PICHA: Huyu hapa ndio Binti wa kwanza wa Ndugai. Aumizwa sana na wanaomsema vibaya Mitandaoni baba yake

PICHA: Huyu hapa ndio Binti wa kwanza wa Ndugai. Aumizwa sana na wanaomsema vibaya Mitandaoni baba yake

Ndugu zangu Watanzania,

Huyu ndiye Binti wa Kwanza wa Mheshimiwa Jobu Ndugai ambaye amefariki Dunia hapo Siku ya Jana.

Embu soma kama ilivyo. Mimi nimeichukua kama picha ila ni Video ya Dakika saba binti Wa Marehemu Ndugai akielezea kwa hisia kali sana na uchungu sana juu ya kifo cha Baba yake na Maneno ya Mitandaoni.👉Catherine Ndugai,Mtoto wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Dodoma amezungumza na kueleza jinsi alivyokutana na Baba yake kwa mara ya mwisho kabla ya kifo chake.

Akizungumza na Ayo TV leo akiwa Mkoani Arusha amesema kuwa yeye hakuwahi kutamani kuingia kwenye siasa na wakati mwingine huwa akiona maneno yanayotolewa kwa wanasiasa hata kama hayamhusu baba yake huwa yanamuumiza.

Aidha, ameeleza kukerwa na baadhi ya watu wanaomzungumzia vibaya Baba yake kwenye Mtandao na kusema hizo ni hisia binafsi za watu na haziwezi kumuathiri kwa kuwa alikuwa anamfahamu Baba yake vizuri
#MillardAyoUPDATES

View attachment 3435343View attachment 3435344
Samia na Kikwete wao itakuwa FUNGA KAZI, acha tu waaendelee kutuchelewesha kupata demokrasia ya kweli kupitia MIFUMO HURU YA UCHAGUZI na KATIBA MPYA.
 
Msikimbilie kutiatia huruma kipindi cha misiba,mnatakiwa mjiulize zamani haya mambo ya kufurahia kifo yalikuwepo?
Je, kwanini siku hizi yanajitokeza? Tatizo nin?
 
Samia na Kikwete wao itakuwa FUNGA KAZI, acha tu waaendelee kutuchelewesha kupata demokrasia ya kweli kupitia MIFUMO HURU YA UCHAGUZI na KATIBA MPYA.
Ya huyo Bi Chura na huyo Luteni tapeli yatavuma sana.
Ila UHURU kamili utapatikana siku ccm ikifa!
 
usawa ni ngumu kupatikana mahali popote pale

rip job
Weka mshahara wa wabunge milioni 3 tu,kata marupuru yote,harafu wajitolee vikao bila posho.Hakutakuwepo na kelele kabisa za siasa.Hao binadamu wako bungeni kimaslahi tu.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Weka mshahara wa wabunge milioni 3 tu,kata marupuru yote,harafu wajitolee vikao bila posho.Hakutakuwepo na kelele kabisa za siasa.Hao binadamu wako bungeni kimaslahi tu.
Na wewe nenda bungeni kama ni rahisi.
 
Na wewe nenda bungeni kama ni rahisi.
Bila bunge inawezekana sana,na kuwa na bunge la wananchi wa mapato ya kawaida inawezekana.
Ili kulitakasa bunge mishahara yao liendane na GDP.
Na huo ndio muarobani wa wanaotamani kula bila kunawa.
 
KIFO NI KOFO.
FURAHA YAO NO VIFO VYETU NA FURAHA YETU NI VIFO VYAO.
MUNGU FUNDI.
 
Mara nyingi watu wanaosomeaga ualimu ni wale wenye mentality ya uoga wenye kuwaza hivi"bora niwe na kidogo chenye uhakika kuliko nitafute kingi ambacho sina uhakika nacho"
Tufanyaje sasa mkuu, ndiyo kazi yatuweka mjini at least
 
Back
Top Bottom