Picha kutoka gazeti la Mambo Leo la mwaka wa 1934. Watazame Mangi waliopambana na Rajabu Kirama - Mangi Ngilisho na Shangali

JK,
Hebu angalia haya maneno hapa chini:

''Lakini ukoloni ulikuwa na faida zake, na Rajabu Ibrahim Kirama nyota yake itakuja kunyanyuka na mwanga wake kuangaza sehemu nyingi za Uchaggani, lau kama itakaribia karne moja kabla ya historia kumtambua.

Nyota hii ya Rajabu Ibrahim Kirama itang’ara ilhali Chifu Abdieli anaishuhudia kwa macho yake.

Uhasama huu baina ya Chief Abdiel Shangali aliyekuwa akipambana na Rajabu Ibrahin Kirama kwa ajili ya jitihada zake za kueneza Uislamu Uchaggani taratibu ukapoteza ukali wa nguvu zake kwani Wachagga haukupita muda mrefu wakajitazama upya na kutambua kuwa kwa hakika adui hakuwa nduguye Mchagga Muislam; adui mkuu kwao wote ulikuwa ukoloni ambao ulihitaji nguvu ya pamoja kukabiliana nao.

Katika jitihada hizi za kujiletea maendeleo Wachagga wakaunda Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) Umoja wa raia wa Kilimanjaro.

Petro Njau akiwa kiongozi ili isimamie maslahi ya Wachagga kama taifa.

Katika kanuni za KCCU, zinawataja Wachagga kama watu waliozaliwa huru na wenye haki ya kulinda uhuru wao.[1]

Petro Njau anaeleza kuwa KCCU kilikuwa, ‘chama cha siasa cha kikabila’.

Hii fikra ya kuwa Kilimanjaro yote ni nchi ni fikra ambayo ilijijenga sana katika kabila la Wachagga. Kwani kila viongozi wa Wachagga walipokuwa na mkutano wa viongozi ukisoma taarifa za mikutano hiyo maneno, ‘nchi’, ‘taifa’, ‘raia’, ‘uchaguzi’, ‘kura’, na ‘utawala’, yanajitokeza katika majadiliano kiasi kura imepata kufananishwa na johari, yaani kitu chenye thamani kubwa.

Petro Njau katika kura anaeleza wazi akitaka ieleweke kuwa kuwa, ‘kura moja kwa mtu mmoja’.

Wachagga walikuwa na bendera, walikuwa pia na wimbo wa taifa na siku maalum ya Wachagga maarufu kwa jina la ‘Chagga Day’.

Petro Njau akimwandikia Mangi Mkuu Thomas Marealle alimfahamisha kuwa kachaguliwa kwake kwa kura za Wachagga ndizo zilizompa heshima ndani ya taifa la Wachagga.''
(Nimenyanyambua kutoka kitabuni)

Ningependa kukufahamisha kuwa Petro Njau alikuwa moja wa waandishi wa Rajabu Ibrahim Kirama mwingine ni Joseph Merinyo.

[1] Kanuni za Chagga Citizens’ Union, Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama.

..very interesting.

..ilikuwaje Petro Njau, na Joseph Merinyo, wakawaelewana na Rajabu Ibrahim Kirama? Nini kiliwaunganisha?

..nje ya shughuli na harakati zake za kueneza Uislamu, Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa mtu wa aina gani?

..lakini hiyo habari ya kusema Wachagga walikuwa mpaka na wimbo wa taifa lao inaweza kuchochea chuki zinazoota mizizi wakati huu dhidi ya hawa ndugu zetu.
 
Chief Kidaha wa Usukuma alikuwa na bendera kama Chagga Council.

Tunafanya nini na historia hizi?

Petro Njau na Joseph Merinyo In Shaa Allah nitarejea.
 
..very interesting.

..ilikuwaje Petro Njau, na Joseph Merinyo, wakawaelewana na Rajabu Ibrahim Kirama? Nini kiliwaunganisha?

..nje ya shughuli na harakati zake za kueneza Uislamu, Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa mtu wa aina gani?

..lakini hiyo habari ya kusema Wachagga walikuwa mpaka na wimbo wa taifa lao inaweza kuchochea chuki zinazoota mizizi wakati huu dhidi ya hawa ndugu zetu.
JK,
Umeniuliza ilikuwaje Petro Njau na Joseph Merinyo wakawa na usuhuba na Rajabu Kirama?
Nakunyambulia yale niliyoandikika katika kitabu:

''Mtu anaweza kujiuliza iweje Njau Mkristo akawa upande wa Rajabu Kirama akimsaidia kama mwandishi wake katika masuala yanayohusu Uislam.

