Picha: Hivi ndivyo tunaweza kwenda sayari ya Mars na kurudi Earth

Picha: Hivi ndivyo tunaweza kwenda sayari ya Mars na kurudi Earth

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,560
Habari,

Ni muda sasa utafiti kuhusu sayari ya Mars umekuwa ukiendelea, na mapitio juu ya utafiti huu unaonyesha Mars ni sehemu ambayo hamna wenyewe.

Hii inaonyesha wazi endapo wanadamu tukizichanga karata zetu vizuri basi tunaweza kuanzisha makazi.

Kupitia makubaliano mbalimbali tayari nia imewekwa kufikia 2024 wanadamu tuwe tumetia timu katika sayari hii nyekundu.

Hivyo tuanze kuifanya kuwa ya kijani kwa maendeleo endelevu ya viumbe hai na ifikapo 2050 tuwe na Mataifa mawili.

Kutokana na mikakati na maazimio mbalimbali kufikia 2022 tuwe tayari tumeanza ujenzi huko kwa teknolojia adhimu ya 3D Printing!

Basi mimi leo nakuja kwenu na mawazo yafuatayo;-

isajorsergiostudios Mars Way.png

Kupitia picha hii niliyotengeneza utaweza kuona Earth, Moon na Mars pia International Space Station 1&2 pia satellite inayozunguka mwezi.

Naona tuufanye Mwezi kuwa kituo, makutano au hub ya kurahisisha kufika Mars.

Wanasayansi watokapo katika dunia kwanza wafike ISS na hapo waufikie Mwezi kisha waandae mazingira ya vifaa kutoka dunia kufika katika Mwezi.

Hivyo baada ya mpango mkakati wa Mars wanasayansi waunde kituo kipya cha ISS2 baina ya Mwezi na Mars kurahisisha michakato kama ilivyo ISS na Dunia.

Hii itarahisisha vifaa na malighafi zinazotoka katika Dunia kwenda Mars kuwa na Uhakika.

Same itarahisisha usafiri baina ya Wanadamu wa Mars na Dunia, itakuwa unatoka Earth unafikia Moon kwa ajiri ya usalama kisha Mars. Huku ISS ikitizama anga baina ya Earth na Moon pia ISS2 ikitizama anga baina ya Moon na Mars.

Hivyo kutokea Moon tutaweza kurusha Satellite ya ku-operate Moon bila shaka yoyote.

Kufikia 2030 tunaweza kufanya go and return yaani unatoka Earth unapitia Moon katika mapumziko kisha unafika Mars same kwa Mars to Earth. Unaweza kutoka 2 years Earth ukafanya shughuli zako Mars Kisha kurudi Earth after preferably kila 2 years.

Baba Mars, Mama Moon huku Watoto Earth.
Picha kwa hisani ya: isajorsergio Space zikiwa zimetengenezwa isajorsergio Studios.

- Sergi 🐰
 
Tatizo ni umbali wa kusafiri ndiyo italeta shida, maana unakaa mpaka ndevu zinaota na kuwasha ili uende saloon kunyoa.
 
Tatizo ni umbali wa kusafiri ndiyo italeta shida, maana unakaa mpaka ndevu zinaota na kuwasha ili uende saloon kunyoa.
I think ni umbali wa kawaida. Pia hii ni transformation mpya ambayo hata wanadamu tuseme watakuwa wapya.
 
Subiri kwanza elon musk amalize mipango yake ya hiyo safari,halafu ndio uje na udaku wako Wa kuahirisha kutuma radio signal kwa sababu ya kifo cha qasim solaiman!!!!
 
2012 walisema 2020 tunaingia mars...NASA wakawa wanatafuta volunteers... Elon musk nae alisema 2022
Tajiri wa urusi alijitolea
Leo hii unatuambia 2024

Looks like it won't happen in our lifetime
Believe! 2020 maandalizi yamekwisha anza, hivi sasa utengenezwaji wa vifaa upo unaendelea. Kikubwa hata Scientist Suits za kwenda Mars naona zimeboreshwa na mpya kabisa.

Ujue katika planet zonal tunatazimia 2022 tutume cargo zenye tons kadhaa maana Earth na Mars zitakuwa zimekaribiana mihimili... Same itatokea tena 2024 na hapo tutatuma a lot of tons cargo+baadhi ya watu hapo sasa tutaanza kuijenga Mars kiteknolojia hasa 3D Printing!

Tayari tenda zilitangazwa na kampuni mbili zilishinda tenda ya utafiti na ujenzi ulio sustainable.

Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kuchukua tenda 😢
 
Kwenda Mars nadhani tunahitaji kwenda tu, hatuhitaji kupeleka chochote, Technologia ipo tunahitaji brain tu kule, kwanini tubebane na mizigo kwenda huko? Nitakubali iwe hivyo kwa trip za mwanzo na waende wachache watakaokuwa na kazi za kufanya, kisha ndio sisi wajaza vyoo twende.

