PICHA: Hili jengo linalojengwa Kariakoo kwa PPP ni balaa ni zaidi ya Mlimani City unaambiwa Serikali itajizolea zaidi ya TZS 2.5bn kila mwaka

Huwezi ukafanya project hio kariakoo, Hasa katikati ya kariakoo, ili ufike hapo na Gari lazima uwaombe machinga si chini ya 20 watoe vitu vyao Barabarani ili upite, project gani ya kimataifa unafanya eneo hilo?

Na logic ya majengo ya NHC kkoo ni ya kizamani.

Unakuta Jengo halina basement, ground floor kuna frame 4 tu na juu wanaishi watu wanne, jengo katikati ya kkoo wapangaji 8 tu, juu nyumba wanalipa 200,000-350,000 kwa mwezi, chini Frame 800,000-1,200,000, just imagine chini ya milioni 10 kwa mwezi ghorofa zima katikati ya jiji.

Wawekezaji wanaopewa wanaanza kutoa frame basement, ground floor na 1st floor, kuanzia 2nd floor kuendelea unakuta hata ghorofa 10 ni stoo. So pato la NHC kwa sasa litaongezeka si chini ya Asilimia 100 na baada ya miaka 30 wakikabidhiwa jengo pato linaweza ongezeka hadi asilimia 1000 ama zaidi
 
Kwani Freme pale Kariakoo ni kiasi gani?
Ukigawa hio 2.5B kwa 12; na ukagawa kwa vyumba vitakavyokuwepo (tena hii ni gorofa) sio viwili wala vitatu utaona per unit pesa inayoweza kupatikana ni kubwa kuliko 2.5B ukizingatia kitu cha gharama zaidi hapo Kariakoo ni ardhi ambayo ni mali ya UMMA.... (Prime Area)

Thus inategemea kama dhima ni kutoa huduma kwa wabangaizaji wapate sehemu za kufanya kazi (huenda rent bado itakuwa kubwa sababu serikali atachukua chake na mfanya biashara atachukua chake ili apate faida) kama dhima ni serikali kuchukua as much as possible hio sio pesa kubwa kwa mwaka kwa Kariakoo kwa multi shops ambazo nyingine huenda Government imeshachukua au pameshajaa wahitaji...

Thus narudia tena kama dhima ni kusaidia wabangaizaji hivi kina Machinga Complex waliishia wapi ?
 
Hayo matatizo mbona madogo sana kutatua, watu wamejenga treni za chini ya ardhi, wamebomoa majumba, itakuwa kuondoa machinga mtaani tu?

Tatizo watu hawana imagination na nia.

Ukiwa na imagination na nia hayo mengine yote yanafanyika.
 
Kariakoo panafaa pawe Makumbusho ya Taifa 😂
 

Tunapigiwa hapo kwenye “Mda wa Mkataba”
 
Kama jengo litajengwa mtindo wa magorofa hakuna mpangaji atakayeingia humo kupanga. Chukueni somo kutoka Machinga complex imebaki mahame.

DDC mtaa wa muhonda, narung’ombe, congo, msimbazi demand ipo sana, frame zitalipa hela ya maana tu floor 4 kutoka underground, ground, first, second and third floor (pakikaa fresh) ni uhakika zitapata rent nzuri , huko juu ni ma store au office space tu.

Kwa mitaa ile demand sina mashaka nayo.
 
Mkuu on other aspects nakuelewa sana,

Turudi kwenye frame za Kariakoo na PPP ya Kafulila ....

Bogus project to ever happen..... dont get twisted...

Suala la Serikal kujenga frame na masoko ni so irrelevant kwa uchumi wetu kwa sasa .

Lile eneo wangekodisha tu na serikal ikapata fedha kuliko hizo blabla za PPP na ujanja ujanja...

Kariakoo frame zinazouzika ni za chini tena zinazotazama lami, hizo nyingine ni za kufugia kuku..

Hizo ghorofa sijui whatever labda Godowns na Apartment...
Sasa hizo blabla ni za kuita hadi bunge kwel😂
 
Ardhi mnayo kubwa sana kwanini mjenge magorofa kwa ajili ya biashara?

Kwa kweli nipande gorofa ya 10 kisa naenda kununua mfuko wa pipi? Au shuka?

Grand Bazaar market ya Istanbul ilijengwa miaka 500 iliyopita na ndio soko kubwa duniani mpaka leo
Lina ukubwa wa 30,700 Sq meters na lina maduka 4000
Lipo ndani ya mitaa 60
Na lote halina gorofa
Soko kuwa chini ni bora zaidi au lisizidi gorofa 3 tu
Uende Istanbul na hujaliona hilo soko basi rudi tena

Ila ndio maamuzi yetu sasa tufanyeje?
 
Ulichosahau hapa ni hela ya mwekezaji, nimesahau figure ila ni around 25% serikali na 75% mwekezaji kwa miaka 30 ya mwanzo then baada ya hapo jengo linarudi Serikalini, kwa mahesabu yako ya Milioni 900 ni roughly 2.7B kwa Serikali kwa mwaka.

Na Jengo likiwa na wapangaji 900 sio wote wana frame kuna vigoli vya mpesa na biashara Ndogo ndogo pia hivyo kama 200,000 wanakodisha.
 
Again,

Tatizo wewe unaongelea uchumi wetu wa sasa na Kariakoo ilivyo leo.

Mimi naongelea kinachoweza kufanyika.

Hatuwezi kuelewana.

Wewe uko stuck tulipo leo.

Mimi naona potential ya kinachowezekana kufanyika.

Tupo sehemu mbili tofauti kabisa.
 
Kundunduliza ni misemo ya kimaskini.
 
Dar es salaam imejaa sana kwa sababu watu wamejenga vibanda vya chinichini mji mzima. Sasa ni wakati wa kujenga juu.

Pia, kujenga kwenda juu kunapunguza safari ndefu, badala ya kwenda maduka kumi sehemu tofauti unapata kila kitu sehemu moja.
 
Again,

Tatizo wewe unaongelea uchumi wetu wa sasa na Kariakoo ilivyo leo.

Mimi naonhelea kinachoweza kufanyika.

Hatuwezi kuelewana.

Wewe uko stuck tulipo leo.

Mimi naona potential ya kinachowezekana kufanyika.

Tupo sehemu mbili tofauti kabisa.
Mkuu serikal haina uwezo, narudia haina uwezo wa kuifanya Kariakoo tofauti na ilivyo leo...

Serikal zote duniani ni incompetent kwenye kufanya aina ya biashara zinazofanyika Kariakoo...

Anachofanya Kafulila ni worst case scenario.. anamilikisha mali za umma watu binafsi kwa excuse ya PPP..

Not now, not in future.. .there is no Proper and best Kariakoo than it is right now..... Hiyo Kariakoo mpya ina exist kichwani tu
 
Wala siongelei serikali hii, naongelea what is possible.

Kwa nini point hii ndogo inakuwa ngumu sana kwako kuelewa?

Naona ushajivika utabiri wa all futures kumshinda Sheikh Yahya Hussein.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…