Picha za Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita ambayo imewekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita leo tarehe 11 Januari 2021.
Nimekuja kugundua Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa ni RAIS NA NUSU. Alitumia muda wake madarakani kuijenga Tanzania, sio Butiama au Musoma.
Hebu fikiria ule uwanja wa Ndege wa KIA ulioko Kilimanjaro. Frankly speaking, ule uwanja Nyerere angeweza kuujenga Mugumu Serengeti, ambako ni mkoa wa Mara anakotoka. Kwakeli katika kutembea kwangu Tanzania, nimegundua kuwa mji wa Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara ulipaswa kujengwa kimkakati, ili pamoja na jiji la Arusha, iwe ni major gateway za kuingiza watalii katika ukanda wa utalii wa kaskazini mashariki mwa Tanzania, ambao ndio strongest zone ya utalii Tanzania na Africa Mashariki. Hata wilaya ya Loliondo ina the same features kama Mugumu za kuwa strong gateway za kuingiza watalii wengi.
Lakini, Mwalimu Nyerere hakutazama kwao kwanza, bali alitazama nchi. Nilifanikiwa kumuuliza mzee mmoja ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchi ( kwa sasa ni marehemu), kwanini Mwalimu Nyerere aliamua kuijenga kaskazini mashariki mwa TZ kiutalii, badala ya Mugumu? Yule mzee akanijibu kuwa, Nyerere alikuwa haongozwi na ubinafsi katika kuijenga Tanzania, bali uzalendo na uhalisia wa hali halisi ya mambo. Akasema, pamoja na mapungufu mengi ya Nyerere, lakini weledi wake kiutawala ulimfanya aheshimike sana. Yule mzee akaendelea kusema kwamba, ukanda wa Arusha-Moshi ilikuwa ni sahihi kuliko Mugumu Serengeti kujenga uwanja wa ndege, sababu tourism ecosystem ya Africa Mashariki ilishikiliwa na jiji la Nairobi Kenya kwa kiasi kikubwa, ikifuatiwa na Arusha Tanzania, na miji hii inategemeana sana kiutalii. Vilevile Mlima Kilimanjaro una umuhimu wa pekee katika ecosystem ya utalii ya Kaskazini Mashariki mwa TZ. Kwasabu hizi, ilibidi KIA ijengwe ilipo sasa. Huyo ni Nyerere.
So far, sijashawishika kabisa na justification zinazotiwa na JPM kuijenga Chattle kwa speed na magnitude hii. Kama hospitali za kanda, serikali ilipaswa kutuambia kwanza, why Chattle na not elsewhere huko kanda ya ziwa. Likewise, JPM alipaswa kutuambia, hospitali za kanda zingine, zinajengwa wapi na lini? Ikumbukwe kuwa, tayari Chattle ina uwanja wa ndege wa kimataifa, of which, hakuna so far hakina vivid economic rationale ya kuujenga huo uwanja pale. Ni bora huo uwanja ungejengwa katika mji wa Katoro-Geita sababu wafanyabiashara wengi wangeutumia kuliko kwenda Mwanza. Frankly, mji wa Chattle hauna any economic rationale ya kujengwa uwanja wa ndege kwa sasa. Alafu hatujazungumzia proposed ujenzi wa uwanja wa mpira Chattle, na ujenzi unaoendelea wa maofisi makubwa ya umma, ambayo hadhi yake inazidi hadhi ya majengo ya aina hiyo katika wilaya zingine.