Twende moja kwa moja tu hakuna kupitia mwezini wala nini, Mwezini nako kuwe na makazi yake aendaye kule awe amefika.

Kuwe na kwenda tu hakuna kurudi, watakao kwenda waka ijaze Mars, na wakiweza ku develop technologia ya kurudi kutujulisha au kutufahamisha yanayojili huko sawa, lakini kusiwe na hitaji la kurudi duniani. Mwenye ndugu aende nao kama haiwezekani kwenda nao basi ama aende au asiende kabisa.
 
Lazima twende na cargo! Ninaposema cargo ni vifaa na machines kama za ujenzi wa 3D ambazo kwa sasa zinaundwa na kuzidi kuboreshwa kwa wingi na ndugu zangu AI Space Factory na ndio zitawezesha ujenzi wa haraka, akinifu na ubunifu wa TERRA.

Pia Rovers mbalimbali zitahitajika kwa uchunguzi zaidi na usaidizi tuwapo kule, alkadharika vifaa na mitambo yakuweza kupambana na radiation au yakutumiwa tuwapo Mars ni muhimu.

Kumbuka Mars hakutokuwapo mipaka (Nchi, Mataifa) kama Earth kwa mujibu wa mikataba na maridhiano ya Russia, UK, US na China.
 
Kubebana na mizigo ni dalili za uoga, twende tuanze kijima kama tulivyoanza duniani bila magari wala ndege, bila hospitali wa maabara za uchunguzi, bila dawa na wala mashule na technologia za duniani.

Mazingira ya kule ni tofauti, hivyo tuyakabili na tutajifunza upya huko huko tukifika. Ukianza kubeba mizigo itakuwa unahamisha kila kitu, wapo tutakao taka twende na ugali huko. Akili zinakuja unapopata shida, na mazingira yatakuwa na nyenzo za utatuzi tu.

Babu zetu walianza kula nyama mbichi baadaye walianika juani na wapo walio vundika na kuikamua, leo tuna mioto tuna choma, tunachemsha, tuna hoka kwenye mi oven, hadi microwaves.

Leo hii waafrika waliogundua moto hawawezi kuwasha moto bila viberiti vya njiti au gesi, huwa naona documentary wazungu wana pikicha vijiti na mioto inawka lakini leo hata mmasai na mdigo au barbaegi wana viberiti, na kikikosekana hakuna kula.

Nilikotoka mimi tulikuwa tuna washa moto mavi ya ng'ome tunafukia kesho tunaukuta na mtondogoo , lakini leo hata mifugo hatuna.

Kama tumeamua kwenda kule twende tukapambane na mazingira ya kule, unaweza kubeba viberiti halafu hewa ikawa hairuhusu kuwasha mioto hii ya huku duniani.

Twende mikono mitupu tukapamambane na hali ya hewa namzingira ya huko tutaelewa tu cargo za kujengea tutatengeneza huko huko, hatutaki kuanza kuwa wategemezi wa Dunia tena.

Assume Mungu ndiye angekuwa ametuamuru tuondoke duniani kwake na twende huko Mars na asiruhusu tubebe chochote, kama Alivyo mtimua Adam na demu wake Eve, akasema tokeni hapa na mtakula kwa jasho na kuzaa kwa uchungu, tizama leo Adam na Eve wana maghorofa, Magari, Nguo za kumwaga na hadi mabling bling.

Tusiwe waoga, twende kifala nasi tuka prove hayo ma AI kama na huko yanaweza kufanya kazi.

Hakuna kubeba ugali wala pilau, maji wala soda. Labda BEER tu.

Lakini nduguzetu ukiruhusu kubeba, wataleta hadi senene Mars.
 
Mr. Nanye Go nisome kwa umakini,

Mars Cargo Jets zitaondoka na zana wezeshi ambazo tumefanya tafiti na kuona ndizo zinazofaa kwa Mars. Mfano wa zana hizo ni teknolojia adhimu ya 3D Printing ambayo itawezesha kujenga majengo lengwa kwa muda stahiki na ubora pia.

Hivyo ni lazima machines hizi zilizotengenezwa kwa ajiri ya Mars zibebwe hadi Mars kuanza shughuli.

Ikumbukwe nia kubwa ni kuweza kupambana na radiation at first ambayo inaonekana ndio kikwazo kikubwa.

Pia kutahitajika Solar Circles Cercs za kutupatia nishati. Hapo tutaweza kuanza kuyatafiti maji na ustawi wa mimea.

Kupitia Cargo chakula ni muhimu maana hadi leo sijawahi kuona Mwadamu asiyekula.
 
And probably Adam na Eve/Hawa/Mishil walikuta mahitaji muhimu. Maji, Matunda na mboga,

Miale na mionzi yenye kipimo, hali ya hewa wezeshi and alike kazi yao ikawa kurandaranda tu.
 
Back
Top Bottom