Picha: Kaburi la Ruge laanza kuchimbwa huko kijijini kwao Bukoba

Picha: Kaburi la Ruge laanza kuchimbwa huko kijijini kwao Bukoba

Hivi ndege toka south africa ingepeleka mwili wa marehemu bukoba moja kwa moja au mwanza airport kuna tatizo gani?kisha kuagwa na kuzikwa.
Kwa nini uletwe dar kisha tena safari ianze kwenda bukoba?
Dar ndipo watu wengi walipo. I mean almost marafiki.. serikal.. wafanyakaz wenzie.. wengi wapo dar. Ni bora wakamalize taratib huko then wampeleke bukoba.
Na vile pesa si tatizo sion shida yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ndege toka south africa ingepeleka mwili wa marehemu bukoba moja kwa moja au mwanza airport kuna tatizo gani?kisha kuagwa na kuzikwa.
Kwa nini uletwe dar kisha tena safari ianze kwenda bukoba?
Afrika inahitaji watu wenye mtazamo chanya kama wewe.
 
Nimeona hilo kaburi ghafla nimekumbuka pale Mungu anaposema mwanadamu ni mavumbi na hakika utarudi mavumbini.
 
Mila za kichaga kaburi huchimbwa siku ya mazishi; kama mazishi ni Jumatatu, uchagani kaburi litaanza baada ya saa sita usiku Jumapili.
Mkoa wa kagera kwa sehemu kubwa kijiografia ni milima hivyo basi chini ya ardhi ni mawe changarawe na miamba migumu

Ndo maana kaburi huandaliwa mapema sana ili kuepuka adha ya kusubiri siku ya mazishi na kuhangaika kuchimba sehemu tofauti tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona nyerere hakupelekwa butiama moja kwa moja. Hujachangia chochote huna undugu nae kaa kimya hayakuhusu. ACHA KUFANANISHA NYERERE NA VITU VYA KIJINGA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mila za kichaga kaburi huchimbwa siku ya mazishi; kama mazishi ni Jumatatu, uchagani kaburi litaanza baada ya saa sita usiku Jumapili.
Basi Mila ni tofauti . wahaya kaburi hata ukijichimbia mapema hakuna shida
Pia kuna koo nyingine zina makaburi tayari yaliyojengwa Kwa ajili ya wanaukoo
Seminary ya Rubya ambapo huzikwa mapadre wa jimbo la bukoba huwa kunatengenezwa makaburi kabula hata mapadre hawajafa
Sasa kama uchagani mnachimba mapema kanisa katoliki linao utaratibu wa kuzika maaskofu kanisani ambapo makaburi huwa yamechimbwa tayari je hapo hamuharibu utamaduni wenu
Na je makaburi yenu hamuyajengei Kwa ndani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom