlis.
Ikiwa swali nalijua nalijibu silijui nasema hilo silijui.
Ikiwa "mdingi" umemkusudia ni babu yangu
Salum Abdallah yeye
alikuwa TAA kisha TANU toka mwanzo na mwaka 1955 aliasisi
Tanganyika Railway African Union (TRAU).
Hakupatapo kuwa AMNUT na kweli alishughulikiwa mwaka wa 1964
baada ya maasi ya wanajeshi yeye na viongozi wengine wa vyama
vya wafanyakazi waliwekwa kizuizini.
Ukitaka kujua kisa cha yeye kuwekwa kizuizini nitakueleza.
We sema tu.
Ni historia kama hizi ndizo zinazonifanya kuwa mjuzi wa historia
ya Tanganyika.
Iko siku nitakuwekeeni hapa
Majlis yaliyopitikana ndani ya jela ya
Uyui, Tabora alikozuiwa babu yangu kati ya 1964 - 1965.
Bwana Jela alikuwa
Mzee Munthali na Mkuu wa Mkoa Tabora
alikuwa
Rashid Kheri Baghdelleh.
Hawa wote wakifahamiana vizuri sana na baba yangu.
Kwa ajili hii habari nitakazowawekea hapa ni kutoka "kinywa cha
farasi."
Habari zinatoka kwa
Munthali kuja kwa baba yangu.
Habari zinatoka kwa
Baghdelleh kuja kwa baba yangu.
Kutoka kwa hao wawili ndipo nilipozipokea mimi.
Unauona huo upokezi?
Sikuishia hapo.
Nimepokea habari nyingine kutoka kwa
Bilal Rehani Waikela
aliyekuwa kizuizini na babu yangu.
Waikela na babu yangu wote walikuwa mstari wa mbele kupambana
na ukoloni.
Hayo mengine uliyoandika sioni sababu ya kuyasemea.
Nanren,
Zimenifikia taarifa hivi punde kuwa gazeti la Raia Mwema la leo tarehe
6 May 2015 wamechapa makala ya
Mtemvu ambayo iko hapa
Majlis.
Wakati wewe unajitisha na historia hii ya TANU leo kuna magazeti
yanaingia katika blog yangu na wakikuta kitu cha manufaa wanakichapa.