Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Waislamu wengi wakat ule kuonekana ilitokana na harakati kubwa na nguvu kuwekwa dar(pwani) ambapo kulikuwa kuna idadi kubwa ya waislamu....
 
Hakuna ukweli ambao Wazanzibari HAWAPENDI kuusikia kama huu na sijui kwa nini inakuwa hivyo!
John Okello atabaki kuwa mtumuhimu sana wa kukumbuka katika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar milele na milele.

Kayoka,
Itapendenza kama utafungua uzi wa Okello.
Hakika ni mtu muhimu sana katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar.

Hapa ulipomleta si pake.
Hapa tunajadili historia ya TANU.
 
Huwezi kuiongelea "soksi" bila kugusia "kiatu". Mbona unakua kama "watoto wa mama Salma"

DSC03585.JPG

Kushoto Kwenda Kulia: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdul Sykes na Lawi Sijaona
Ukumbi wa Arnautoglo Kwenye dhifa ya Kumuaga Nyerere Kwenda UNO safari ya pili 1957

Hapo bado Nyerere anaweka sharubu kama za Hitler.

Nashukuru sana Mohamed Said hii inaonyesha jinsi Historia aidha kwa makusudi au kwa kudharau inapofifishwa.
 
DSC03585.JPG

Kushoto Kwenda Kulia: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdul Sykes na Lawi Sijaona
Ukumbi wa Arnautoglo Kwenye dhifa ya Kumuaga Nyerere Kwenda UNO safari ya pili 1957

Hapo bado Nyerere anaweka sharubu kama za Hitler.

Na ndio kipindi pekee katika maisha yake alipata kuvaa "kibepari" kabla ya kuanza kuvaa "kijamaa"
 
Mimi nikiiangalia picha hizi nakumbuka tu kazi ya kwanza aliyoifanya Mwalimu baada ya uhuru kupitia iliyoitwa "operation makuti" katika kubadilisha mazingira ya mji wa Dar es Salaam. Hizo mnazoziona ndizo nyumba za wakati huo mjini Dar es Salaam toka Kariakoo, Ilala hadi Magomeni na ndio maana hata kuna sehemu ilijulikana kama Magomeni Makuti...nyumba hizo za makuti ndizo zilitamalaki.

9429573.jpg

Nakumbuka mtaa maarufu wa Idrissa Magomeni ulivyoweza kuwa na nyumba za kisasa (kwa wakati huo), barabara za lami zenye mitaro ya kisasa kupitisha maji machafu. Magomeni Makuti, Magomeni Mikumi, Magomeni Kota zote ziliweza kuunganishwa kwa barabara za lami zikipita mabasi ya DMT (Dar es Salam Motor Transport) hadi Mikumi mwisho. Sehemu kama za Gerezani zilikaliwa na walowezi wengi wakiwa Manyema, Wanubi na Wazulu.

Kwa nini hizo barabara zilizojengwa kitaalamu hazikuweza kudumu ni mjadala mzito unaohitaji mada yake peke yake. Hivyo hivyo baadaye nyumba za starehe za kisasa chini ya DDC zilizokuja kujengwa baadaye Karikaoo. Magomeni hadi Ilala na kuwekewa "fittings" za Kisasa (wakati huo) nazo hazikudumu kwa sababu ambazo hasa zilihusiana na utamaduni wa wakazi wa hizo sehemu...hawakujua matumizi rasmi ya vifaa vya kisasa vilivyowekwa.

L - R: Sheikh Suleiman Takadir aka Makarios, John Rupia, Julius Nyerere na Bantu Group 1955

Butiama kulikuwa kuna nyumba zipi? tunaomba tuoneshe.
 
Mohamed said tafadhari uwe unalipia haya matangazo ya vitabu vyako hapa jf au kama vipi anzisha forum yako ujitangaze zaidi na zaidi.

Massa,
Siwezi kulipa hisani ambayo JF wamenifanyia mimi.
Nani akinijua kabla sijaandika JF?

Hakika sina cha kuilipa JF.
Hata kama nitaanzisha jukwaa langu halitaweza hata kwa mbali kuifikia JF.
 
Unalinganisha Dar es Salaam na Butiama? Mwishowe utalinganisha Kigoma na Dubai!

Kumbe hapalingani eeh? sasa endelea na raha za historia ya TANU, kama unazo picha za babu zako wakiwa katika harakati za Uhuru unaweza kutuwekea pia.

