Picha: Kwa mtu aliye mgonga Twiga kama hivi faini yake huwa bei gani?!

Picha: Kwa mtu aliye mgonga Twiga kama hivi faini yake huwa bei gani?!

Wakuu, naaamini humu kutakuwa na wajuzi watakaoweza kujibu swali langu hili.

Kama umegonga Twiga kama inavyoonekana hapo pichani, faini yake huwa ni shingapi?

Hii picha nimekutana nayo huko X na imenipa maswali mengi.

Na hiyo hela ukishalipa inaenda kwa familia ya Twiga kama fidia au inaenda wapi?

Fuso kopo sana,yaani ndo imebonyea hivyo!?
 
Twiga yuko nyumbani kwake. Njia inakatiza uani kwenye nyumba ya twiga.
Hizi sheria, basi tu unakuta mnyama pori ana haki kuliko binadamu, Kuna jamaa aliwahi kugonga Swala akamuweka ndani ya gari aisee nilimshangaa sana maana angedakwa hapo unaweza kusikia anafungwa miaka ya kutosha
 
Angefungwa huyo. Hukumbuki yule mama alikula mvua kwa kukutwa na nyama ya swala? Nafikiri aliachiwa baada ya watu wa haki za binadamu kuingilia.

Hizi sheria ni kwa ajili ya kulinda hawa wanyama vinginevyo wataisha. Ni sheria ndani ya eneo la hifadhi. Nje ya hifadhi hakuna hizi sheria.
 
Back
Top Bottom