PICHA: Hii ndio maana halisi ya mfariji wa Taifa. Rais Samia Abarikiwe sana

Lucas, hoja yako ya kumuita mfariji wa Taifa haiwezi kufunika ukweli mchungu kwamba kuna Watanzania kama Mzee Kibao waliouawa kikatili, wengine wamepotea bila kupatikana hadi leo, na hakuna hatua za maana zilizochukuliwa chini ya uongozi wa huyu unayemsifia.
Faraja siyo tabasamu la dakika chache kwenye kamera, bali ni kuhakikisha haki, ulinzi wa maisha, na hatua thabiti dhidi ya maovu yanayowakuta wananchi.
Watanzania hawana upungufu wa kumbukumbu kiasi cha kumeza sifa zisizoakisi hali halisi. Uongozi bora si maigizo ya kutembelea wagonjwa pekee, bali ni uwajibikaji wa kweli kwa changamoto na majeraha ya taifa.
 
Kunywa sumu UFE tu maana huna faida yoyote ile hapa Duniani na hata Mbinguni
Mazee unasikitika kwa kifo na wakati huo huo unataka mtu mwingine afe hii sio sawa mtu wa Songwe ingawaje mligawanywa na wahuni ili waibe mapato ya Tunduma kirahisi wewe ni ndugu yangu still..
 
Rais Samia ni muwajibikaji na anayejali haki sana katika kuongoza kwake serikali yetu.
 
Unafiq wa hali ya juu kabisa, embu rejea hotuba ya bi Tozo dhidi ya hayati kuhusu kukopa kopa kwa hovyo aliyosemea hayati 'Kongwa'.
 
Mkuu umesahau kwa wengi, kifo ni kifo tu!!!
 
Kunywa sumu UFE tu maana huna faida yoyote ile hapa Duniani na hata Mbinguni
Mimi nimekunywa damu ya Yesu Kristo, niko hai ndani yake sasa na hata milele...

Nakushauri na wewe inywe utakuwa hai...

Nawashauri na hao bwana zako na bibi zako mnywe maana hamtakufa, mtakuwa hai hakika...
 
Mkuu, naona unaanza kutuangusha sasa. Hapo kwenye msiba na faraja ndipo tulitegemea kuona machozi yakibubujika kama maji sasa. Lakini wapi, umekausha tu !🤣
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…