Elections 2010 PICHA: Kampeni za Slaa jijini Dar es Salaam leo

Elections 2010 PICHA: Kampeni za Slaa jijini Dar es Salaam leo

Asante Mugumu... espesheli kwa picha hii chini... ivi kwa nini nchi yenye uwezo wa kulima na kupata unga ina mikate ya bei zikuazo ?

Bango_mwembeyanga.jpg
 
Mdau ahsante kwa picha hizo.Inapendeza sana tuwahi vituoni siku ya kuwapoteza ccm,tena huu ndio muda wa kukagua majina kwenye vituo vyenu,nasikia kuna watu wamewekewa REMARKS kwamba wamepoteza sifa za kupiga kura,sasa sjui wamerudi udogo au wamekuwaje!:yield:
 
Mungu wetu tunayekuabudu, kukutukuza, kukuomba na kukulilia sikiliza kilio chetu utuondelee CCM na Kikwete na wale wote ambao wameifisadi nchi yetu. Amina.

Mulangira: usingeweka amina,si ndo tungeitikia Amina! Mi nimeitikia tayari!
 
Tuwekee jinsi ya kuhakiki majina kwa mtandao,watu wanansumbua sana ili niwatumia gateway,plz saidia.
 
Eeeeee Mungu wa Mbinguni. Tunaomba kwamba uwape watu wako wa Tanzania busara na hekima ili wapige kura ya kuleta mabadiliko katika nchi. Tuwezeshe kuiondoa nchi hii kutoka mikononi mwa mafisadi na kuirudisha mikononi mwa mwananchi wenye nchi. Eee Mungu tuondoe MIsri Utumwani utuingize Kanaani, nchi ya ahadi, naam nchi ya neema iliyojaa maziwa na asali, yaani huduma muhimu za jamii: elimu, tiba bure. Muungu tunakuomba kwamba kwa njia ya kura watu wako wamwidhinishe Dr. Slaa kuwa rais wa 5 wa nchi yetu. Tuna imani ya kuwa chini ya uongzi wake watu watapata maisha bora.

NAAM TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!
 
Nilikuwa kwenye gazeti moja la pro kikwete ambapo niliongea na some waandishi wanasema wazi wazi kwamba kura yao kwa slaa ila pesa za kikwete press team 2010 wanazila lakini wanampigia slaa. (........................)
 
Nilikuwa kwenye gazeti moja la pro kikwete ambapo niliongea na some waandishi wanasema wazi wazi kwamba kura yao kwa slaa ila pesa za kikwete press team 2010 wanazila lakini wanampigia slaa. (........................)

Ha ha ha, I bet you hata fisadi wa habari Muhingo wa Rweyemamu atampigia Dr Slaa kura
 
Bila ubishi Dr Slaa anakubalika. Kama uchaguzi utakuwa wa haki na watu tukapige kura basi kuna uwezekano wa CCM kuanguka vibaya sana mwaka huu.
 
Sasa sijui huo mkutano wa Jumamosi utakuwaje!

Jamani, kama Mheshimiwa Rais Kiwete anaitakia nchi yetu amani na maendeleo, basi atumie siku zilizobaki kutayarisha hotuba ya kukubali kushindwa, na kuwaaga Watanzania kwa tabasamu yake. Itakuwa vibaya sana kama atajaribu kung'ang'ania madaraka.

JK atakuwa Rais Mstaafu na heshima zake kama ataondoka kwa heshima kama walivyofanya Kaunda na Moi.
 
Tuwekee jinsi ya kuhakiki majina kwa mtandao,watu wanansumbua sana ili niwatumia gateway,plz saidia.

Ndugu usijisumbue kuhakiki kwa mtandao, kwa sababu mimi nimehakiki jina na kituo vipo kwenye database ya NEC lakini kituoni jina halipo katika yale yaliyobandikwa, ushauri wangu nenda kituoni kwako, muda umekaribia kwisha (anyway check hapa www.nec.go.tz)
 
mbona mkutano umejaa watoto wa shule!!! Bwahahahaha

Mkutano wa JK wafunga shule tano Send to a friend
Tuesday, 26 October 2010 21:08
0diggsdigg

Kizitto Noya, Mwanza
SHULE nne za msingi na sekondari zilizo kwenye Kata ya Nkome wilayani Geita, jana ziliahirisha masomo ili wanafunzi wahudhurie mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete Shule hizo za sekondari za Kabwela na Nyamboge na shule za msingi za Ihumilo na Mwaloni zenye zaidi ya wanafunzi 5000 kwa pamoja zilisitisha masomo na wanafunzi kufurika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ihumilo ambako mkutano huo ulifanyika. Source: Mwananchi
 
Luteni Makamba upo? Huchelewi kusema wanaohudhuria mikutanao ya wapinzani ni wahuni.
 
pamoja na umati huu mkubwa la muhimu kushinda vyote ni kuhimiza watu wakapige kura... na kuhakikisha kura zilizopigwa ni salama!!!
tafadhali tukumbuke tangazo la Mrisho mpoto kuhusu upigaji kura..
tukapige kura. tuhamasishane zaidi na zaidi
 
ngoja niimbe wimbo huu na kucheza
"namshangaa Bwana Yesu kila niendapo namkuta"
namshangaa Bwana yesu kila nindapo namkuta"
eeeeeeeeee namkuta ...............eeeeee namkutaaaa
:hippie::hippie::hippie::hippie::hippie::hippie::hippie::hippie:

:smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:
 
Back
Top Bottom