PICHA: Kama unalijua hili tangazo, punguza ulaji wa chumvi na sukari, ongeza mazoezi

Hili tangazo siyo la Kizamani kihivyo...nadhani angalau aliyekuwepo wakati wa vitu vifuatavyo
  1. Kama umepaka mafuta ya shanti / rays
  2. Umetumia mafuta ya kupikia inaitwa superghee, pride nk
  3. Umeogea sabuni ya lux
  4. Umetumia baiskeli aina ya swala
  5. Umewahi kusikiliza kipindi cha chibuku inayorushwa RTD (Radio Tanzania Dar -es Salaam) na kipindi cha Mikingamo wa umma
  6. Umepaka mafuta ya mkebe inayoitwa Yollanda
  7. nk nk nk nk angalau unaweza kuwa mtu zamani kidogo angalu.



 
Miaka 22 iliyopita ni juzijuzi. Usijifariji mkuu, ni jioni tayari, pita Kariakoo shimoni nunua mabilinganya, mapilipili hoho, makaroti na mabamia pika chukuchuku. Kula. Usisahau kufanya mazoezi.

Hilo tangazo hata kama ulilitazama ITV ukiwa primary angalau darasa la saba wakati huo wewe tayari unajukuu sasa!
 
Umekuwa serious Sana mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Uzi umekaa kimasihara huu
 
Humu JF wapo mpaka watu Wana miaka5 na tangazo wanalijua.
Hili tangazo vijana at late 29'S and early 30'S wanalijua maana ilikua kama katuni kwao enzi ni wakiwa na miaka5 au6.

Labda useme tangazo la miaka ya themanini au tisini mwanzo
Vijana ni wale waliozaliwa 2000s wengine wote tunaitwa mishangazi au age go.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Humu JF wapo mpaka watu Wana miaka5 na tangazo wanalijua.
Hili tangazo vijana at late 29'S and early 30'S wanalijua maana ilikua kama katuni kwao enzi ni wakiwa na miaka5 au6.

Labda useme tangazo la miaka ya themanini au tisini mwanzo
Makondeko bar,woowoowoo tukunyema
 
Uzee au ujana wa mtu wa 40+ inategemea na eneo husika kwa mfano kwenye mpira wa miguu unaitwa mzee lakini ukija kwenye siasa unaitwa "mtoto mdogo"
 
No, 1990.....
Siyo kweli, nina kumbukumbu tripu ya kwanza narudi Bongo ilikuwa mwaka 2000 ndio Mengi alileta hiyo Jackport Bingo baadaye Wahindi wakamletea kiwingu nao wakaanzisha Aladins Bingo.

Sikiliza nyimbo ya Sugu na Balozi Dar Dsm utaelewa, halafu fuatilia hiyo nyimbo ilitoka mwaka gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…