upo sahihi kabisa,et kisa mwl amepga pics na hvyo vizee vilivyovaa bagharashia et navyo vimepigania uhuru
je km hzo samani jamaa alimuuzia mwl n wakat mwlm anakwend kuziona watu wakakusanyika hapo kw kuwa walijua mwl angeenda wakala mapics,leo hii et nao wapigania uhuru
# mohamed; utakufa kihoro km takadiri na kanxa yako ya udini
Tarangile,
Unaandika umekasirika na kutumia lugha zisizo za kiungwana.
Kuanzia leo asubuhi pamekuwa na hamu kubwa ya watu wengi kupitia
Majlis na kusoma.
Nimefahamishwa mmoja wa akina mama waliokuwa katika ile sherehe
ya
Mwalimu Nyerere kupokea samani kwa ajili ya ofisi yake ni marehemu
Bi. Khadija Said ni mama ya rafiki yangu
Bwana Athman Kassanda.
Bi. Khadija Said ni huyu wa pili kushoto:
Huyu mama kazikwa kiasi cha majuma matatu yaliyopita.
Nina hakika wengi watawatambua wazee wao katika hizi picha.
Haitakuwa vyema kama wewe utawatukania baba na mama zao.
Huijui historia ya
Ali Msham na watu wa nyumbani kwake katika harakati
za TANU.
Nitakufahamisha kwa ufupi.
Baada ya kufungua tawi la TANU 1954 hapo nyumbani kwake
Ali Msham
alitoa sehemu katika nyumba yake akaanzisha shule chini ya Tanganyika
African Parents Asociation (TAPA).
Hizi shule zilikuwa maarufu wakati wa kudai uhuru.
Baada ya kufungua shule hii alitoa sehemu ndogo ya nyumba yake akafungua
biashara ndogo ya mafuta ya taa na kumpa
Mama Maria Nyerere aendeshe.
Hizi zilikuwa nyakati ngumu sana kwa TANU na wazee wanazikumubuka sana.
Abdulrahman Msham anasema kaka yake binamu
Omari Likonda mtoto wa
shangazi yake
Biti Mwanaisha Msham dada yake
Ali Msham ndiye aliyekuwa
akimsindikiza
Mama Maria nyumbani jioni na kumbebea mzigo yake hadi nyumbani
kwake Magomeni Majumba Sita.
Omari Likonda yu hai na sasa ni mtu mzima.
Watu hawa si wa kutukanwa na kufanyiwa kebehi.
Hawa wanastahili heshima zote.
Watu hawa wameacha alama katika historia ya nchi yetu.
Huyo hapo chini ni
Abdulrahman Ali akiwa mbele ya nyumba ya baba yake Ali
Msham.
Hapo aliposimama ndipo lilipokuwa tawi la TANU wakati wa kupigani uhuru wa
Tanganyika.