Picha: Hospitali ya Rufaa ya Chato iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi. Kuhudumia takriban watu milioni 18 mikoa ya Kanda ya Ziwa

Ok, sasa nimeelewa. Kibao hapo kwenye construction site kinasomeka kuwa client ni Chato District Council. Kumbe ni hospitali ya halmashauri wameamua iwe ya tofauti sana na halmashauri zingine, na hata jina wakataka isomeke ni ya rufaa ya kanda!
 
Kanda ya Burigu ndiyo mikoa ipi?
Habari inasomeka kuwa ni hospitali ya rufaa ya kanda ya Burigi
 
Zamani kulikuwa na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma ikijulikana kama CDA

Sasa zama hizi za ustawishaji wa jiji la Chato sijui mamlaka yao inaitwaje??

Mje, mtujuze...

Mkuu kama unasema kweli basi hiyo mamlaka ni upuuzi yani walishindwa hata kupanda miti Dodoma huko
 
Duh....... Mbona ni jirani zaidi kumpeleka mgonjwa Bugando Mwanza ukitokea Geita, kuliko kumpeleka Chato
Bugando ni ya misheni siyo ya serikali. Chato ikikamilika ruzuku itaondolewa Bugando. Huduma za matibabu zitakuwa ghali sana. Wote wa kanda ya ziwa mtalazimika kufuata huduma za bei rahisi Chato referal.

Nakumbuka kuna mbunge mmoja wa mikoa ya kusini alihoji umuhimu wa kuwa na referal hosipital 2 kanda ya ziwa wakati kule Mtwara na Lindi hakuna hata moja, majibu aliyopewa na speaker ni Mungu mwenyewe anajua.

Ila kwa hayo mabunduki niliyoyaona hapo kwenye uwekaji jiwe la msingi mhhhh.
 
Hawezi kutuambia anaumia kaburini wakati YEYE ndie alitengeneza imperial presidency and rubber stamp parliament...

Very right. Nyerere asingeweza kushangaa haya. Aliyatarajia lakini hakuwa na ujasiri (guts) wa kuyazuia. Angeumia ndani kwa ndani tu na kutoa hotuba za mipasho kama za enzi za mzee ruksa.

Alizidiwa na hofu ya CCM kuondolewa madarakani endapo katiba ingerekebishwa kusimamia misingi thabiti ya demokrasia.

“I can’t let my country go to the dogs”. Alisema. Naona hadi dakika ya mwisho hakuamini chama kingine nje ya CCM kushika madaraka pamoja na kujua hatari ya katiba iliyopo kwa Rais atakayekuwa na hulka ya udikteta.

Sisi ni watu wa maslahi binafsi zaidi; hatuna ujasiri wa kufa kudai haki na utawala bora. So let it be. Kila mtu na lwake.
 
Milele na milele uishi meko.
Tunakupenda na tunaomba uongeze % heslib wakatwe 40% .
Na tra ongeza iwe 28% badala ya 18%.
Asante Meko
 
That's the classic catch-22 the contry is and will be engulfed in for decades to come.

CCM ikiruhusu misingi ya utawala bora na demokrasi wanaweza kuondolewa madarakani. Tunakwama hapo.

Labda atokee mwana CCM mwana demokrasia na mtawala bora awasaliti wenzie. Lakini unampataje mtawala bora kutoka CCM wakati ili uibuke ndani ya CCM ni lazima upikwe na upitishwe na mfumo CCM kwanza, wa chama kushika hatamu, bunge dhaifu, mahakama zinazoufyata mbele ya serikali, and imperial Chairman President with carte blanc rule?
 
Wote ni walewale sijaona tofauti kati ya Bugando na Muhimbili
 
Kwa miaka kumi kumi kila Rais akiamua kufanya hivi kwa Nini Tanzania isiwe Kama Ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…