JK,
Hebu angalia haya maneno hapa chini:
''Lakini ukoloni ulikuwa na faida zake, na Rajabu Ibrahim Kirama nyota yake itakuja kunyanyuka na mwanga wake kuangaza sehemu nyingi za Uchaggani, lau kama itakaribia karne moja kabla ya historia kumtambua.
Nyota hii ya Rajabu Ibrahim Kirama itang’ara ilhali Chifu Abdieli anaishuhudia kwa macho yake.
Uhasama huu baina ya Chief Abdiel Shangali aliyekuwa akipambana na Rajabu Ibrahin Kirama kwa ajili ya jitihada zake za kueneza Uislamu Uchaggani taratibu ukapoteza ukali wa nguvu zake kwani Wachagga haukupita muda mrefu wakajitazama upya na kutambua kuwa kwa hakika adui hakuwa nduguye Mchagga Muislam; adui mkuu kwao wote ulikuwa ukoloni ambao ulihitaji nguvu ya pamoja kukabiliana nao.
Katika jitihada hizi za kujiletea maendeleo Wachagga wakaunda Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) Umoja wa raia wa Kilimanjaro.
Petro Njau akiwa kiongozi ili isimamie maslahi ya Wachagga kama taifa.
Katika kanuni za KCCU, zinawataja Wachagga kama watu waliozaliwa huru na wenye haki ya kulinda uhuru wao.[1]
Petro Njau anaeleza kuwa KCCU kilikuwa, ‘chama cha siasa cha kikabila’.
Hii fikra ya kuwa Kilimanjaro yote ni nchi ni fikra ambayo ilijijenga sana katika kabila la Wachagga. Kwani kila viongozi wa Wachagga walipokuwa na mkutano wa viongozi ukisoma taarifa za mikutano hiyo maneno, ‘nchi’, ‘taifa’, ‘raia’, ‘uchaguzi’, ‘kura’, na ‘utawala’, yanajitokeza katika majadiliano kiasi kura imepata kufananishwa na johari, yaani kitu chenye thamani kubwa.
Petro Njau katika kura anaeleza wazi akitaka ieleweke kuwa kuwa, ‘kura moja kwa mtu mmoja’.
Wachagga walikuwa na bendera, walikuwa pia na wimbo wa taifa na siku maalum ya Wachagga maarufu kwa jina la ‘Chagga Day’.
Petro Njau akimwandikia Mangi Mkuu Thomas Marealle alimfahamisha kuwa kachaguliwa kwake kwa kura za Wachagga ndizo zilizompa heshima ndani ya taifa la Wachagga.''
(Nimenyanyambua kutoka kitabuni)
Ningependa kukufahamisha kuwa Petro Njau alikuwa moja wa waandishi wa Rajabu Ibrahim Kirama mwingine ni Joseph Merinyo.
[1] Kanuni za Chagga Citizens’ Union, Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama.
..very interesting.
..ilikuwaje Petro Njau, na Joseph Merinyo, wakawaelewana na Rajabu Ibrahim Kirama? Nini kiliwaunganisha?
..nje ya shughuli na harakati zake za kueneza Uislamu, Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa mtu wa aina gani?
..lakini hiyo habari ya kusema Wachagga walikuwa mpaka na wimbo wa taifa lao inaweza kuchochea chuki zinazoota mizizi wakati huu dhidi ya hawa ndugu zetu.