Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Mkuu Mohamed Said naomn unisaidie vitu viwili.

la kwanza ni naomba ya kupata vitabu vyako especcially kama kuna softcopy za kudownload.

La pili,naomba unisaidie kujua akina nani kutoka kaskazini(kwa majina) walikuwa vinara wakati wa kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Nashukuru.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mohamed Said naomn unisaidie vitu viwili.

la kwanza ni naomba ya kupata vitabu vyako especcia lly kama kuna softcopy za kudownload.

La pili,naomba unisaidie kujua akina nani kutoka kaskazini(kwa majina) walikuwa vinara wakati wa kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Nashukuru.

Gazaniga,
Ikiwa uko nchini unaweza kununua kitabu cha Abdul Sykes nakala ya Kizungu
au Kiswahili Ibn Hazim Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema kwa nakala
shs: 10,000.00 au Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue.

Wanaharakati wa Kaskazini Arusha ni kundi la Japhet Kirilo na Moshi ni kundi
la Yusuf Olotu maarafu kama Yusuf Ngozi.

Hii ni kwa kuwataja wachache.
 
Shukran Sheikh,
 
Hakuna ukweli ambao Wazanzibari HAWAPENDI kuusikia kama huu na sijui kwa nini inakuwa hivyo!
John Okello atabaki kuwa mtumuhimu sana wa kukumbuka katika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar milele na milele.

Kuna Tofauti kati askari wa kukodi , Mercenary na wapigania uhuru. Okelo hakuwa mpigania uhuru bali ni askari wa kukodi kwa ajii ya kuipindua serikali halali ilochaguliwa na wananchi na pia kusimamia mauaji ya waislam .

yeye anakumbukwa pamoja na walomtuma kwa unyama alowafanyia waislam wa znz.
 
Waislam wa nchii hii sio walijitolea wao binafsi na mali zao kwa ajili ya kuona nchi hii inakua huru.
walitoa mali zao na ardhi zao kwa watanzania wenzao kama mchango wao kwa taifa hili , mfano
  1. Sheikh Mohammed Abdalla Tambaza, kila mtu anajua eneo lote la Upanga Shule Ya Tambaza, Msikiti wa Maamur , Maeneo ya Makaburi ya Kisutu , nk
  2. Mzee Mwinyi mkuu mwin'juma wa Magomeni ametoa ardhi yake kwa matumizi ya waislam na watanzania
  3. Sewa Haji , aliejenga Hospital ya Muhumbili
  4. Majengo ya Bunge ya mwanza yalotolewa na Familia ya Karimjee
  5. maeneo ya makaburi ya kinondoni
huku waislam wakijitolea hali na mali zao upande mwengine wao wakatumia nafasi hio ya uhuru kujikusannyia ardhi nyingi kwa matumizi yao wenyewe
 
Nanren,post yako No #22 umeielezea vizuri sana hii dhana ya mtu/watu fulani kutaka/kupenda kupiga picha na mtu wanaeamini kwamba ana kitu cha tofauti nao,leo umenifungua macho kwani nakumbuka baada ya mimi kuondoka kijijini kwetu mwaka 2005 kwenda kusoma,nilirudi baada ya miaka sita na kilikuwa kipindi cha sikukuu basi wote waliokuwa wananifahamu kila nilipokutana nao na akawepo mpiga pic karibu walikuwa wanapenda sana tupige picha pamoja,nahisi ni picha za ukumbusho tu na ndivyo walivyoniambia baada ya kuwauliza so,hata hao wazee hapo si ajabu walitaka tu wapige picha na Mwl Nyerere kwa ajili ya ukumbusho wao na vizazi vyao kwamba may be walishawahi kukutana na mwalimu fulani au hata mpigania uhuru wa taifa letu,yote yanawezekana na naamini kipindi hicho hakuna mtu aliyekuwa hana hamu ya angalao kukaa karibu na alipo Mwl Nyerere kutokana na title aliyokuwa amejijengea ktk jamii iliyomzunguka.
 
Last edited by a moderator:
Kuna Tofauti kati askari wa kukodi , Mercenary na wapigania uhuru. Okelo hakuwa mpigania uhuru bali ni askari wa kukodi kwa ajii ya kuipindua serikali halali ilochaguliwa na wananchi na pia kusimamia mauaji ya waislam .

yeye anakumbukwa pamoja na walomtuma kwa unyama alowafanyia waislam wa znz.

Zanzibar ilipataje uhuru na ilikua mwaka gani?
Na hiyo serikali halali iliingia vipi na chini ya rais nani madarakani kabla ya mapinduzi ya Field Marshal John Okello.?
 
