KWELI Picha inayoonesha watu wakinywa maji machafu pembeni ya dimbwi imepigwa nchini Tanzania

KWELI Picha inayoonesha watu wakinywa maji machafu pembeni ya dimbwi imepigwa nchini Tanzania

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Oicha hii inasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya watu wanadai imepigwa nchini Tanzania, lakini kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Serikali yetu imefanya mimi siamini kama ni kweli imepigwa nchini kwetu.

Je, hii picha ni Tanzania?

1669363812704.png
 
Tunachokijua
JamiiForums imefanya ufuatiliaji na kubaini kuwa picha hii ni mazingira ya Tanzania, ilipigwa kijiji cha Wami Sokoine wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Picha hii ilipigwa na kutumiwa katika ukurasa wa X (Zamani Twitter) wa East Africa Radio na ITV mnamo Novemba 4, 2015. Picha hii ilitumika kuelezea adha ya maji iliyokuwapo katika kijiji cha Wami.

Pia, Capital Radio walichapisha picha hii siku hiyo ya Novemba 4, 2015.

Wananchi wa kijiji hicho walikuwa wakilalamika kutumia maji machafu yanayotumiwa na mifugo kwa muda mrefu hali iliyotishia afya za wananchi hao kwa kuhofia kupata magonjwa, na hununua dumu moja lenye maji safi lita 20 kwa Tsh. 1500/-

Aidha, JamiiForums imefanya mawasiliano na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ili kujua hali ya sasa ya eneo hilo ambapo wamekiri bado eneo hilo lina ukame.

Mkazi huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi alisema

"Hii sehemu ni Dakawa Wilayani Mvomero ndiyo kuna hivi vijiji. Inaishi jamii ya Wamasai ambao wanategemea maji kwenye mabwawa. Jua likiwakwa Mabwawa huwa yanakauka. Kulikuwepo na uhaba wa maji ila Wiki hii Mvua imenyesha sana"
Kila kukicha ni afadhali ya Jana, Tz ya 2020 ++ Ina maisha magumu kuliko ya miaka ya mkoloni
 
Ooh kama toka 2015 hadi sasa wapo hivyo, serikali Iko wap hapo?

Au serikali ipo DAR pekeake,
Serikali haiangaiki na wamasai wapumbavu wanaoama ama sana Kila Kona ya nchi hii
 
The people of Wami Sokoine village, Mvomero district, Morogoro region have complained about using dirty water used by livestock for a long time, a situation that threatens the health of the people for fear of getting diseases.
Huu si ni uchochezi tu? Hebu futa maneno WAMI SOKOINE VILLAGE andika Nzega au Makunduchi au Pemba au Rombo, tofauti ni nini? Nani anapenda maji machafu? Hizi ni mbinu ovyo za Wapinzani kujijengea uhalali, kufitinisha wananchi na serkali yao. Si muda baadaye watasema "MIAKA SITINI BAADA YA UHURU" au "WENYEWE WANATEMBELEA VX". Cheap politics.
 
Je, hii picha ni Tanzania?

View attachment 2427093
Hili ni tambiko la kabila la Wakaguru. Mvua ya kwanza ukinywa maji yake huwa yana neema kwa mwaka mzima. Na si hapa tu - ukienda India, mji wa Veranasi jimbo la Bihar panapogawanyika Mto Ganges kuelekea Bangladesh, Wahindu hupaona ni mahala patakatifu kunywa kuoga au hata kufa sehemu hiyo. Kila mwaka Mahujaji huwa ni wengi kuliko Makka.
 
hapa lazima kuna walakini.

haiwezekani jamii hiyo yote pasiwe na hata mmoja mwenye Ustaarabu wa kutumia chombo mbadala na ndoo
Wanakunywa baada ya hapo wanachota ya kubeba kupeleka majumbani mwao, bilauri au vikombe si sehemu yake hapo.
 
Hayati alijaribu kufika maenei yooooote TZ. Bila kubagua mjini au vijijini , ila kazi ya muuumba haina makosa ikaishia njiani
 
Back
Top Bottom