Kumbe ndio maana Zitto alikuwa anampigia debe Membe, hata kama hajajiunga rasmi, lakini hizi ni dalili atajiunga.
Endapo patakuwa na muungano kati ya Chadema na ACT, ni vyema umakini wa hali ya juu uwepo kwenye kumsimamisha mgombea Urais, hasa upande wa Tanzania Bara.
Yaliyotokea 2015 yanatosha, hakuna haja ya kudanganyika tena na wahamiaji, ni wakati sasa wa upinzani kumsimamisha mgombea wao, watu wenye sifa wapo.