Picha: Hivi ndivyo tunaweza kwenda sayari ya Mars na kurudi Earth

Mkuu haya mawazo wazungu wanayo toka miaka ya 90 huko pitia
 
Mars Ina thin atmosphere sio kwamba haina kabisa hivyo juhudi zikifanyika Kuna uwezekano wa kuliongeza na kutandaza hewa ya oxygen kitu hiki kitachukua gharama sana na muda mrefu,ikiwezekana hivyo tu Basi mars patakuwa sehemu ya kuishi.
Iko hivi hili mmea uote ustwa vizuri unahitaji hewa ya carbon dioxide na ikiwa atmosphere yakule ni tiny huoni itakuwa gharama kubwa kutengeneza hewa ya oxygen kupotia mmea huo kulingana na uhitaji wa viumbe jee ni hesabu gani walio piga ya kuweza kutengeneza hewa ya oxygen hiweze kufikia at least 30% na izalishwe carbon dioxide iweze kufika 60% je wataizalosha na nini maana ili ipatikane inahitajika vitu Kama burning material na decaded sijui ndio mwili ulio oza na gas zingine kuchangia
 
Kwanza bado mwanadamu hajatia guu lake! Akifika kitajulikana Nini kifanyike ila Cha kwanza ili hayo yote yafanyike watadili kwanza na atmosphere hili si lakitoto Kuna mitambo maalum itatakiwa kusambazwa mars Sasa na ukubwa ilionao hehe! Itafanya kazi muongo mmoja.. hata hivyo si lazima ianze miti hapo ni mitambo kwanza mkuu shughuli Ni pevu
 
Kama tu dunia imeshindwa kuwa suluhisho LA kudumu LA radioactive waste, itaweze kuwa na suluhisho LA solar radiation bado safari in ndefu sana
 
Haya masuala yanaenda kimkakati, Hyperloop ni teknolojia yenye kasi zaidi ya Rocket Jets hivyo uhakika wa muda sio tatizo tena.
Asante mkuu kwa kunitoa wasiwasi wa muda.
Mkuu funguka zaidi juu ya teknolojia hii namna inavyeweza kutufikisha Mars kwa njia ya 'short cut'
 
Hahaha kumbuka kuvuja kwa pakacha ni nafuu kwa mchuuzi. Wakiondoka sisi tunapumua,dunia imejaa hii ndugu, ukiwakatisha tamaa ni kujiongezea mzigo.
Kule kwetu kuna msemo, kijana akikuaga anaondoka nyumbani kwenda kutafuta maisha, mpe mzigo wa baraka kisha msindikize, ukimgomea unaweza kumlisha mpaka ufe au afe yeye.
 
Mkuu isajorsergio nimeona LEXUS nao wameamua kulivalia njuga swala la kuondoka lakini wao wamejikita kwenye safari ya mwezini.
Nimeangalia design zao za LEXUS-LUNAR nikacheka tu. Hivi NASA na SpaceX wamefikia stage gani ya design ya vyombo na logistic ya kwenda huko kuishi? Na vipi yule tajiri Brandon aliyetaka kufanya Space tourism yeye anaanza lini?
 
Ubunifu wa vifaa na vitendea kazi kwa asilimia kubwa unaangazia utendaji, mahitaji na muda siyo urembo ndio maana designs mbalimbali zinaonekana kituko lakini kuna sababu katika hilo.

Artis chombo hiki hivi karibuni kitaondoka kwenda Moon na kisha kurudi.

NASA Space Ship hii kwa uhakika kinatarajia kuanza shughuli za kupeleka watalii, watafiti na watu wa media hivi karibuni.

Mpango wa Billionaire kwenda Moon bado upo kama mkataba unavyotanabaisha.
 

kitu ambacho mpaka sasa mashirika makubwa kama nasa wameshindwa kufika kwa haraka ni mifumo ya vyombo ambavyo utumia nishati kubwa kutembea kwenda sayari nyengine hata kupelekea mda mrefu kufika chombo chochote.
kama wataweza kuwa na utafiti wa (gravitation magnet motion ) basi hii itafanya hata kufika huko pluto.ni wazo tu katika kufikiria


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hakika, lakini kwa muenendo huu wa ushirika kati ya Elon Musk (SpaceX) na NASA kuna mazuri zaidi yanakuja.

Elon kuja na hii Hyperloop itaongeza kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…