Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Katika picha hiyo hapo chini aliye hai kadri ya ufahamu wangu ni Mrs. Frank Humplink.
Katika watu hawa saba mimi nimebahatika kukutana na wanne: Mrs. Humplink nimekuwa nikienda nyumbani kwake Lushoto wakati wa uhai wa mumewe, Frank Humplink, Peter Colmore nimezungumza na yeye nyumbani kwake Muthaiga, Nairobi na kwenye simu, Ally Sykes.
Hawa wote ni watu ambao wameninufaisha sana kwa kunieleza historia za maisha yao na mimi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwaandika kama sehemu ya historia muhimu sana ya Tanganyika katika miaka ya 1950.
Waliobakia Fundi Konde na Salum Mapanga sikupata kuwajua kwa karibu ingawa Fundi Konde nimemtaja katika historia ya maisha ya Ally Sykes. Fundi Konde na Ally Sykes wote walikuwa askari katika King's African Rifles na walipigana Burma.
Hawa wote wawili walipata medali za vita kama walenga shabaha hodari na wote walikuwa vijana wanamuziki bingwa walipokuwa vitani Ally Sykes akipiga saxaphone na Fundi Konde akipiga guitar na kuimba.
Baada ya vita Fundi Konde aliporudi Kenya alitunga na kurekodi nyimbo zilizokuwa maarufu Afrika ya Mashariki katika miaka ya 1950 - 1960.
Frank Humplink historia yake ya maisha yake katika muziki ni kubwa na inaungana na historia ya Peter Colmore, Fundi Konde na Eduardo Masengo.
Hawa walikuwa wanamuziki katika bendi aliyounda Peter Colmore iliyoitwa Jambo Boys.
Ukipenda kusoma historia hii ingia hapo chini:
http://mohamedsaidsalum.blogspot.com/.../thepioneer-of...