Picha: Kuwa makini na bidhaa za online

Picha: Kuwa makini na bidhaa za online

Jamani zingine meme tu hizo. Mnashuka povu. Ooh nimeagiza sijui maker nini sijui nshaagiza iphone. Uwongooo bwana uwongo huooo. Nani kawahi agiza kama hivo alete picha.jamaa nae kadownload tu hiyo kaclop
Screenshot_20240319-194124~2.png
 
Mimi ni mtumiaji mzuri sana wa bidhaa za online. Kusema kweli sijawahi kupata tofauti na nilichoagiza.

Sikatai kwamba online kuna vitu visivyofaa, hapana, ila we mwenyewe jiongeze sometime. Mfano unajua kabisa iphone labda ni milioni tatu, we unaipata kwa elf 90 online, jiulize hapo hiyo ni iphone au nini.

Nilichokuja kugungundua watu wengi wananunua bila kusoma product description vzuri, unakuta mtu kanunua toi la baiskel badala ya baiskeli yenyewe.

Online ni sehem nzur sana ya kufanya shoping, cha msingi tu zingatia haya;

1. Nunua kwenye trusted webs au apps, mfano amazon, ebay, aliexpeess etc. website nyingine nyingi kuna phishing huko utakuta card yako imemalizwa hela.
2. Soma product description kwa umakini, kama ni kiatu soma uone material yaliyotengeneza ni ngozi au polyster. Hapo utapata hadi size ya hicho unachotaka kununua.
3. Soma comments za watu waliokwisha kununua hiyo product wanaizungumziaje, utapata mengi sana huko.
4. Soma refund policy endapo umeletewa kitu ambacho ni tofauti na kwenye product description. Mimi sjawahi letewa tofauti na nilivyoagiza, ila nimeshawahi kuwa refunded coz mzigo wangu ulipotea haukunifikia, nikarudishiwa ela yangu.
5. Usione kitu online ukanunua hapo hapo, weka kwenye cart kwanza kipitie, kisome vzuri, endelea kucheki alternatives, unaweza pata kizur zaid kwa bei nzur zaidi. Kwa hiyo usikurupuke. Mimi kununua kitu nachotaka naweza tumia hata wiki nzima
 
Wachina bana, kipindi Niko chuo ndo kikuu inaanza, nikawa naagiza hizi Bluetoothspeaker wananitumia zipo poa tu, nikajenga uaminifu na kikuu, kibembe sasa nikaona suti na manguo makali wanauza Bei Chee, nikaagiza suti kama nne na nguo zingine kibao, nikawa nawaringishia washkaj kua zikifika watanikoma

Kibembe siku zinafika nikapigiwa na agent wao maana walikua wanafanya home delivery, Jamaa akaniletea, kibaya npo geto na Hawa washkaji niliokua nawaringishia, aisee kufungua mzigo majamaa walicheka mpaka wakakaa chini

Hawa majamaa sijui wanatumia vipimo Gani, walileta vi suti na vinguo vidogo labda wa kuvaa mtoto wa la 5, nilichukia mno
Sio tatizo Lao ni lako
 
Back
Top Bottom