Inaweza kuwa ni mvutano katika jamii uliokuwapo baina ya Petro Njau na Joseph Merinyo kwa upande mmoja dhidi ya utawala wa Mangi kwa upande wa pili kwani katika miaka ile Njau na Merinyo walianza kukwaruzana na Wamishionari na serikali ya Kiingereza.

Hii ikawa ndiyo historia ya wao siku zote kuwa upande unaopingana na mamlaka.[1]

Bila shaka ni katika mgongano huu Njau kama njia moja ya kulipiza kisasi dhidi ya Wamishionari na serikali kutafuta haki ya Wachagga wote akawa upande ule wa Waislam alioona kuwa hawapewi haki wanayostahili.

Lakini ukweli ni kuwa Petro Njau alikuwa binadamu mtu ambae katika misha yake yote alisimama upande wa haki.

Historia ya maisha ya Petro Njau kwa mkono wake mwenyewe kwa aliyoyaandika[2] anasema kuwa alimaliza shule mwaka wa 1910 na kupasi vizuri lugha ya Kidachi na akaajiriwa kama mwalimu wa shule ya chekechea.

Wakati ule Wachagga walikuwa na mila ya kuua mtoto wa pili waliozaliwa mapacha.

Mila hii ilimkera sana akawa anapita kutafuta watoto mapacha na kunusuru wale waliokuwa wauawe.

Kazi hii aliifanya na Mjerumani mmoja aliyeitwa Shwester Bertha Shulz wakawa hawa watoto wanapelekwa kulelewa na Wamishionari Moshi.

Hawa watoto walipokua Njau aliwarejesha kwa wazazi wao ambao waliwapokea kwa furaha. Njau alikuwa mtu aliyependa elimu kwa kujua faida yake lakini hakuzifurahia shule za Wamishionari kwa ajili ya ubaguzi wake wa kutoa elimu kwa waumini wao tu.''

[1]Angalia Emma Hunter, ‘’Political Thought and the Public Sphere in Tanzania Freedom, Democracy and Citizenship in the Era of Decolonisation,’’ Cambridge University Press, 2015 p. 119.
[2] Maelezo mafupi ya maisha na kazi za Mzee M. P. Njau (hakuna tarehe), Nyaraka za Mzee Rajabu Ibrahim Kirama.
 
Mi babu yangu mzaa mama alikuwa muislam na mzee mohamed kamtaja humu. Bahat nzur babu yangu alikuwaga mshikaji wangu na nilibahatika kumhoji sana kuhusu uislam na ilikuwaje akawa muislam. Alifariki cku nyingi sana nikiwa na miaka 14. Alikuwa na mafaili mengi sana mpaka leo yapo ila nini kilimfanya awe muislam sio kama mzee muhamed anavyotudanganya hapa. Babu yangu alikuwa anaitwa Ally Nangeda. Ni mkibosho hakuwa mmachame na yeye alifanikiwa kufika saud arabia na nchi nying za kiarabu miaka yake ya ujanani. Kisa kimoja ambacho anijibu ni kwanini aliamua kuwa muislam. Aliniambia miaka ya 1925 alienda moshi mjin. Kule kwenye kuhangaika kwake akakutana na mama mmoja mtu mzima na alimpenda akamtunza na kumpa kila kitu na kumfunza hiyo dini. So ule ukarimu wa yule mama ulimfanya atafakar dini yake na watu wake ambao by then wote ni wakristo. Akaona kwa upendo wa yule mama itakuwa hiyo dini ni ya kweli. Since then mzee akaenda deep. Akazamia tanga mombasa yemen saudia oman alikuja kurud kwao ana wattoto wakubwa. Sasa ana mafile mengi kuhusu hawa jamaa balaa.ameacha watoto wa kutosha. Kaacha mji mwananyamala dar. Kisauni mombasa na tanga na majengo moshi japo aliishi maisha yake ya uzeen kijijin. Watoto wengine wamebadili dini wengine mpaka leo ni waislam. Niishie hapo kwa kifupi.
 
Kitali,
Umeandika vyema na bila shaka yoyote hayo majalada ya babu yetu yatakuwa na mambo mengi muhimu.

Machame Uislam uliingia mwaka wa 1930 babu yetu kaingia Uislam baada ya kwenda Moshi mwaka wa 1925.

Msikiti wa kwanza Moshi Mjini umejengwa 1899 kwa hiyo Uislam ulikuwako na babu yetu kaukuta.

Sijui kwa nini umeniita muongo.
Hili limenisikitisha.

Babu yetu mimi nimemtaja kwa kuwa yupo katika moja ya Nyaraka za Rajabu Kirama nilizozipitia wakati wa utafiti wa kuandika maisha yake.

Mimi nitakuwa vipi nadanganya kwa kunakili kwa wasomaji kile ambacho kipo katika maandishi?