MSHUME+KIYATE.jpg
 
Sawa.
Ila sipo kushindana na Moh Said kama vile ni ligi, eti yeye abandike picha na mimi niweke.
Nimetoa tu kama 'possible explanation for certain observation'
I may be right, I may be wrong. And I am more interested in reading rather than digging for photos from sources I don't have...
I hope "umenisoma"

Nakujibu hivi: You re totally wrong!
 
Mimi nikiiangalia picha hizi nakumbuka tu kazi ya kwanza aliyoifanya Mwalimu baada ya uhuru kupitia iliyoitwa "operation makuti" katika kubadilisha mazingira ya mji wa Dar es Salaam. Hizo mnazoziona ndizo nyumba za wakati huo mjini Dar es Salaam toka Kariakoo, Ilala hadi Magomeni na ndio maana hata kuna sehemu ilijulikana kama Magomeni Makuti...nyumba hizo za makuti ndizo zilitamalaki.

9429573.jpg

Nakumbuka mtaa maarufu wa Idrissa Magomeni ulivyoweza kuwa na nyumba za kisasa (kwa wakati huo), barabara za lami zenye mitaro ya kisasa kupitisha maji machafu. Magomeni Makuti, Magomeni Mikumi, Magomeni Kota zote ziliweza kuunganishwa kwa barabara za lami zikipita mabasi ya DMT (Dar es Salam Motor Transport) hadi Mikumi mwisho. Sehemu kama za Gerezani zilikaliwa na walowezi wengi wakiwa Manyema, Wanubi na Wazulu.

Kwa nini hizo barabara zilizojengwa kitaalamu hazikuweza kudumu ni mjadala mzito unaohitaji mada yake peke yake. Hivyo hivyo baadaye nyumba za starehe za kisasa chini ya DDC zilizokuja kujengwa baadaye Karikaoo. Magomeni hadi Ilala na kuwekewa "fittings" za Kisasa (wakati huo) nazo hazikudumu kwa sababu ambazo hasa zilihusiana na utamaduni wa wakazi wa hizo sehemu...hawakujua matumizi rasmi ya vifaa vya kisasa vilivyowekwa.

Mag3,
Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa mtaa ambao Ali Msham alifungua tawi
la TANU 1954 kama ulivyo hivi sasa.

DSCN1811.JPG
 
Safi sana mkuu ndo ajabu hyo pia watu walikua hawajui kuwa ilikua ikifika ramadhani huyo nyerere alikua anafunga pia.

Kufunga ni tunu kubwa kwa dini yoyote...Naamini asingeweza kupata support ya watu kama asingejitahidi kuwa miongoni mwao. Nyerere hata hivyo hakuachia hapo kufunga. Alikuwa ni mtu anayefunga mara kwa mara hasa inapotokea kipindi cha majaribu au wakati mgumu wa uongozi wake.

Kama tunafahamu hilo, tufunge na kuzidi kuomba dua tuendelee kuwa wamoja na tujenge Taifa lenye mustakabali wa watanzania walio wote. Dini zetu zisiwe ndio chanzo cha kutufarakanisha.
 
The man himself Okello, J
 
Attachments

  • 1430677327503.jpg
    1430677327503.jpg
    24.6 KB · Views: 231
A man himself aliyesababisha mpaka leo Visiwa vya Zanzibar vinapumua na kusaza. A father of Zanzibar Island.
 
Attachments

  • 1430677520414.jpg
    1430677520414.jpg
    39 KB · Views: 225
WAZEE+WA+TANU.jpg

Waliokuwa Katika Picha Hii na Ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU
(Wengine: Hawapo)

  1. [*=left]Abdallah Shomari (Tandamti No. 3)
    [*=left]Nassoro Kalumbanya (Simba)
    [*=left]Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo)
    [*=left]Mtoro Ally (Muhonda)
    [*=left]John Rupia (Misheni Kota)
    [*=left]Julius Nyerere (Pugu Sekondari)
    [*=left]Said Chaurembo (Congo/Mkunguni)
    [*=left]Jumbe Tambaza (Upanga)
    [*=left]Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
    [*=left]Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande)
    [*=left]Mshume Kiyate (Tandamti)
    [*=left]Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo)
    [*=left]Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
    [*=left]Rajab Simba (Kiungani)
    [*=left]Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala)
    [*=left]Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
    [*=left]Makisi Mbwana (Aggrey/Congo)
    [*=left]Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
    [*=left]Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo).

Waislam ndio waliopigania uhuru wa hii nchi, ilo linajulikana sana sema yule alipewa bendela aipeperushe ndiye aliyeleta figisufigisu mpaka mfumo kristo ukachukua nafasi kutoka kwa maelekezo ya mkoloni muingereza.
 
Back
Top Bottom