Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika kuna kusudi maalumu la Mungu kumuinua Rais Samia na kumketisha kitini. Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe kumpa kibali Rais wetu kuwa Rais wa Taifa letu. Ni Chaguo la Mungu Mwenyewe kwa Rais Samia kuwa Mtumishi wetu Watanzania.
Nimeshuhudia mara nyingi sana kwa Macho yangu watu au mtu au kikundi kikipata tabasamu katikati ya majonzi au huzuni baada ya kumuona au kukutana uso kwa uso au ana kwa ana na uso wa Rais wetu Mpendwa na kipenzi cha watanzania.
Rais Samia ni kiongozi ambaye akijitokeza sehemu na kuwepo Sehemu au eneo fulani la watu. Unaona watu wakitabasamu ,nyuso zao zikijaa furaha na bashasha na uso wa matumaini. Ni kiongozi ambaye uwepo wake unaleta furaha na mtu kujisikia amani ya moyo na utulivu . Mtu anajiona mwepesi na kupungua kwa Mawazo.
Ndio sababu unaona hata akipita katika wodi za wagonjwa au kutembelea majeraha sehemu fulani hospitalini unaona namna wagonjwa wanavyopata kutabasamu na kujawa na furaha katika nyuso zao. Watu wanajihisi kupona na kila mmoja kutamani kupata bahati ya kupewa mkono wa pole wa Rais wetu Mpendwa.
Leo hii kwa mara nyingine tena Familia ya Mheshimiwa Jobu Ndugai ambaye ametangulia mbele za haki imejikuta ikitabasamu baada ya kufikiwa na mkono wa pole wa Rais wetu Mpendwa.imetabasamu katikati ya majonzi ,huzuni na maumivu ya kumpoteza mpendwa wao. Lakini imejisikia wepesi na kupata faraja kubwa sana baada ya kumuona na kukutana ana kwa ana na Rais wetu.
Hii ndio Maana halisi ya Mfariji wa Taifa na kiongozi anayependwa na kukubalika na watu. Ndio Maana ya uongozi na kiongozi wa watu,ndio Maana ya utumishi na mtumishi wa watu. Ndio maana halisi ya cheo kuwa kwa ajili ya kuwapa watu matumaini. Ndio maana halisi ya kiongozi kusimama na watu nyakati ngumu na za huzuni na majonzi kuwapa faraja , matumaini na kuwatia moyo.
Kwa hakika Taifa limepata na kubahatika Kuwa na kiongozi mwenye moyo wa upendo, huruma, unyenyekevu na mwenye kujali Watu. Wengine unakuta hana habari na matatizo au shida za watu. Mwingine unakuta anajifanya utafikiri haoni matatizo ya watu. anajifanya yupo Bize muda wote na hawezi kujumuika na watu na kuwapa faraja au kuwafariji.
Kwa hakika watanzania tunapaswa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutupatia zawadi hii ya kuwa na Rais Samia kitini. Watu na viongozi aina ya Rais Samia hawazaliwi kila siku na hawapatikani kila mahali. Ni nadra sana kuwapata na kuwa nao. hivyo watanzania hatuna budi kumlinda Rais wetu kwa maombi na kwa gharama yoyote ile iwayo.