Uamuazi wa hili nawaachia wasomaji.
Angalia hapo chini majina yaliyomo katika nyaraka hiyo:

[1] Taarifa haina jina la mwandishi iliyoandikwa kwa mkono katika karatasi mbili moja ni taarifa na karatasi ya pili ina majina ya wazee 18 tarehe 1 November, 1945 : Mhamed bin Makwini, Sofiani bin Ngelechi, Ali bin Nangeda, Hassani bin Kisamu, Salim bin Choloi, Abubakali bin Tira, Abudian bin Ngelechi, Hamissi bin Mchomba, Salim bin Urawe, Rashidi bin Maimbi, Ali bin Mzuli, Rashidi bin Ngowiya, Salehe bin Mangale, Omali bin Mkenya, Ali bin Tuta, Hassana bin Mangale, Asumani bin Mbonika, Ramazani bin Mota.

Angalia barua ya tarehe 5th November, 1945 kutoka kwa Rajab Kirama, Jamiatu Islam, Machame kwa Sulemani Rajabu inayoeleza kuwa alikwenda na wenzake kwa Mangi tarehe 27th October, 1945 kusadikisha kuwa Kibosho kuna Waislam 500 ambao hawana msikiti kwa hiyo apatiwe kiwanja cha kujenga msikiti, (Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama).
 
Chief nzima hakuna waislam200. Naweza nikakuhesabia na nyumba na misikiti. Cc wanakijiji nakumbuka tuliwasaidia waislam kujenga msikiti mmoja kati ya mitatu iliyokuwepo kibosho. Na kwa taarifa yako. Uislam haukunezwa kibosho bali ni mtu mmoja mmoja alitoka alivyofika mjin akabadili dini. Coz mpaka kufika 1890 kibosho yote ilikuwa chini ya katoliki. Ila Mangi Sina aliyekuwa mtawala wetu yeye kipindi wazungu wako aliagiza walinz kutoka usambaan kuja kumlinda na makaz yao wakaweka kindi ndipo walipokuwepo waislam na by then kule kulikuwa kunaitwa porin. So hao wakuja waliwekwa pale kulinda himaya ya Mangi. Kama nilivyokuambia uislam haujawah kuenezwa moshi ila mtu tu anatoka anarud akiwa muislam ndivyo ilivyo. Na ndio maana watoto wao wengi wamebadili dini. Ungekuwa mtafit mzur ungemjua babu yangu na mzee mmoja anaitwa Amri ngao. Babu yangu alikufaga miaka 1986 na amri miaka 1998. Babu amefariki akiwa na miaka 89.
 
Mimi sina tatizo na haya uliyoandika.

Mimi nimeandika kitabu kutokana na nyaraka alizoacha Rajabu Ibrahim Kirama zenye umri wa miaka 90 sasa.

Ikiwa unayoyajua wewe yanapingana na yaliyomo kwenye nyaraka hizi hii ni kati yako na yale yaliyoandikwa na hao waliokuwapo mwaka wa 1930 hadi Mangi Ngilisho Sina alipoombwa na Waislam ruhusa ya kujengwa msikiti Kibosho.

Nimekuwekea na majibu ya Mangi Ngilisho katika barua yake ya mwaka wa 1945.

Msomaji ni juu yake sasa kuamua.

Mimi sina langu hapo nawasoma Mangi Ngilisho na Rajabu Ibrahim Kirama kwa ushahidi wa barua walizoandikiana.

''Mangi Ngilisho alikuwa ameshalitolea uamuzi mapema suala la kujenga msikiti.

Katika barua kali iliyoandikwa kwa hati ya mkono na kuambatanishwa na karatasi iliyokuwa na majina hayo 18 yameandikwa maneno haya yakieleza msimamo wa Mangi Ngilisho Sina:

Waissiramu walio Kibosho ni 500 waliyokwenda kwa mangi kutaka mahali pakujenga mussikiti walipomuuliza Mangi wao amesema hamwezi kupata hata mkifika kwa District Officer [Afisa Mtendaji wa Wilaya] Moshi na Arusha kwa pissii hamuwezi kupata maana mimi Mangi Ngilisho c/s Sina nimeweka sahihi mbele ya Bwana pissii Arusha wakati nilipovunja mussikiti ule wa kwanza ndipo nilipoweka sahihi kama katika nchi yangu ya Kibosho sitakubali kujenga mussikiti haya ndiyo majibu Mangi aliyowajibu wazee waliopelekwa na jamiaya waissiram wa Kibosho wazee waliyokwenda majina yao ni haya...

