Picha: Camera ya simu ipi inaweza kupiga picha bora zaidi kama hizi?

Simu yenye Camera nzuri sana ninayo faham ni Samsung Galaxy S23 Ultra sport; kamera yaKe ni kali kuliko Iphone 14. Picha kama hiyo inaweza kuwa imepigwa kwa simu kuanzia Samsung Galaxy S21 Ultra au hata Iphone 12 promax na kuendelea juu. Bei zake watakujuza wengine.

Naona hapo kwa Picha inaonekana kasha la S10? inaweza kuwa ndiyo camera aliyopigia. Picha pia hutegemea sana Mwanga na kizuizi cha mwanga (back ground) hivyo yaweza kuwa pia ni Camera ya kawaida kama hiyo S10
 
Kwani yeye kapiga na kamera ipi!??
 
Nimejaribu kuifuatilia hiyo s23, nimeshtuka sana baada ya kukuta inauzwa Tsh 2.3m. Mkuu hakuna simu ya bei chee inayopiga picha kama hiyo?
 
Hapo lazima ujipange, hizi simu zetu za laki 3 haziwezi kutoa picha kama hizo
Dah! Na kweli mkuu. Kwani hakuna yenye walau uhafadhari hata tu ya kurekodia vipindi? Walau yenye kuanzia 50MP, ya kimaskini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…