PreGE2025 POTOSHI Picha hizi za Boniface Mwangi leo Mei 22, 2025

PreGE2025 POTOSHI Picha hizi za Boniface Mwangi leo Mei 22, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu hizi picha zinazomuonesha Boniface Mwangi akiwa na amjeraha ni za leo Mei 22, 2025?
1747990866959.png

1747990893600.png
 
Tunachokijua
Boniface Mwangi ni mwanaharakati kutokea nchini Kenya ambaye alikuja kuhudhuria kesi ya Tundu Lissu. Taarifa zilionesha Mwangi akifuatwa hotelini na watu waliojitambulisha kama polisi na baadaye mtandao wa watetezi wa Haki za binadamu Tanzania (THRDC) walithibitisha kuwa Mwangi anashikiliwa na polisi kituo cha kati Dar es salaam.

Mwangi alipatikana Mei 22, 2025 katika mpaka wa Horohoro akiwa na hali mbaya kwa kuonekana kuwa ameshambuliwa.

Madai

Kumekuwapo na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazomuonesha Boniface Mwangi akiwa na majeraha na kudaiwa kuwa zimetokana na kushambuliwa Mei 22, 2025. Mtumiaji mmoja wa X alichapisha picha hizo na ujumbe uliosomeka;

“Kitendo kilichofanywa na Serikali ya TZ hakikubaliki hata kidogo, Walishindwa nini kumrudisha #BonifaceMwangi nchini kwao bila kumduru? Hii inaweza kuwaletea shida kubwa Watanzania waishio Kenya…” Tazama hapa

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa picha hizo zinapotosha uhalisia kwani hazihusiani na tukio la Mei 22, 2025 kama inavyodaiwa. Ufuatiliaji kwa kutumia Google image reverse seach na maneno muhimu (Keyword search) umebaini kuwa picha hizo ni za tukio lililomtokea Boniface Mwangi Aprili, 2025.

Aprili 21, 2025 Citizen TV ya kenya iliripoti taarifa yenye kichwa kinachosomeka “Activist Boniface Mwangi says assaulted, robbed by Nairobi cops” ikiwa na maana “Mwanaharakati Boniface Mwangi asema alivamiwa na kuporwa na polisi wa Nairobi”. Taarifa hiyo iliambatana na Picha zinazookekana kutumika hivi karibuni na kuhusishwa na tukio lake la kushambuliwa alipotoka Tanzania.

Mwangi kupitia ukurasa wake wa X tarehe 21 Aprili, 2025 alichapisha taarifa pamoja na picha zinazomuonesha kuwa na majeraha akiwa hospitalini ambazo ndizo zilizotumika tena Mei 22, 2025. Katika taarifa hiyo Mwangi alieleza kuwa majira ya saa 3:30 Usiku tarehe 2 April, 2025 alivamiwa na watu waliojitambulisha kama polisi.
Wakenya wanapenda attention sana
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Wakenya wanapenda attention sana
Attention wanapewa na Watanzania wasiojitambua ambao wanawatukuza sana hawa jamaa! Wenyewe utawasikia, "Wakenya hivi" "Wakenya vile" huku wakisifia mambo ambayo hata wenyewe wanaweza kuyafanya kama sio unafiki wao! Matokeo yao, Wakenya wamefikia wapo above all, na ndo maana mara kwa mara huwa wanawakashifu Wabongo na wana kila uhalali wa kutukashifu kwa sababu tumezidi shobo!
 
Back
Top Bottom