Wachina bana, kipindi Niko chuo ndo kikuu inaanza, nikawa naagiza hizi Bluetoothspeaker wananitumia zipo poa tu, nikajenga uaminifu na kikuu, kibembe sasa nikaona suti na manguo makali wanauza Bei Chee, nikaagiza suti kama nne na nguo zingine kibao, nikawa nawaringishia washkaj kua zikifika watanikoma
Kibembe siku zinafika nikapigiwa na agent wao maana walikua wanafanya home delivery, Jamaa akaniletea, kibaya npo geto na Hawa washkaji niliokua nawaringishia, aisee kufungua mzigo majamaa walicheka mpaka wakakaa chini
Hawa majamaa sijui wanatumia vipimo Gani, walileta vi suti na vinguo vidogo labda wa kuvaa mtoto wa la 5, nilichukia mno