PICHA: Kama unalijua hili tangazo, punguza ulaji wa chumvi na sukari, ongeza mazoezi

1999-2000 ni miaka zaidi ya 24, waliokuwa na 20 kipindi kile saa hii Wako 40s.
Humu JF wapo mpaka watu Wana miaka5 na tangazo wanalijua.
Hili tangazo vijana at late 29'S and early 30'S wanalijua maana ilikua kama katuni kwao enzi ni wakiwa na miaka5 au6.

Labda useme tangazo la miaka ya themanini au tisini mwanzo
 
Sasa hili tangazo mbona la juzi tu hapa? ITV yenyewe imeanzishwa miaka ya 90 katikati! Ungeleta matangazo kama yale ya "Pika kwa Kimbo, Pika kwa Kimbo" au yale ya kumbi za sinema kama Empire Cinema, Drive In Cinema, Odeon Cinema n.k.
 
1999-2000 ni miaka zaidi ya 24, waliokuwa na 20 kipindi kile saa hii Wako 40s.
Miaka 40 bado kabisa. Hapo ndio akili imeanza kukomaa. Ndio maana hata Katiba ya Tanzania inaruhusu mwananchi wa kuanzia miaka 40, kugombea kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi. Uzee unaanzia miaka 60.
Pamoja na porojo zote hizo, kuzingatia ULAJI SAHIHI hakujalishi umri wa mtu. Kila mtu anatakiwa kuzingatia sana ulaji na unywaji sahihi wakati wote wa maisha yake- tangu utoto hadi uzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