PICHA: Kanye West na mkewe wajiongezea ulinzi maradufu

PICHA: Kanye West na mkewe wajiongezea ulinzi maradufu

Hii ndiyo tunaita "kukumbuka shuka asubuhi".
 
Kanye West alinukuliwa akisema kua tukio la kuvamiwa kwa mkewe lilimfanya awe "helpless" na akasema atafanya kila liwezekanalo kuilinda familia yake(ofkoz pesa anayo)

Hivyo basi kwa kushirikiana na mkewe Kim Kardashian, wameboresha safu yake ya ulinzi(Kim) kujihami na shambulio jipya kufuatia lile la Paris lililohatarisha maisha yake na kuporwa mali zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 10.

Sasa atakuwa na ulinzi wenye hadhi ya mkuu wa nchi. Vyanzo vilivyo karibu na Kim vimesema kuwa, sehemu ya timu yake ya ulinzi inaundwa na wafanyakazi wa zamani wa Secret Service, wenye silaha nzito.

Kutakuwepo na walau timu moja ya mapande ya watu kila aendapo. Pia gari yake itakuwa na silaha.

Baada ya shambulio hilo la Paris, Kim alikutana na wanajeshi wa zamani wa jeshi la Israel, CIA pamoja na wafanyakazi wa zamani wa Secret Service. Kanye alikutana na wamiliki wa makampuni makubwa mawili ya ulinzi.

Mlinzi wake, Pascal Duvier amebakizwa. Pia ulinzi umeimarishwa kwa dada zake, Kourtney, Khloe, Kendall na Kylie.

View attachment 415558

These people are so overrated na full vituko.
 
Binti alizidi kuonyesha ving'aro ng'aro vyake kwenye social media na kusema gharama ya kila king'aro ng'aro chake. Hiki milioni ngapi na kile milioni ngapi blah blah blah kumbe njemba zinapiga mahesabu tu jinsi ya kuvichukua ving'aro ng'aro hivyo na hatimaye wamefanikiwa tena kirahisi mno.
 
Walikua wanaviorodhesha kwenye notebook na walikua na calculator[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom