Picha hizi zinathibitisha uhusiano wa karibu kati ya Kenya na Uingereza

Picha hizi zinathibitisha uhusiano wa karibu kati ya Kenya na Uingereza

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Karibu marais wote wa Kenya wamewahi kuonana na malkia Elizabeth II kasoro William Ruto ambaye ameenda kumzika.

Hapa kwetu ukiondoa mwalimu Nyerere Nani mwingine?

Tuliwahi kumuweka mtu mmoja pale ikulu kila uchwao yeye alikuwa akiwaita wazungu mabeberu. Yule mtu sijui tuliteleza wapi?

20220919_060721.jpg
20220919_060716.jpg
20220919_060711.jpg
20220919_060705.jpg
 
Malkia ni muwekezaji Kenya, wakenya ni manamba wa wawekezaji kutoka nje, huo ndiyo uhusiano wa Kenya na nchi za magharibi, a master and obedient servant.

Kenya is very submissive to west. Ni nchi hatari sana kushirikiana nayo ku-pursue pan africanism agenda.

Wakenya ni wazungu. Pathetic
 
Kwahiyo ulitaka viongozi wa nchi zote za Africa washindane kwenda kuonana na Malkia? Fikra za kitumwa hizi.
Tunaongelea uhusiano mwema. Vyuoni kuna programs za Foreign Relations unajua zinalenga nn?

Acha kuwa kama yule jamaa aliyekuwa akimuogopa kila mzungu na kumuita beberu.
 
Kwahiyo kuwa na uhusiano na UK,(wazungu) ni ishala ya maendeleo kwa mtu mweusi? Hata kama hao viongozi kwenye nchi zao kumejaa Rushwa,umaskini,ufisadi,lakini kwa vile wanauhusiano na UK(wazungu,). Hilo pekee linatosha! Tunastahili kukenua na kushangilia!
Hizi ni "colonial mentality"
 
Hivi mkuu kabla ya kuandika huwa unafikiria kwanza, au huwa unaandika ndio baadae unafikiria?, Sasa kuonana na Malkia ndio sifa?, Kuwathamini na kuwanyenyekea wazungu kwako ndio jambo la maana?, Hivi hujui ni kiasi gani Nyerere alivyowachachafya wazungu na wengi aliwatimua na kufunga balozi zao?

Mkuu, weka posts zenye kuibua mijadala ili watu waweze kuweka michango yenye tija, punguza ushabiki na posts nyepesi nyepesi Kama hizi.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Navyosikia Malikia alitaka kumsalimia Mwalimu kwa kummpa mkono huku amevaa gloves, Mwalimu akaona hii ni dharau na yeye akampa kile kifimbo...na huo ndio ukawa mwisho wa marais wa Tanzania kukutana na huyo malikia 🐒
 
Malkia ni muwekezaji Kenya, wakenya ni manamba wa wawekezaji kutoka nje, huo ndiyo uhusiano wa Kenya na nchi za magharibi, a master and obedient servant.

Kenya is very submissive to west. Ni nchi hatari sana kushirikiana nayo ku-pursue pan africanism agenda.

Wakenya ni wazungu. Pathetic
Ukweli mtupu!
Hata hii choko choko ya bomba la mafuta(Hoima - Tanga), kuna mkono wa huyu jirani mnafiki.
 
Wakenya huwa nao wanajionaga Wazungu na kujipendekeza kwa Wazungu ni kawaida yao, Kifupi hata siku tukitaka kuikomboa Africa basi moja ya watu watakaotukwamisha niKeTz
Ukweli mtupu!
Hata hii choko choko ya bomba la mafuta(Hoima - Tanga), kuna mkono wa huyu jirani mnafiki.
Wacheni kujitenga na ulimwengu majirani, ushirikiano/umoja ni nguvu, and for your information Sir, sisi sio wanafiki!!!
 
Tunaongelea uhusiano mwema. Vyuoni kuna programs za Foreign Relations unajua zinalenga nn?

Acha kuwa kama yule jamaa aliyekuwa akimuogopa kila mzungu na kumuita beberu.
Hiyo foreign Relations ni lazima kila kiongozi aende kwa Malkia?

Malkia yeye alikua haitaki hiyo foreign Relations kutoka upande wake?

Yeye alikua anawafuata hao viongozi kwenye nchi zao?
 
Ambao hawakumuita mzungu beberu mbona hujaweka picha zao wakiwa na malkia?
 
Back
Top Bottom