Oicha hii inasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya watu wanadai imepigwa nchini Tanzania, lakini kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Serikali yetu imefanya mimi siamini kama ni kweli imepigwa nchini kwetu.
Je, hii picha ni Tanzania?
Je, hii picha ni Tanzania?
- Tunachokijua
- JamiiForums imefanya ufuatiliaji na kubaini kuwa picha hii ni mazingira ya Tanzania, ilipigwa kijiji cha Wami Sokoine wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Picha hii ilipigwa na kutumiwa katika ukurasa wa X (Zamani Twitter) wa East Africa Radio na ITV mnamo Novemba 4, 2015. Picha hii ilitumika kuelezea adha ya maji iliyokuwapo katika kijiji cha Wami.
Pia, Capital Radio walichapisha picha hii siku hiyo ya Novemba 4, 2015.
Wananchi wa kijiji hicho walikuwa wakilalamika kutumia maji machafu yanayotumiwa na mifugo kwa muda mrefu hali iliyotishia afya za wananchi hao kwa kuhofia kupata magonjwa, na hununua dumu moja lenye maji safi lita 20 kwa Tsh. 1500/-
Aidha, JamiiForums imefanya mawasiliano na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ili kujua hali ya sasa ya eneo hilo ambapo wamekiri bado eneo hilo lina ukame.
Mkazi huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi alisema
"Hii sehemu ni Dakawa Wilayani Mvomero ndiyo kuna hivi vijiji. Inaishi jamii ya Wamasai ambao wanategemea maji kwenye mabwawa. Jua likiwakwa Mabwawa huwa yanakauka. Kulikuwepo na uhaba wa maji ila Wiki hii Mvua imenyesha sana"