Uchaguzi 2020 PICHA: Ingetokea kada wa CHADEMA ndiye angetinga hivi kwenye mkutano wa mgombea wa CCM, angetoka salama?

Uchaguzi 2020 PICHA: Ingetokea kada wa CHADEMA ndiye angetinga hivi kwenye mkutano wa mgombea wa CCM, angetoka salama?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Nimemfuatilia sana huyu jamaa kwenye mkutano wa Chadema uliokuwa unahutubiwa na Mh. Tundu Antiphas Lissu, alivyokuwa anahangaika, mara atoe kiredio chake mfukoni kama vile anawasiliana na mtu asiyeonekana, mara atafute namna ya kusogea karibu zaidi na alipo Mh. Lissu, mara atafute nafasi ya kusikia vizuri zaidi anayasema...lakini wana Chadema hata hawakuhangaika naye!

UVCCM ahangaika kumsikiliza Mh. Lissu.jpg

Sasa nikabaki najiuliza, je hali ingekuwaje kama mwana Chadema ndiye angetinga katika mkutano wa CCM na magwanda yake halafu mara anapiga picha, mara kama vile anawasiliana na mtu, mara anajaribu kusogea na alipo mgombea. Je, kweli angetoka salama?

Nawavulia kofia wana Chadema kwa kutomjali huyu na kutohangaika naye katika hizo juhudi zake hizo pamoja na kuvaa fulana ya hapa kazi tu na. kofia ambayo yawezekana ni ya wana Usalama au vijana wa UVCCM.
 
View attachment 1601410

Hapa anaonekana akitoa simu yake mfukoni kuwasiliana na mtu​
Duh, Mag3 asante sana mkuu kumbe na wewe ulikuwa makini kumfuatilia? Hata mimi nilikuwa naye sambamba kwa kila tukio alilokuwa analifanya. Alikuwa anahangaika sana nikasema wacha niwe naye sambamba! CHADEMA kwa kweli wana uvumilivu wa hali ya juu!
 
Hapo umeharibu kabisa, hivi hujui kama unawagawa Watu kupitia timu?
Mfano mimi Yanga nakuelewaje hapo acha hizo bwana.
Ushawaona washabiki wa timu ya Simba wanahangaika na washabiki wa yanga!?
Ndiyo utakapojua kwa nini mechi iliahirishwa!
 
Inawezekana ni mtanzania masikini kama tulivyo wengi, hakua na shati lingine la kuvaa, lakini akaona isiwe nongwa wacha niende hivyo hivyo kumsikiliza rais wa awamu ya sita.

After all, CDM ni full amani, tofauti na kule kwingine kwenye mabunduki na gari la machumachuma.
 
Nimemfuatilia sana huyu jamaa kwenye mkutano wa Chadema uliokuwa unahutubiwa na Mh. Tundu Antiphas Lissu, alivyokuwa anahangaika, mara atoe kiredio chake mfukoni kama vile anawasiliana na mtu asiyeonekana, mara atafute namna ya kusogea karibu zaidi na alipo Mh. Lissu, mara atafute nafasi ya kusikia vizuri zaidi anayasema...lakini wana Chadema hata hawakuhangaika naye!

Sasa nikabaki najiuliza, je hali ingekuwaje kama mwana Chadema ndiye angetinga katika mkutano wa CCM na magwanda yake halafu mara anapiga picha, mara kama vile anawasiliana na mtu, mara anajaribu kusogea na alipo mgombea...je kweli angetoka salama?

Nawavulia kofia wana Chadema kwa kutomjali huyu na kutohangaika naye katika hizo juhudi zake hizo pamoja na kuvaa fulana ya hapa kazi tu na. kofia ambayo yawezekana ni ya wana Usalama au vijana wa UVCCM
Chadema wameelimika!! Ccm washamba!!
 
Back
Top Bottom