Waislam wa nchii hii sio walijitolea wao binafsi na mali zao kwa ajili ya kuona nchi hii inakua huru.
walitoa mali zao na ardhi zao kwa watanzania wenzao kama mchango wao kwa taifa hili , mfano
  1. Sheikh Mohammed Abdalla Tambaza, kila mtu anajua eneo lote la Upanga Shule Ya Tambaza, Msikiti wa Maamur , Maeneo ya Makaburi ya Kisutu , nk
  2. Mzee Mwinyi mkuu mwin'juma wa Magomeni ametoa ardhi yake kwa matumizi ya waislam na watanzania
  3. Sewa Haji , aliejenga Hospital ya Muhumbili
  4. Majengo ya Bunge ya mwanza yalotolewa na Familia ya Karimjee
  5. maeneo ya makaburi ya kinondoni
huku waislam wakijitolea hali na mali zao upande mwengine wao wakatumia nafasi hio ya uhuru kujikusannyia ardhi nyingi kwa matumizi yao wenyewe

Mbona unaandika kama hujui historia yako? Hao waislamu unaodai walijitolea Mali zao kwa "watanzania" wenzao ilikua ni mwaka gani?
Punguza kukusha Madrasa, mwenzio bi faizafox kajigomboa na elimu dunia walau anajua dunia inavyokwenda.
 
Last edited by a moderator:
Zanzibar ilipataje uhuru na ilikua mwaka gani?
Na hiyo serikali halali iliingia vipi na chini ya rais nani madarakani kabla ya mapinduzi ya Field Marshal John Okello.?

Tanganyika ukenya uganda zanzibar zote zilipatiwa uhuru mmoja baada ya mwengine kuanzia 1961 . 1962 na 1963.
Zote uhuru ulipatiwa December.
Znz harakati za kugombea uhuru ziliwashirikisha wote ASP ZNP ZPPP na Umma party .
uchaguzi ulifanyika ma ZPPP na ZNP wakaunda serikali ya uhuru.
Zanzibar ikajiunga na UN mwaka huo huo ma pia ikawa mwanachama wa CWealth.
Then okelo akatumwa kufanya mapinduzi.
Uhuru wa Zanzibar ulipatikana 23 Dec. 1963
 
Mbona unaandika kama hujui historia yako? Hao waislamu unaodai walijitolea Mali zao kwa "watanzania" wenzao ilikua ni mwaka gani?
Punguza kukusha Madrasa, mwenzio bi faizafox kajigomboa na elimu dunia walau anajua dunia inavyokwenda.

Usiwe mvivu wa kufikiri.
Jisomee nani aliijenga Muhimbili na mwaka gani.
Kabla ya hapo ilikua ikiitwa jina gani. Jee hujaona hata ile wodi pale ikiitwa Sewa Haji ?

Jee huujuu ukumbi wa bunge wa mwanzo ? Ule mpaka kedho unsitwa karimjee

Jee huijui shule ys Tambaza ? Kile kiwanja na shule ys muhimbili vyote ni ardhi za familia ya Mzee Tambaza.
Jee huyajui makaburi ya kisutu?
Na pale makaburi mnayozikana kinondoni zote zile ni ardhi za waislam.
 
Last edited by a moderator:
Nnahisi kwa kuwa hilo ni baraza la wazee, Ali Sykes siku hizo ni kijana.

Wewe Shori acha mambo ya kuhisi; mbona Dossa Azziz aliyekuwa umri mmoja na Ally sykes yumo kwenye hiyo picha?
 
Mzee Mo:said na wazee wake wa k/koo,enzi hizo k/koo na migo nyumba za udongo,hao wenye baskeli miaka hiyo walikuwa wanazo kweli kweli.
 
Usiwe mvivu wa kufikiri.
Jisomee nani aliijenga Muhimbili na mwaka gani.
Kabla ya hapo ilikua ikiitwa jina gani. Jee hujaona hata ile wodi pale ikiitwa Sewa Haji ?

Jee huujuu ukumbi wa bunge wa mwanzo ? Ule mpaka kedho unsitwa karimjee

Jee huijui shule ys Tambaza ? Kile kiwanja na shule ys muhimbili vyote ni ardhi za familia ya Mzee Tambaza.
Jee huyajui makaburi ya kisutu?
Na pale makaburi mnayozikana kinondoni zote zile ni ardhi za waislam.

Mbona unazidi kuweka wazi ni jinsi gani ubongo ulivyojaa "jibini"?
Ni lini jina "Tanzania" au "watanzani" lilipatikana? Alafu rudi nyuma soma hoja zako ulizojikakamua kuandika uone kama vinawiana kimiaka.
Yani wewe kukalili wodi ya Sewa Haji ilijengwa mwaka gani unaona umemaliza kila kitu kuhusu Tanzania.?
Na hao waislamu unaosema waliwasaidia "watanzania" wao walikua RAIA wa wapi na walikua wanaitwaje?
Mbaya zaidi inaonekana waliwasidia watu wa Dar tu. Turudi shule mkuu, we leo hata ukibebeshwa pembe za ndovu sintohamaki.
 
