Hii ni hospitali ya wilaya ila imebadirishwa kuwa ya kanda.
Pia ni makosa kwa sababu hospitali ya kanda ji hospitali ya rufaa ya mkoa iliyoboreshwa lakini geita tayari kuna hospitali ya rufaa ya mkoa wa geita ambayo tayari imejengwa toka mwaka 2016.. kwa nini kuwa na hospitali mbili za rufaa mkoa mmoja ambao haona watu wengi kama dar au mwanza.
Tungeweza ifanya hospitali ya rufaa ya mkoa wa geita ambayo ni mpya kuwa hositali ya kanda kama ilivyo hospitali ya rufaa ya mkoa wa mbeya.
Na baada ya hapo tukajenga hospitali kubwa kanda ya magharibi ambako kumesahauliwa sana mikoa ya rukwa, katavi na kigoma.
Tanzania tuna kanda 7
1. Kanda ya pwani/ mashariki - dar, morogoro, pwani, Tanga
2. Kanda ya nyanda za juu - Iringa, mbeya, songwe na Njombe
3. Kanda ya kusini - mtwara, lindi na ruvuma
4. Kanda ya magharibi - Katavi, rukwa, kigoma na tabora
5. Kanda ya kaskazini - kilimanjaro, arusha, manyara
6. Kanda ya kati - Dodoma, Sindida
7. Kanda ya ziwa- simiyu, Mara, shinyanga, mwanza, geita, kagera
Picha za Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita ambayo imewekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita leo tarehe 11 Januari 2021.