baba-mwajuma
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 4,178
- 7,591
Huwezi ukafanya project hio kariakoo, Hasa katikati ya kariakoo, ili ufike hapo na Gari lazima uwaombe machinga si chini ya 20 watoe vitu vyao Barabarani ili upite, project gani ya kimataifa unafanya eneo hilo?Point nzima ya kuweka watu kama Kafulila na PPP ni kuongeza value, sasa unawekaje project kisomi halafu biashara iendelee kienjeji enyeji tu?
Weka wawekezaji wa kimataifa hapo, weka international mall, weka rents za kubadilisha eneo zima livutie biashara za kimataifa tuondokane kwenye umachinga.
Tatizo hatuna watu daring wenye vision ya kuona kinachoweza kuwa, tuko stuck kuangalia kilichokuwa.
Classic problem of induction scenario.
Na logic ya majengo ya NHC kkoo ni ya kizamani.
Unakuta Jengo halina basement, ground floor kuna frame 4 tu na juu wanaishi watu wanne, jengo katikati ya kkoo wapangaji 8 tu, juu nyumba wanalipa 200,000-350,000 kwa mwezi, chini Frame 800,000-1,200,000, just imagine chini ya milioni 10 kwa mwezi ghorofa zima katikati ya jiji.
Wawekezaji wanaopewa wanaanza kutoa frame basement, ground floor na 1st floor, kuanzia 2nd floor kuendelea unakuta hata ghorofa 10 ni stoo. So pato la NHC kwa sasa litaongezeka si chini ya Asilimia 100 na baada ya miaka 30 wakikabidhiwa jengo pato linaweza ongezeka hadi asilimia 1000 ama zaidi