[1] Taarifa haina jina la mwandishi iliyoandikwa kwa hati ya mkono katika karatasi mbili moja ni taarifa na karatasi ya pili ina majina ya wazee 18 tarehe 1 Novemba, 1945: Mhamed bin Makwini, Sofiani bin Ngelechi, Ali bin Nangeda, Hassani bin Kisamu, Salim bin Choloi, Abubakali bin Tira, Abudian bin Ngelechi, Hamissi bin Mchomba, Salim bin Urawe, Rashidi bin Maimbi, Ali bin Mzuli, Rashidi bin Ngowiya, Salehe bin Mangale, Omali bin Mkenya, Ali bin Tuta, Hassana nin Mangale, Asumani bin Mbonika, Ramazani bin Mota. Angalia barua ya tarehe 5 Novemba, 1945 kutoka kwa Rajabu Kirama, Jamiatu Islam, Machame kwa Sulemani Rajabu inayoeleza kuwa alikwenda na wenzake kwa Mangi tarehe 27 Oktoba, 1945 kusadikisha kuwa Kibosho kuna Waislamu 500 ambao hawana msikiti kwa hiyo apatiwe kiwanja cha kujenga msikiti, (Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama).

Bwana Kitali bahati mbaya jina la babu yako halipo katika orodha hii kwa hiyo si kuwa mimi ni mtafiti nisiye na viwango ndiyo maana jina la babu yako sikuliona.

Jina la babu yako sikuliona kwa kuwa halipo katika Nyaraka za Rajabu Kirama.
Waliokuwamo wote nimewataja na ukienda kwenye faharasha (index) ya kitabu utawaona.
 
Ferru...
Katika picha hiyo na waliokuwa hai kipindi hiko wako wazalendo wengi walioshuhudia mabadiliko ya TAA na kuundwa kwa TANU mwaka wa 1954.

Katika picha hiyo yuko Ramadhani Mashado Plantan ambae kaka zake wawili walishiriki katika siasa za TAA.

Mwalimu Thomas Saudtz Plantan alikuwa Rais wa mwisho wa TAA katika kizazi cha Wajerumani na uongozi wake ulipinduliwa mwaka wa 1950 na vijana wa enzi za Waingereza wakiongozwa na Abdulwahid Sykes.

Schneider Abdillah Plantan yeye aliungana na vijana katika kuutoa madarakani uongozi wa kaka yake Thomas Plantan.

Ramadhani Mashado Plantan yeye alikuwa mmiliki na mhariri wa gazeti lake mwenyewe Zuhra ambalo ndilo lilikuwa sauti ya TAA na baadae sauti ya TANU na Nyerere.

Alikuwapo pia Mzee bin Sudi yeye mwaka wa 1972 Rais wa Sudan Jaffar El Nimiery alipozuru Tanzania alifika makao makuu ya TANU Lumumba akiwa ameongozana na mwenyeji wake Mwalimu Julius Nyerere.

Mzee bin Sudi ndiyo alisoma risala ya kumkaribisha Nimiery Makao Makuu ya TANU.

Haikupita miezi mingi baada ya sherehe hii Mzee bin Sudi akafariki dunia.
Shukrani sana mzee wangu.
 
Mi babu yangu mzaa mama alikuwa muislam na mzee mohamed kamtaja humu. Bahat nzur babu yangu alikuwaga mshikaji wangu na nilibahatika kumhoji sana kuhusu uislam na ilikuwaje akawa muislam. Alifariki cku nyingi sana nikiwa na miaka 14. Alikuwa na mafaili mengi sana mpaka leo yapo ila nini kilimfanya awe muislam sio kama mzee muhamed anavyotudanganya hapa. Babu yangu alikuwa anaitwa Ally Nangeda. Ni mkibosho hakuwa mmachame na yeye alifanikiwa kufika saud arabia na nchi nying za kiarabu miaka yake ya ujanani. Kisa kimoja ambacho anijibu ni kwanini aliamua kuwa muislam. Aliniambia miaka ya 1925 alienda moshi mjin. Kule kwenye kuhangaika kwake akakutana na mama mmoja mtu mzima na alimpenda akamtunza na kumpa kila kitu na kumfunza hiyo dini. So ule ukarimu wa yule mama ulimfanya atafakar dini yake na watu wake ambao by then wote ni wakristo. Akaona kwa upendo wa yule mama itakuwa hiyo dini ni ya kweli. Since then mzee akaenda deep. Akazamia tanga mombasa yemen saudia oman alikuja kurud kwao ana wattoto wakubwa. Sasa ana mafile mengi kuhusu hawa jamaa balaa.ameacha watoto wa kutosha. Kaacha mji mwananyamala dar. Kisauni mombasa na tanga na majengo moshi japo aliishi maisha yake ya uzeen kijijin. Watoto wengine wamebadili dini wengine mpaka leo ni waislam. Niishie hapo kwa kifupi.
Huyu nangeda nna undugu naye pia japo mimi ni Christian
 
Back
Top Bottom