Tanganyika ukenya uganda zanzibar zote zilipatiwa uhuru mmoja baada ya mwengine kuanzia 1961 . 1962 na 1963.
Zote uhuru ulipatiwa December.
Znz harakati za kugombea uhuru ziliwashirikisha wote ASP ZNP ZPPP na Umma party .
uchaguzi ulifanyika ma ZPPP na ZNP wakaunda serikali ya uhuru.
Zanzibar ikajiunga na UN mwaka huo huo ma pia ikawa mwanachama wa CWealth.
Then okelo akatumwa kufanya mapinduzi.
Uhuru wa Zanzibar ulipatikana 23 Dec. 1963

Unaona ulivyo FUTUHi sasa, we umedai Zanzibar ilikua huru hata kabla ya The Field Marshal J. Okello hajafanya mapinduzi, na kusema alitumwa kwenda kuwaua waislamu. Sasa hivyo vyama viliundwa kwa minajili ipi?
 
Uwongo mweupe. Mimi nilikuwepo tena wakati najitambua kabisa. Hizo kofia, Joho, Koti, Misuri, yalikuwa ni mavazi ya kawaida na wala hayakutafsiriwa kwamba mvaaji ni mtu wa dini fulani.

Na kofia zilikuwepo aina tofauti. Hapakuwa na kapelo wala alshababu. Zilikuwa zikiitwa vibandiko, na zingine zilizokuwa na hadhi kubwa, zilikuwa kama anayovaa Mh. Mkono. Kanzu nakoti juu, bila kusahau fimbo mkononi.

Dini zote walivaa kwa sababu zilikuwa bei rahisi, zilikuwa zikipatikana kwa wingi na lakini upande wa kofia wengine walivaa kwa kuficha nywele zisizochanwa.

Tuliishi bila kubaguana na tuliheshimiana na kuelewana. Kwa sababu hapakuwa na chuki, watu hawakuwahi hata kufikiria vazi fulani ni la dini fulani. Zilikuwa na mavazi yanayoitwa casual tu na fashion kama vile leo wanawake wengi mijini na vijijini wanavaa madela na mitandio kwa sababu ya upatikanaji wake kwa wingi, bei poa na inampa urahisi wa kufanya movements za aina tofauti tofauti.

NITAKTAA MPAKA KESHO UNAPOTAKA KUPOTOSHA KWAMBA ETI VIBANDIKO VILIASHIRIA UISILAM. HUO NI UWONGO!.

Safi sana mkuu ndo ajabu hyo pia watu walikua hawajui kuwa ilikua ikifika ramadhani huyo nyerere alikua anafunga pia.
 
Wewe Shori acha mambo ya kuhisi; mbona Dossa Azziz aliyekuwa umri mmoja na Ally sykes yumo kwenye hiyo picha?

Bulesi,
Baraza la Wazee wa TANU hakika lilikuwa kama jina lake linavyosema ni
baraza la wazee.

Dossa unamuona hapo na Nyerere sababu ni kuwa Dossa alikuwa na gari
na mara zote alikuwa na Nyerere katika safari na mizunguko hapo mjini.

Dossa aliweza kufanya haya yote kwa kuwa Dossa hakuajiriwa alikuwa na
biashara yake mwenyewe kwa hiyo alikuwa huru kushughulikia mambo ya
TANU mchana kutwa.

Ally Sykes alikuwa akifanya kazi Government Stores kwa hiyo nyakati za
mchana hakuweza kupatikana pale New Street Makao Makuu ya TANU
ilipokuwa ofisi ya Nyerere.

Katika utafiti wangu picha ambayo niliyoiona ya Ally Sykes na Nyerere ni
moja tu.

Picha hii ilipigwa nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata kabla ya uhuru.

Picha ya chini ni nyumba hiyo ndogo ni ofisi ya TANU baada ya kujengwa
upya kubadili ile ya asili iliyojengwa kati ya 1929 - 1933.

lgfs7bIjHJlJMGjt46f17asiPWNqqXjBtXN6F761Hu4i=w480-h360
 
upya kupisha ile ya asili iliyojengwa kati ya 1929 - 1933.

lgfs7bIjHJlJMGjt46f17asiPWNqqXjBtXN6F761Hu4i=w480-h360

Na hilo jumba refu linalojengwa (hii picha ya muda kidogo, sasa hivi limekwisha jengwa) ndiyo kwetu nilipozaliwa.

Mimi na TANU tuna historia ndefu sana, si wengi wanaoweza kutamba kuzaliwa hapo jirani na palipozaliwa TANU. Nyerere binafsi yake akija kununuwa sigara "karata" dukani kwetu halafu baadae akabadili akija mtu kumnunulia sigara SENATE.
 
Back
Top Bottom