Elections 2010 PICHA: Kampeni za Slaa jijini Dar es Salaam leo

Elections 2010 PICHA: Kampeni za Slaa jijini Dar es Salaam leo

Mimi ni mwanachama Hai wa CHADEMA.
Naombeni ni seme sikufurahishwa na yule mgombea ubunge wa TEMEKE.
Alipewa dakika Mbili kuangalia uwezo wake wa kujenga hoja, anaanza kusema kama Kikwete hakufunzwa na Mama yake tutamfunza sisi.
 
Kuna kipindi Daily News walitoa picha ya Kikwete na wakaandika mamoth crowd, walikuwa sahihi sasa sijui wangeitaje kama wangekuwa wakichapicha picha bila zengwe.
Tukapige kura kwa umakini mkubwa ndugu zangu watanzania
 
Bora kikwete angeacha kampeni na kuwapa watz wanachotaka badala ya sasa anavyotishia watz...........hatumtaki na ajue hivyo...
 
Vyombo vya DOLA havijajiandaa kuwa na Commander-in-Chief mwingine zaidi ya JK. Tukumbushane tarehe 01/11/2010.
 
kweheri kwaheri wewe CCM,
umetudhurumu wewe CCM,
hatukutaki wewe CCM,
potea kabisa wewe CCM.

wamelaaniwa wote,
tena wameoza wote,
hawatufai wote,
tuwanyime kura zote
shairi maridadi
 
mbona mkutano umejaa watoto wa shule!!! Bwahahahaha
Umeona uniform ya shule gani hapo? hao ni vijana wenye umri zaidi ya miaka 18 ila kwa kuwa lishe ya waTZ ni ya kubabaisha na kukosa matumaini lazima waonekane wadogo. Subiri baada ya 31/oct utaona sura za matumaini
 
Ingekuwa Kenya kweli. Dr Slaa angekuwa Rais. Ndivyo Mwai Kibaki alivyoukwaa Urais mwaka 2002 kabla hajauvuruga ule wa 2007.
 
Bango_mwembeyanga.jpg


Wapenzi na wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa na bango lenye ujumbe mbalimbali, katika mkutano wa mgombea urais kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam hii leo.

SlaakuhutubiaManzese.jpg

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake wa kampeni leo mchana.

MpigaPicha_Mwembeyanga.jpg

Mmoja wa wananchi waliohudhulia mkutano wa mgombea uaris kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akipiga picha huku akiwa amevalia kofia yenye picha ya mgombea huyo

SlaakuhutubiaMwembeYanga1.jpg

SlaakuhutubiaMwembeYanga2.jpg


Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, katika mkutano wa kampeni, kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke hii leo.

Picha zote kwa hisani ya Joseph Senga
Kompyuta yangu imegoma kufungua hizi picha tangu jana nifanyeje?
 
Back
Top Bottom