Picha: Ephrahim Kibonde wa Clouds FM atiwa nguvuni

Picha: Ephrahim Kibonde wa Clouds FM atiwa nguvuni

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Shame on u Kibonde sikutegemea unaweza kufanya vitu kama ulivyofanya leo pale ubungo asbh uuuuh ivi nn maana ya public figure ya Tz hii mnatuonyesha nn duh Polen clouds maana jamaa kachemsha.


attachment.php


UPDATES:

Kibonde wa Clouds anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, amemgonga dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walipofika kupima ajali, Kibonde karudi nyuma kaendesha gari lake kasepa! Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia.

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge. Trafiki aliingia ktk gari lake nakumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde kagoma na kumtaka trafiki ashuke ktk gari lake, trafiki naye kagoma kushuka. Mchezo ulioendelea Kibonde aliondoa gari na kuanza kupiga misele, akizunguka mitaa akiwa na trafiki huyo! Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kila kiunga cha jiji hususani eneo la Mwenge na Ubungo. Hayawi, hayawi yakawa, Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo nikashuhudia senema ya Kibonde na trafiki! Trafiki wa kike aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde iliyokuwa kasi, gari hiyo haikuonesha dalili za kupunguza mwendo.

Trafiki alikomaa kusimama mkono wake ukiwa juu kuashiria kumtaka Kibonde asimame huku akipaza sauti ktk radio call akisema ananigonga, afande, ananigonga! Akiwa ktk hali hiyo, kuna gari ilikotokea sikujua ikakatisha kati ya trafiki na gari ya Kibonde ndiyo ikawa kigingi cha gari ya Kibonde na kutiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki ambapo kwa sasa amepelekwa Oystabay! Kwa utafiti wangu kidogo nilioufanya nikifukuzana na muda kuwahi kanisani, ni kwamba Kibonde na watu wengine aliokuwanao ndani ya gari lake walikuwa 'TINGASI'!




 

Attachments

  • kibonde na traffic.jpg
    kibonde na traffic.jpg
    77 KB · Views: 8,115
Mshenzi huyo. Na akawekwe rockup/lokapu asiishie counter tu kutoa maelezo kisha aachiwe..
 
Hangover hiyo...chezea long wikend
 
Alivunja sheria za barabarani nini?

Mleta mada weka picha zaidi na habari kamilifu tafadhali
 
kagonga gari ya mzungu mmoja ilikuwa mbele yake, Mzungu kashuka garini traffick wakaja na kibonde kashuka eti anaanza kumletea kibesi mzungu kwakuona sijui yule mgeni nchi hii akaanza kumsukuma mzungu mwenyewe mrefu kibonde anaonekana kama mbilikimo kwake
trafick wanamzuia akaanza kuwafanyia fujo uuuuh yn kasombwa tanganyika jeki kapelekwa kituoni
 
Achaa ujingaaa wewe...Uyo sio Kibondeee....mbonaa jamaaa...Ndio anatokaaa Home mda huu...
 
kagonga gari ya mzungu mmoja ilikuwa mbele yake, mzungu kashuka garini traffick wakaja na kibonde kashuka eti anaanza kumletea kibesi mzungu kwakuona sijui yule mgeni nchi hii akaanza kumsukuma mzungu mwenyewe mrefu kibonde anaonekana kama mbilikimo kwake
trafick wanamzuia akaanza kuwafanyia fujo uuuuh yn kasombwa tanganyika jeki kapelekwa kituoni

we mwenyew zero kweli, sasa kwanin hukutoa habari yote,,
 
Back
Top Bottom